Fainali kombe la Mapinduzi, Simba zaidi ya uijuavyo

Fainali kombe la Mapinduzi, Simba zaidi ya uijuavyo

Simba isiyo na golikipa! He sasa sheria inaruhusu kucheza bila golikipa? Wewe usije kuwa unazungumzia mashindano ya kugombea kuku mtaani kwenu. Hii tunazungumzia kombe la Mapinduzi ya Kumng'oa Sultan Jamseed kule Zanzibar ambayo yalishirikisha timu nyingi zikiwemo KCC ya Uganda na Yanga (ambayo bahati mbaya ni kuwa imeonyesha kiwango duni kama timu ya daraja la tatu sijui kwa nini, labda njaa) ambazo zote kwa nyakati tofauti zilishaondoka.

Pale golini kuna mtu, siyo golikipa, huenda hulijui hilo, subiri masaa mawili yajayo utapata jibu lako.
 
mechi saa mbili na nusu usiku simba chama funga hao sukari kama yanga
 
Hatua hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kuwaadabisha wale wote wasiozingatia mikataba. Kukuhakikishia kuwa Yanga hatuna njaa kama ninyi nenda pale TFF ukaone kuna Miloni 200 za udhamini wa Azam TV zimerundikana pale kwa jina la Yanga halafu hazichukuliwi wakati ninyi mmekula kila kitu na mnatamani hata hizo mpewe; ongeeni na TFF wakikubali chukueni tu.

Wangekataa mechi zao zisirushwe live na Azam Tv kama hawakutaka hizo pesa. Sasa inakuwaje mnawakamua kina Kaseja, Jaja na Okwi! Njaa mbaya sana.
 
Wangekataa mechi zao zisirushwe live na Azam Tv kama hawakutaka hizo pesa. Sasa inakuwaje mnawakamua kina Kaseja, Jaja na Okwi! Njaa mbaya sana.

Hujanielewa, huenda wewe ni slow learner kitu ambacho siyo kosa lako. Kila la heri Mtibwa Sugar.
 
jamani kama tbc wanaonesha mnitaarifu mapema, sitaki kumaliza bando kwa sababu ya mabonanza hapa...
 
Naona wana Yanga wote leo wanatafuna miwa kupooza machungu ya mtani jembe. Simba ni shiiiidaaaaaaaaa.
 
Duh! muda aufiki tu! nipo sebuleni nakunywa kahawa kusubilia mtanange, Nina hamu kama namsubilia demu mpya gheto!
 
Hujanielewa, huenda wewe ni slow learner kitu ambacho siyo kosa lako. Kila la heri Mtibwa Sugar.
Mkuu nina kaswali kangu kadogo tu kakizushi hivi ingetokea Simba wangecheza na Azam fainali ungekuwa upande gani?
 
Mkuu nina kaswali kangu kadogo tu kakizushi hivi ingetokea Simba wangecheza na Azam fainali ungekuwa upande gani?

Umelenga haswa Mkuu! Kwa jinsi nisivyoipenda Azam, ningeshangilia Mikia japo ni kwa siri sana kwa hofu ya 'wayahudi'. Simba siichukii bali ni watani wetu, kikwetu tunawaita 'Bhaphughu'.Azam naichukia absolutely, hata chapati huwa sili, juice sinywi, Azam TV siangalii na bidhaa zake zote situmii. Sasa hivi nina changamoto moja tu: sehemu ya kodi anayolipa SSB naipokea kama mshahara, natafuta ufumbuzi nitambue ni kiasi gani ili nisiwe naichukua hiyo pesa, itasaidia watoto yatima. Ni hayo tu Mkuu wangu.

Kila la heri Mtibwa Sugar a.k.a Libolo FC la Bongo.
 
Back
Top Bottom