Sasa na wanao vutia bangi kibera unasemaje maana kibera ni zaidi ya chooni ,ukiingia chooni uwezi kutoka umemwagiwa kinyesi Ila tembea kibera chini una kanyaga kinyesi juu unakutana na fly toilet ,na wakenya wanavita bangi hapo tutegemee kupata vichaa ++
Kwanza kabisa umetumia lugha isiyofaa kabisa kuelezea sehemu wanayoishi binaadam wenzio. Sidhani kama wanapenda kuishi hivyo bali ni mazingira na kutengwa tu kuliwafanya wawe hivyo.
Afrika leo hii hatuna cha kujivunia isipokuwa Uafrika wetu na umoja wetu. Kitachotuokoa kutoka namna tulivyowekwa na ukoloni ni kufuta matabaka na mtenganisho aliotuwachia mkoloni.
Kibera ni neno la Kinubi linalomaanisha pori. Kibera ni moja ya vielelezo vya mtenganisho wa mkoloni. Ukiisoma Historia ya Jiji la Nairobi utagundua kuwa Kibera ilikuwa ni pori ambalo Wakoloni walilitoa sehemu na kuwaweka askari wa Kinubi waliorudi vitani. Kwanini wapewe pori? Ni kuwatenganisha tu na wengine (divide and rule).
Lakini kitu chema walichofanya hao Wanubi waliopewa eneo hilo ni kuuvunja mwiko wa wakoloni na kumkaribisha yeyote ajae hapo Kibera. Ndiyo maana leo hii utakuta Kibera wanaishi makabila yote na wote wanaotengwa na jamii.
Wanubi walioanza kuishi Kibera ni mfano mzuri wa kuigwa si Kenya tu, bali na Afrika nzima. Ni Kibera ambapo makabila yote na dini zote za Kenya yanaishi bila kubaguana. Kama unajuwa uhasama wa kikabila uliopo Kenya kutokana na fitna za kutenganishwa na mkoloni basi kwanza ungepasifu Kibera.
Na pia kama ungefahamu kuwa Kenya ardhi inamilikwa na watu lakini Wanubi waliomilikishwa Kibera walilifumbia macho hilo na kumkaribisha kila ajae, kumbuka kuwa wengi wa wanaoishi Kibera walikimbilia hapo kwa matatizo ya kukosa pa kuishi na kushindwa kumiliki ardhi karibu ya jiji.
Nani asiependa kukimbilia sehemu ambayo haina ubaguzi? Hilo ndilo lililopelekea Kibera kuwa na watu wengi na miundo mbinu duni.
Tuwasifu Wanubi waliokaribisha wakuja hapi kwao. Na kwa sasa tuipongeze serikali ya Kenya kwa kuanza kuchukua hatua za kupaweka sawa Kibera.
By the way, Wanubi hao walipelekwa kupewa ardhi porini (siku hizo ni nje ya mji na siyo kama sasa pamekuwa katikati ya jiji) kwa kuwa walikuwa 100% Waislam, walitengwa. Lakini Alhamdulillah hilo ni fundisho tosha kutoka kwa Waislam kwa kutowatenga na kupokea makabila na dini zote bila kuwabagua.
Uchafu hata Dar upo. Pamekuwa pachafu sana baada ya wimbi la wakuja kuhamia bila mpango. Kama ilivyokuwa Kibera, wenyeji wa Dar, hakuna ataepinga kuwa ni Waislam, hawakubagua.
Ma shaa Allah.