Nioneshe hiyo aya. Siwezi kukubaliana na kitu kutoka kichwani mwako tu.
Halafu naona unakwepa maswali yangu, hauna majibu au haufahamu? Pia umekwepa kuchambua maswali yako na kuja na mojamoja umeamua kuja na lingine jipya kabisa kila post.
Kwa ugeni wa majadiliano namna hii, kweli ni mimi ni mgeni, nilianza kujadiliana mtandao wa yahoo groups mwaka 2005 na Jambo forums mwaka 2007 na Jamii forums toka ianzishwe. Uzoefu wangu ni mdogo sana kama uonavyo.
Wewe mwenzangu mwenye uzoefu naona unarukia hili unaacha njiani kabla hatujamalizana unarukia lile unaacha, ukiulizwa maswali hujibu.
Unaonesha ni mzoefu sana wewe wa mijadala.
Aya inayoashiria mkono na sio kiganja hii apa
وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
[ AL - MAIDA - 38 ]
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Aya imetaja AYDIYAHUMAA ni jam'u Ya YADU
na wala aya haikuitaja KAFFUN kwa maana ya kiganja.
Sasa hii aya mtume aliwakata watu viganja na Qurani imesema Mkono,unasemaje hapo my mother?
Kuhusu maswali yako.nilijibu labda hukuona.
Narudia kwa kurekebisha zaidi.
Kuhusu KUKUsanywa kwa hadithi wakati wa uhai wa mtume wA Allah.kwanza kabisa hadithi ni mafundisho ya mtume iwe vitendo,ama maneno yake.kwa maana akisema neno mtume kwa sisi tunaita hadithi .
Sasa kukusanywa kwa hadithi wakati wa mtume kams unakusudia kuzikusanya zote basi haiwezekani kuzikusanya zote kwa sababu bado mafundisho yalikuwa yanaendelea kwa kuwa mtume alikuwa hajafa.sasa ilikuwa likisemwa neno la mtume wapo ambao waliandika katika masahaba.
Mfano tu
Kulikiwa kuna Kitabu cha Hadiyth kilichoandikwa na Ibn ‘Amr (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kinajulikana kama Swaadiqah الصادقة . Khalifah ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) pia alikuwa na nyaraka zilizoandikwa Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hukumu za Sheria.
Hawa ni masahaba ambao walimuona mtume na wakachukua mafundisho kutoka kwake.lakini haina maana walizikusanya hadithi zote kwa sababu kila sahaba alisuhubiana na mtume kwa namna yake,kwa hyo kila sahaba alikuwa ana zijua hadithi huwenda sahaba mwingine asiijue hadithi hiyo.
Wakati wa kutekwa Makkah kwa amani, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoa hotuba. Al-Bukhaariy anaripoti kuwa kwa maombi ya Abu Shah (Radhiya Allaahu ‘anhu), Swahaba kutoka Yemen, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru hotuba hiyo aandikiwe.
Mtume wa Allah aliamuruhu hotuba hiyo iandikwe kuonyesha kwamba suala la kuandika lilikuepo wakati huo.
Lakini pia katika sulhu ya udaybiya ile mikataba iliandikwa katika makaratasi.na barua mbali mbali ambazo alizituma mtume kwenda kwa viongozi mbali mbali pia ziliandikwa.
Sasa unaposema kukusanya zilikusanywa lini naweza kukuambia zilianza kukusanywa tokea wakati wa Mtume huo huo kwa kuwepo baadhi ya masahaba wakiandika maneno yake na huko ni kukusanya.
Ama unakusudia kusema kwamba kukusanywa kulikamilika lini?
Mfano tukisema siku ya kusmza kukusanya kura za wananchi na siku zimekamilika kukusanywa hayo ni mambo tofauti.
Nadhani nimekujibu kama sijssahau.
ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha