Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Naona bi FaizaFoxy kaenda mitini

Sent using Jamii Forums mobile app

Usiwe na papara kijana. Kuwa na imani na subira.

Salat ni nguzo muhimu sana ya Uislam inataka majibu yenye uhakika.
Qur'an 2:
2_153.gif

153. Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. 153
 
@FaizaFoxy kwakuwa adhan ni wito ama "tangazo" la kuita watu kuswali,. "tangazo" hilo linatolewa kwa taratibu maalum kwa hiyo nipo sahihi nikisema adhan (tangazo) la kuita watu ktk salat lina taratibu zake za namna tutakavyoitana.

nakusudia siyo yeyote anaweza kwenda mahali pa kuswalia na kutoa adhan (tangazo) kwa namna anayoijua yeye,. zipo taratibu za kufuata na ipo namna ya kutoa "tangazo" hilo.

sasa basi taratibu hizo zinafuatwa kwasababu alizianzisha nani?

(rejea za mwanzilishi wa taratibu hizo tafadhali)

Sent using Jamii Forums mobile app
Adhan (Kiarabu: أَذَان [ʔaˈðaːn]), iliyoandikwa pia kama Adhaan, Azan, Azaan au Athan, pia huitwa Ezan kwa Kituruki, ndio wito wa Kiislam kwa sala, unaosikika na mu'azzin kwa nyakati zilizowekwa za siku. Mizizi ya neno ni ʾadhina أَذِنَ inamaanisha "kusikiliza, kusikia, kupewa habari juu ya". Jingine linalotokana na neno hili ni ʾudhun (أُذُن), linamaanisha "sikio".

Kwa kuwa tumekubaliana kuwa adhan (mwito) wa kukumbusha wakati wa salat ilikuwepo na upo kwenye Qur'an basi hakuna tatizo lolote ikiwa umefanyika utaratibu mwito huo uwe vipi. Mradi haupingani na Qur'an.

Naomba uelewe kuwa mwito wa adhan siyo moja ya nguzo za salaat (not obligatory) na itaponadiwa si lazima kuwe na sala na pia ikiwepo au isiwepo adhan basi haivunji sala.

Pia elewa kwa kuwa adhan ni mwito wa kukumbushana kuswali, leo hii kwa bahati mbaya kabisa mapokeo mbali mbali ya wanazuoni kuhusu adhan yanatofautiana na adhan zinatofautiana kati ya madheheb na madheheb ya Kiislam. Tofauti za namna ya adhan itolewe vipi na pia hata baadhi ya maneno ya adhan yanatofautiana. (Binafsi pia kuwepo na madhehebu katika Uislam sikubaliani napo kabisa, hii nje ya mada hii).

Kwa hiyo adhan ipo ndani ya Qur'an vipi iitwe hilo si tatizo na ni njema sana ikifatwa kwani licha ya ukumbusho wa kuswali pia ni ukumbusho wa "shahada" ambayo ndiyo nguzo ya Kwanza katika Uislam.

Kwa bahati mbaya mpaka leo hii viwango vizuri vibavyokubalika na Ummah wote wa Kiislam hatuna. Inabidi kazi kubwa ifanyike kiwango aina moja cha adhan kiwepo kwa Waislam wote.

Kwa historia ya sasa ya Kiislam taratibu hizo zilianzishwa kwa ndoto ya Abdullah bin Ziyad na Mtume Muhammad (PBUH) hakulipinga hilo na akamteua Muadhin kuwa Bilal Ibn Rabah.
 
Nam ukhtyi nimesoma post hyo kuna aya umezibainishya kuwa sala ilikuepo hapo kabla ila hakuna idadi ya rakaa na hakuna kuwa kuna sala ya ijumaa kuwa ni rakaa ngapi.asa kwa kuwa sala ilikuepo tokea hapo lazima pia ilikuwa na idadi ya rakaa na kwa kuwa sala ya ijumaa imetajwa kwenye Qurani bila shaka lazima iwe sala maalumu yenye mavitendo maalum na rakaa maalum.
Ndo mana nikauliza sala ya ijumaa kwa mujibu wa Qurani pekee ina idadi ya rakaa ngapi,na sala ya ijumaa ina idadi ya rakaa ngapi?
NAKUBALIANA NAWE KUWA SALA ILIKUEPO HAPO KABLA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuwa salat ni jambo muhimu sana katika Uislam na kwa kuwa maswali yote yanahusu salat. Naomba uliza moja moja ili niweze kutoa majibu ya uhakika kwa kila kipengele.

Maana kuna salat aina kadhaa zimetajwa kwenye Qur'an kuna salat ambazo hazikuwepo kabla ya Mtume Muhammad (PBUH) na kuna salat ambazo zilikuwepo kabla ya Mtume Muhammad (PBUH). Naomba twende taratibu.
 
"Kwa historia ya sasa ya Kiislam taratibu hizo zilianzishwa kwa ndoto ya Abdullah bin Ziyad na Mtume Muhammad (PBUH) hakulipinga hilo na akamteua Muadhin kuwa Bilal Ibn Rabah."

naomba unijuze maelezo hayo niliyo 'copy' kutoka ktk post yako hiyo wewe uliyapata katika 'historia' aliyokusimulia nani?

Mbona historia zipo nyingi sana na zote zinazoitwa "hadith za Mtume" in fact hizo siyo hadith za Mtume bali wana historia wameandika kwa kuhadithiwa na wengi tu. Msome Bukhari, msome Muslim na wengine (sijui kama umewahi kuwasikia) kina Sayyid Ibn Taus, Allamaha Hilli na pia Msome Shaikh Al Albani kaingia deep kuhusu Adhan mpaka zingine kasema ni "bidaa".

Huyo uliyemuita safuher mpaka leo kashindwa kuleta Ayat za Qur'an zinazoongolea "adhabu ya kaburi" alizoahidi kuleta. Na hii ni open challenge kwake kwa kuwa kaahidi na mwenzake pia aliahidi anajiita Zurri na mwengine yeyote anaejuwa kuwa zipo aje amwage darsa. Mimi nasema hakuna.

Unaweza pia kuwasaidia kama na wewe unaamini zipo.

Nnakushangaa sana, kwani watu walioizulia Qur'an na walioahidi kuleta ayat za Qur'an na hawazileti hauwaulizi chochote kuhusu hilo, unaniulza na kunifanyia "scrutiny" mimi nnaewapa jibu ya kila swali lenu. Ajiib.
 
"Nnakushangaa sana, kwani watu walioizulia Qur'an na walioahidi kuleta ayat za Qur'an na hawazileti hauwaulizi chochote kuhusu hilo, unaniulza na kunifanyia "scrutiny" mimi nnaewapa jibu ya kila swali lenu. Ajiib."

huna haja ya kunishangaa kwakuwa muanzilishi wa 'thread' hii ni wewe na maudhui ya 'thread' ni maswali kuelekezwa kwako na pia majibu utoe wewe kwa yale ambayo unayaweza, pia yale usiyoweza wengine wenye ilmu nayo watayajibu.

Zurri na safuher wao niwaulizeje hali ya kuwa siyo wenye 'thread'?

usisahau kuwa hata wewe ulishaniambia kuwa 'yangu kwao technically siyo maswali'

Unapenda sana kunitaja bibie. Ungekuwa unajibu maswali ingekuwa bora zaidi.

Kwa haya maelezo yako unaonyesha ni kwa jinsi gani huzijui hadithi za mtume achilia mbali elimi yenyewe ya hadithi.

Hadithi za mtume ni yale masimulizi kufikia kwake mtume. Hadithi za mtume zina sehemu mbili nazo ni sanadi na matini. Masimulizi hayo ndio huitwa hadithi.

Imwam al Bukhari na Imaam Muslim hawa ni miongoni mwa wanazuoni maarufu walio kusanya hadithi za mtume. Soma "Muqadimmah fi Sahihi Muslim" utangulizi wa sahihi muslim. Hawa hawakumdiriki mtume wa Allah,kwahiyo walikuwa wanashughulika na sanadi ya masimulizi ifike mpaka kwa mtume na matini zake. Hizi ndio hadithi. Sasq unapokataa hadithi hali ya kuwa hujui hadithi ni nini huu ni uhayawani ns unaihujumu elimu. Tqngu mwanzo nilijua tu wewe huzijui hadithi za mtume.

Umemgusia Imaam al albaniy,huy ni mwanazuoni bingwa wa hadithi habari zake zimetangaa na Allah amempa kabul sana. Huyu ameishi katika elimu ya hadithi na kazi zake zinathibitisha hilo. Imaam al Albaniy anazikubali hadithi,na ukiona anaongelea jambo fulani ni "bidaa" ujue anarejea katika mafundisho ya mtume na hadithi za mtume. Imaam al Albaniy amekufa kabla ya kukimaliza kitabu chake kiitwacho "Sahihi siirat an Nabiy" kitafute uoe alivyo pita na alivyo nukui hadithi za mtume.

Sasa inakuwaje unazikataa hadithi za mtume hali ya kuwa huzijui na hujui nini maana ya hadithi ? Nilikuuliza jana unitajie vitabu japo vitatu tu ulivyo visoma vya historia ya mtume ambavyo havina hadithi zake. Hujataja mpaka muda huu.

Hitimisho langu ni kuwa,ndio maana maswali yangu marahisi huwa unashindwa kuyajibu sababu huna elimu wala hujui hadithi za mtume ni nini ?
 
Huyu bi mkubwa anakataa hadithi za mtume,hali ya kuwa neno lenyewe Hadithi hajui lina maanisha nini katika ulimwengu wa Elimu ya Hadithi.
 
Mbona historia zipo nyingi sana na zote zinazoitwa "hadith za Mtume" in fact hizo siyo hadith za Mtume bali wana historia wameandika kwa kuhadithiwa na wengi tu. Msome Bukhari, msome Muslim na wengine (sijui kama umewahi kuwasikia) kina Sayyid Ibn Taus, Allamaha Hilli na pia Msome Shaikh Al Albani kaingia deep kuhusu Adhan mpaka zingine kasema ni "bidaa".

Huyo uliyemuita safuher mpaka leo kashindwa kuleta Ayat za Qur'an zinazoongolea "adhabu ya kaburi" alizoahidi kuleta. Na hii ni open challenge kwake kwa kuwa kaahidi na mwenzake pia aliahidi anajiita Zurri na mwengine yeyote anaejuwa kuwa zipo aje amwage darsa. Mimi nasema hakuna.

Unaweza pia kuwasaidia kama na wewe unaamini zipo.

Nnakushangaa sana, kwani watu walioizulia Qur'an na walioahidi kuleta ayat za Qur'an na hawazileti hauwaulizi chochote kuhusu hilo, unaniulza na kunifanyia "scrutiny" mimi nnaewapa jibu ya kila swali lenu. Ajiib.
'historia' ambazo ndani yake yapo mafundisho nayo tunayafuata mfano ni namna ya kuadhini.,

taratibu za kuadhini, namna ya kuadhini kadhalika lugha ya kutumia wakati wa kuadhini, pia ni nani aadhini je Quran imeelekeza mambo hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'historia' ambazo ndani yake yapo mafundisho nayo tunayafuata mfano ni namna ya kuadhini.,

taratibu za kuadhini, namna ya kuadhini kadhalika lugha ya kutumia wakati wa kuadhini, pia ni nani aadhini je Quran imeelekeza mambo hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo nimeshakujibu juu kidogo,soma post namba 3152.
 
Unapenda sana kunitaja bibie. Ungekuwa unajibu maswali ingekuwa bora zaidi.

Kwa haya maelezo yako unaonyesha ni kwa jinsi gani huzijui hadithi za mtume achilia mbali elimi yenyewe ya hadithi.

Hadithi za mtume ni yale masimulizi kufikia kwake mtume. Hadithi za mtume zina sehemu mbili nazo ni sanadi na matini. Masimulizi hayo ndio huitwa hadithi.

Imwam al Bukhari na Imaam Muslim hawa ni miongoni mwa wanazuoni maarufu walio kusanya hadithi za mtume. Soma "Muqadimmah fi Sahihi Muslim" utangulizi wa sahihi muslim. Hawa hawakumdiriki mtume wa Allah,kwahiyo walikuwa wanashughulika na sanadi ya masimulizi ifike mpaka kwa mtume na matini zake. Hizi ndio hadithi. Sasq unapokataa hadithi hali ya kuwa hujui hadithi ni nini huu ni uhayawani ns unaihujumu elimu. Tqngu mwanzo nilijua tu wewe huzijui hadithi za mtume.

Umemgusia Imaam al albaniy,huy ni mwanazuoni bingwa wa hadithi habari zake zimetangaa na Allah amempa kabul sana. Huyu ameishi katika elimu ya hadithi na kazi zake zinathibitisha hilo. Imaam al Albaniy anazikubali hadithi,na ukiona anaongelea jambo fulani ni "bidaa" ujue anarejea katika mafundisho ya mtume na hadithi za mtume. Imaam al Albaniy amekufa kabla ya kukimaliza kitabu chake kiitwacho "Sahihi siirat an Nabiy" kitafute uoe alivyo pita na alivyo nukui hadithi za mtume.

Sasa inakuwaje unazikataa hadithi za mtume hali ya kuwa huzijui na hujui nini maana ya hadithi ? Nilikuuliza jana unitajie vitabu japo vitatu tu ulivyo visoma vya historia ya mtume ambavyo havina hadithi zake. Hujataja mpaka muda huu.

Hitimisho langu ni kuwa,ndio maana maswali yangu marahisi huwa unashindwa kuyajibu sababu huna elimu wala hujui hadithi za mtume ni nini ?
Acha porojo. Nisome tena. Hakuna hadith za Mtume Muhammad, kuna hadith za wanazuoni wanahadithia kuhusu Mtume Muhammad na mengi mengineyo.

Msimzulie Mtume.

Al Albany hadith zilizohusishwa na Mtume kuwa sahihi nyingine alishazipangua kuwa hizo ni uzushi tu. Moja wapo ni hiyo ya adhan zingine. Unaijuwa adhan ipi hiyo kasema ni "bidaa'?

Porojo ndeeeefu haina kichwa wala miguu.

Nakuvuta dana ili ulete uzushi wako uliotaka kuizushia Qur'an. Au uombe toba mbele za watu kuwa huo upuuzi haupo kwenye Qur'an au sitokuacha. Kumbuka hilo.
 
Huyu bi mkubwa anakataa hadithi za mtume,hali ya kuwa neno lenyewe Hadithi hajui lina maanisha nini katika ulimwengu wa Elimu ya Hadithi.
Hadith hata za alfu lela u lela ni hadith au unataka kulipa neno hadith maana mpya?
 
Acha porojo. Nisome tena. Hakuna hadith za Mtume Muhammad, kuna hadith za wanazuoni wanahadithia kuhusu Mtume Muhammad na mengi mengineyo.

Msimzylie Mtume.

Al Albany hadith zilizohusishwa na Mtume kuwa sahihi nyingin alishazipangua kuwa hizo ni uzushi tu. Moja wapo ni hiyo ya adhan zingine. Unaijuwa adhan ipo hiyo kasema ni "bidaa'?

Porojo ndeeeefu haina kichwa wala miguu.

Nakuvuta dana ili ulete uzushi wako uliotaka kuizushia Qur'an. Au uombe toba mbele za watu kuwa huo upuuzi haupo kwenye Qur'an au sitokuacha. Kumbuka hilo.

Hivi kwanini hujibu maswali yangu ?

Kama hakuna hadithi za mtume kuna nini ?

Al Imaam al albaniya,ana vitabu vingi sana,nakukumbusha tu ana kitabu kiitwacho "As Silsila ahadithi Sahih" na "Silsila ahadith Dhaif".

Hadithi za mtume maana yake ni masimulizi aliyozungumza mtume na kauli zake,kipindi akiwa hai. Masimulizi haya yamekuwa ni yenye kurithishwa mpaka yametufikia hapa leo hii.

Naona umetumia tamko "Bidaa" tamko hili unalikuta katika hadithi za Rasul.

Lakini,ungesoma historia ya ukusanywaji wa hadithi za mtume usingekimbia maswali ninayo kuuliza zaidi ungekiri tu ukweli.

Nakuuliza swali sasa,naomba ulijibu swali hili,unaposema wanazuoni wanahadithia kuhusu mtume,wao wanakuwa wameyapata wapi hayo masimulizi ? Sasa kile kinachosimuliwa kuhusu mtume kibakuwa cha Mwanazuoni au cha mtume ? Usiwe mjinga kiasi hicho,yaani unajichanganya sana.

Sasa wanazuoni wanachokisimulia kinaitwaje ? Bila shaka yanaitwa masimulizi ya mtume,yaani hadithi za mtume,wewe bdio unashika bendera ya wajinga na vilaza wote humu jf. Yaani unazikataa hadithi kwa kauli ila unazikubali kivitendo.

Wanazuoni wanakuwa wamenasibishwa kwazo sababu wao wamezikusanya ila ni hadithi yaani masimulizi ya mtume. Nilikuuliza huko nyuma nini maana ya Hadithi hukujibu. Sasa ifike wakati uwe na adabu bibie,haya mambo huyajui lakini unakalia ubishi na ujinga.
 
Hadith hata za alfu lela u lela ni hadith au unataka kulipa neno hadith maana mpya?

Nakufundisha sasa,tamko Hadithi kilugha ni Habari au masimulizi au jambo jipya, ila kiistilahi katika ulimwengu wa Kiislamu,hadithi ni masimulizi khasa ya mtume,ama kauli au vitendo.
 
kwa maana hii bibi., Qur'an siyo maneno ya M/Mungu tuseme ni maneno ya mtume aliyoambiwa na M/Mungu.

ni sahihi kusema hivyo?

Back
Top Bottom