Wote tunajua katika ulimwengu wa kiislamu Mungu hawezi kua na mtoto. Yuko mbali sana, ni Mtakatifu sana, haiwezekani kueleweka kibinadamu na hata kimapokeo haina maana, wapo hata wakristo wengine ambao wanapata shida tunaposema Yesu ni mwana wa Mungu. Lakini mawazo yote haya yabadilishi ukweli kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.
Ukweli huu ninaoutoa hapa chini haupingiki.
●Huu ni uthibitisho ambao unajulikana sana.
Yohana 1:1 "__Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
na ili kukuelewesha zaidi..soma msitari hapa chini
Yohana 1:14__"Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli."
●Katika Yohana 10:29-30 Yesu mwenyewe anasema kuwa yeye na Mungu ni wamoja
Yohana 10:29-30__"29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
30 Mimi na Baba tu umoja."
Maneno haya yaliwafanya wale wasioamini watake kumpiga mawe Yesu, kwasababu ya kutokuamini kwao
●Kitabu cha Waebrania 1:8 kinasema "
Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Mungu hapa anamuita Yesu mwana wake "Mungu" ambapo tukirudi nyuma inaonekana pia katika Zaburi 45:6-7
●Pia katika Waebrania 1:6 Mungu anasema "Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu."
Hili linathibitisha kuwa Yesu ni Mungu na na malaika wote wa Mungu wamsujudu.
●Biblia inafundisha kuwa Mungu ndiye ahukumuye katika (1Samweli 2:10, Zaburi 50:6 na vifungu vingine vingi).
Hata Yesu naye pia ni hakimu katika (Yohana 5:22; 27, Yohana 9:39, Matendo 10:42 na 2Timotheo 4:1)
Kwahiyo Yesu ni Mungu.
Kwahiyo nawambia, katika kila kona kwenye Biblia, hitimisho moja tu ndilo linawezekana kuleta maana halisi ya vifungu vyote hapo juu vikiwekwa pamoja, nali ni...
Yesu ni Mungu
Yesu ni mwana wa Mungu.
Ukweli ni kwamba Yesu ni Mungu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ukweli kwa mujibu wa isiyokuwa uislamu.
Kwa mujibu wa uislamu ukweli kwamba sio Mungu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Unapingana na Biblia:
Mathayo 27:
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?