Fainali Uzeeni!....

Fainali Uzeeni!....

...WoS, umezungumzia suala la maana sana sana sana mydear...ni ukweli usiopingika katika post zote humu ndani, ni MTM pekee aliyegusia suala la ndoa na maisha ya uzeeni,...very strange!....

..ama kuna haja kubwa ku invest mapenzi kwa mke/mume jamani...
Ni Mke/Mume pekee atayekustiri uzeeni!

Siyo siri mmoja wa wale niliowatumia hili bandiko ni mwenza wangu!

Nimefurahi kuona hata naye limemkuna, akaniandikia kwa kirefu sana and I was so moved!!

Thanks again.
Nawatia moyo na wengine humu mfanye hivyo hivyo..
Mtashangaa jinsi mada hii inavyoweza kuwasha moto wa uhusiano mwema na mazungumzo mazuri!!
 
........Sasa Mbu tukitoka kule kwenye generals......nadhani hili ulilooanisha hapa ni la msingi kuliko kuwekeza kwenye majumba na mashamba na elimu za watoto....Mwenzi wako!! Unawekezaje kwa mwenzi wako kwa maisha ya pamoja uzeeni?........nafikiri tukiliwaza hili na kulitilia maanani hata maumivu ndani ya ndoa huwenda yajapungua...maana wajiandalia list ya vitu au matendo ya uwekezaji. Mie nawekeza kwa spouse wangu kipenzi ili hata tukizeeka basi atazeeka nami kwa furaha na memories njema nyingi zaidi ya zile mbaya......... !!

Mbu ninaomba msaada wa list ya vitu ambavyo one can use/do tu invest for uzee na mwenzi wake!!
Baba/Mama anapokuwa na nyumba ndogo/kidumu hadharani, huwa anakuwa na mawazo ya who's going to be with him/her uzeeni?

...Genius!...maswali yako yamekaa kimtego mtego,...mtu akikurupuka na jibu la hovyo hovyo anakuwa amejichongea.
Mwj1...katika suala hili, naomba Nyumba ndogo/Serengeti Boys/Vidumu etc vilaaniwe kwa nguvu zote!

Hamna kitu mbaya kama kwenye old age unajikuta moyoni una madonda ya 'mke wangu/mume wangu' alini cheat na fulani...hiyo ni sumu...ndio maana binafsi sitaki hata kuifikiria hiyo scenario. Madhali umeiulizia, naomba kukujibu kwamba...hali hiyo hata kama mtakuwa mmesameheana, bado itakuwa ni kovu pale watoto watapokuja kuwataka ushauri wa ndoa zao zitapokuwa zimekubwa na misuko suko ya aina hiyo. Old memories zitajirudia tu...

Sidhani kama itakuwa rahisi ku list down mambo mnayostahiki kuyajengea msingi wa maisha yenu (mpaka kifo kitapowatenganisha) kwani mambo yenyewe ni haya haya kila siku mnayofanyiana. Kuheshimiana, kusaidiana, kuoneana huruma, kupendana, kusameheana, kuongea, kusikilizana na kuelewana, kukubaliana, kupeana subira,...kujaliana,...nk nk nk...

Iwapo maishani mwenu mtajijengea hayo tajwa, na mkafanikiwa kuendelea hivyo hivyo mpaka uzeeni, wallahi maisha hayatakuwa na regrets. Maisha na mtu mnayesikilizana na kuheshimiana ni yenye heri kulikoni maisha yenye utajiri wa kupindukia (lakini ndani ya nyumba ni viburi, dharau, kuvunjiana heshima na taka taka nyingine tosha!)

Correct me if am wrong...
 
Siyo siri mmoja wa wale niliowatumia hili bandiko ni mwenza wangu!

Nimefurahi kuona hata naye limemkuna, akaniandikia kwa kirefu sana and I was so moved!!

Thanks again.
Nawatia moyo na wengine humu mfanye hivyo hivyo..
Mtashangaa jinsi mada hii inavyoweza kuwasha moto wa uhusiano mwema na mazungumzo mazuri!!

You are so blessed my dada, tellng you nenda popote uliza hili swali generally majibu utakayoyapata ni ya aina moja, definition ya neno zima la investment, kuwekeza mara nyingi tunadefine in economic terms........hata kama tunazungumzia social protection hata yenyewe tunaidefine kiuchumi uchumi.....social protection inadefiniwa kwa uwezo wa kuishi vizuri i.e. chakula, malazi na mavazi (Economic wise) sasa sijui ni kwa vile issue nzima ya mahusiano tunaichukulia for granted kuwa its given na love yetu tunaidefine kwa terms za kuoa/oana kuwa mkishakubaliana kuoana basi ni uthibitisho wa mapenzi baina yenu so anything bad coming eith the 'marriage' tunaichukulia ni kawaida.....hence slogans za ndoa ni uvumilivu, msalaba, n.k hatufahamu ni kwa jinsi gani hayo tunayoyavumilia, na kuyabeba kama misalaba yanategeneza nyufa za mahusiano yetu uzeeni.... maumivu wakati wa ndoa za ujanani, hutufanya uzeeni tuishi si kwa mapenzi bali kwa mazoea kuwa huyu ni mwenzangu, wenetu wanashare damu zetu....

Nakumbuka kuna mama mmoja alikuwa anatuusia juu ya uvumilivu katika maisha ya ndoa..akasema yeye alimfumania mumewe na mdogo wake wa tumbo moja ambaye alikuwa anaishi naye, akachukua maamuzi magumu ya kumrudisha mdogo wake kwao na kuendelea kuishi na mumewe kwa upendo wa hali ya juu, huyu mama alisamehe lakini mpaka leo akisimulia habari hii hulia machozi ya kwikwi......tayari ni ufa na anaishi kwa kuwa aliolewa na huyu bwana ni mume wake!!

You are very right Mbu.hayo hayo tunayofanyiana tukayaona ni madogo!
 
Hata hujakosea kunisoma mydia....amini usiamini mawazo ya wazee wetu walio wengi ni hayo..namsomesha mtoto aje anitunze uzeeni......... mimi nilishawahiambiwa nimekusomesha na sasa ni jukumu lako kunitunza na kusomesha wadogo zako' na huyo si mzazi ambaye hajenda shule! Nakubali wapo walel ambao dhana ya kusomesha kwa faida ya uzeeni ishatoka but kwa waliowengi bado ipo na ndio kilio kikuu kwa wale ambao wamesomesha na bahati mbaya watoto wakafariki either kwa maradhi au lah......wengi wanalia mwanangu ameondoka hata matunda yake sijayafaidi!!

Ni wachache wenye kuamini kumsomesha mtoto kwa faida ya mtoto mwenyewe.

....ni mbaya sana, sana sana!...haipendezi hata kidogo. Mbaya kuliko zote eti kwakuwa wewe kidogo una unafuu, basi unastahiki uwasomeshe na wadogo zako - watoto-"wajukuu"- wa mzee aliyezaa na mke wa pili (dogo dogo,) mama mzazi alipoanza kukongoloka. Kwanini kuwabebesha mizigo watoto?

Kama mlifuatilia wazee wa jumuiya ya Afrika mashariki waliobahatika kupata mafao yao, wengine baada ya msoto wote ule eti wakaenda kuoa dogo dogo na kuzaa nao! Hivi sisi wabantu tumerogwa ee?...
Kiukweli, kusaidia ni hiari bana,...sio kwakuwa mdada/kaka ana kajinafasi kidogo/kasoma...basi ndio anatwishwa limzigo la ku support wazee, na ndugu wengine...haikubaliki bana....angalau wazee, lakini sio wengine ndio nao wajibweteke kisa dada "kaulopu!"

Nawashukuru sana wazazi wangu kwakweli, hawakuwa na akili za kusaidiwa. Wote wawili walijiwekezea kwa nafasi zao.
Mwenyezi Mungu awajaalie pepo, Ameen.

Somehow naamihi huenda huyu Babu anajaribu kuinvest kwka huyu binti hahahahahahah.

....LOL,...haya sasa umeanza, umeona anataka ku invest nini sasa na wewe...'mstaafu' huyo!

Siyo siri mmoja wa wale niliowatumia hili bandiko ni mwenza wangu!

Nimefurahi kuona hata naye limemkuna, akaniandikia kwa kirefu sana and I was so moved!!

Thanks again.
Nawatia moyo na wengine humu mfanye hivyo hivyo..
Mtashangaa jinsi mada hii inavyoweza kuwasha moto wa uhusiano mwema na mazungumzo mazuri!!

WoS,....nimefurahi sana kusikia hilo,...mw'mungu awazidishie mapenzi, huruma na maisha yenye heri na nyie.
 
You are so blessed my dada, tellng you nenda popote uliza hili swali generally majibu utakayoyapata ni ya aina moja, definition ya neno zima la investment, kuwekeza mara nyingi tunadefine in economic terms........hata kama tunazungumzia social protection hata yenyewe tunaidefine kiuchumi uchumi.....social protection inadefiniwa kwa uwezo wa kuishi vizuri i.e. chakula, malazi na mavazi (Economic wise) sasa sijui ni kwa vile issue nzima ya mahusiano tunaichukulia for granted kuwa its given na love yetu tunaidefine kwa terms za kuoa/oana kuwa mkishakubaliana kuoana basi ni uthibitisho wa mapenzi baina yenu so anything bad coming eith the 'marriage' tunaichukulia ni kawaida.....hence slogans za ndoa ni uvumilivu, msalaba, n.k hatufahamu ni kwa jinsi gani hayo tunayoyavumilia, na kuyabeba kama misalaba yanategeneza nyufa za mahusiano yetu uzeeni.... maumivu wakati wa ndoa za ujanani, hutufanya uzeeni tuishi si kwa mapenzi bali kwa mazoea kuwa huyu ni mwenzangu, wenetu wanashare damu zetu....

Nakumbuka kuna mama mmoja alikuwa anatuusia juu ya uvumilivu katika maisha ya ndoa..akasema yeye alimfumania mumewe na mdogo wake wa tumbo moja ambaye alikuwa anaishi naye, akachukua maamuzi magumu ya kumrudisha mdogo wake kwao na kuendelea kuishi na mumewe kwa upendo wa hali ya juu, huyu mama alisamehe lakini mpaka leo akisimulia habari hii hulia machozi ya kwikwi......tayari ni ufa na anaishi kwa kuwa aliolewa na huyu bwana ni mume wake!!

You are very right Mbu.hayo hayo tunayofanyiana tukayaona ni madogo!

...hapo penye wekundu hapo,..."living together for the sake of,...?" hapana bana. Tuishi pamoja kwasababu tulipendana, tunapendana, na tutaendelea kupendana (Kupendana kwa maana kamili ya mapenzi ikiwamo kuheshimiana) mpaka kifo kitapotutenganisha, sio kwasababu nimekuzoea..It's not right!
 
.........kweli uzee upo, kuwekeza ni lazima. Mie nikifikiria uzee huwa napata nguvu mpya ya kutengeneza my future.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
tuwafariji wazee pia

...wajibu wetu. Haipendezi kuacha mzazi/wazazi wako waadhirike. Jinsi umri unavyokwenda, na Speed ya maisha inaongezeka kwa kasi kubwa sana,...inabidi kuwastiri kwa siku zao chache zilizobakia duniani. "What goes around comes around!"...jitengenezee baraka zako nawe utakuja stiriwa!

Tatizo liko kichwani mwetu!

Tatizo gani, na Kivipi bana?...
 
...hapo penye wekundu hapo,..."living together for the sake of,...?" hapana bana. Tuishi pamoja kwasababu tulipendana, tunapendana, na tutaendelea kupendana (Kupendana kwa maana kamili ya mapenzi ikiwamo kuheshimiana) mpaka kifo kitapotutenganisha, sio kwasababu nimekuzoea..It's not right!

Wewe ninaanzisha taasisi ya mambo ya jamii...ntakushirikisha uyajue yaliyomo!!
Tell you wazazi wetu wengi kwa sasa wanaishi kwenye hiyo dhana ya mazoea..nimeolewa/oa jamii inajua na uzee huu nikikinzana nani atanielewa? It is very sad and am telling you wale ambao wanachukua ujasiri na uthubutu wa ku'toka' ndani ya chungu cha moto kukingali mapema wanapewa majina yote maovu na vidoe wananyooshewa...Life is not as we see from outside my sweetheart!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...wajibu wetu. Haipendezi kuacha mzazi/wazazi wako waadhirike. Jinsi umri unavyokwenda, na Speed ya maisha inaongezeka kwa kasi kubwa sana,...inabidi kuwastiri kwa siku zao chache zilizobakia duniani. "What goes around comes around!"...jitengenezee baraka zako nawe utakuja stiriwa!

...

Hizo baraka zako wazitengenezaje if I may ask Mbu?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Karma.....
Do good unto others and good will be done unto you

Aksante Babu I hope that 'others' haiko limited kwa wazazi tu......kwa sababu once unapoamua kuwa good kwa wazazi ndipo hapo wengine wanapoamua kuigeuza hisani kuwa deni.....mzazi unafikiria kuwa 'good' kwake anaichukulia kuwa ni jukumu lako kuwa'good' kwake na hapo anatafuuta justification ya wewe kuwa 'good' kwake.............Nakumbuka ilishawahitokea kwa one of my closest frioends.......yeye mzee wake aliamua kukopa pesa 'mkopo' kwa matumizi ambayo hayakuwezakuwa accounted for.. (ni mzazi hawezimwuliza ulikopa za nini) ila akaambiwa '''" nimekopa kiasi kadhaa, niosaidie" bahati mbaya best hakuwa na hiyo pesa kwa wakati huo....akatafuta kwa mbinde akapata ila ikapungua kama 30% ya deni.....akafunga safari toka huko alikokuwa akamletea mzee (ambaye si kuwa ni masikini, he had a lot of vitega uchumi ) aliishiwa kutupiwa visenti vyake akisindikizwa na maneno.......unanichezea?? Nimekwambia ninadaiwa kiasi flan, utanleteaje pungufu?? Nimekusomesha kwa faida gani??

So we can get picture that what we think sisi kama sisi, inaweza ikawa tofauti kabisa na wanavyofikiria baadhi ya wazee wetu! What I want to say here ni kuwa kile ambacho sie/wewe unadhani unakitoa kwa moyo wa kujitolea, mzazi anaweza kuinterprete kuwa ni wajibu wako kufanya hivyo......after all amekusomesha na asingekusomesha usingekamata hizo dolari unazozikamata leo!! na they are right!
 
wazee husema ujana maji ya moto

na wataalamu wanasema,ukitaka kuishi vizuri,
yatazame maisha yako kuanzia mwishoni kuja mwanzoni...

weka picha siku unayokufa,nini umeacha,nani atakulilia?
halafu rudi taratiibu mpaka leo ulipo
 
Wewe ninaanzisha taasisi ya mambo ya jamii...ntakushirikisha uyajue yaliyomo!!
Tell you wazazi wetu wengi kwa sasa wanaishi kwenye hiyo dhana ya mazoea..nimeolewa/oa jamii inajua na uzee huu nikikinzana nani atanielewa? It is very sad and am telling you wale ambao wanachukua ujasiri na uthubutu wa ku'toka' ndani ya chungu cha moto kukingali mapema wanapewa majina yote maovu na vidoe wananyooshewa...Life is not as we see from outside my sweetheart!!

...wala sikubishii myluv,...si ndio jamii tunayoishi? ...mwisho wa siku ni vile wewe unaamini ni sahihi hata mbele ya Mw'Mungu akusamehe ufanyalo ndilo. Haya maisha ya kuishi kwakuogopa jamii itakufikiriaje, mnh!...

Anyway...kuna miiko, mila, tamaduni na desturi... Tatizo linakuja kwenye ku balance/kuoanisha hayo matatu na Imani yako kidini na tafsiri ya maisha ya sasa na sheria za nchi.

...Psychological abuses nyingi kwenye ndoa zinatokana na mmoja wapo wa wanandoa atapotumia udhaifu wa tafsiri ili kuvutia upande wake. Mfano, kwenye sheria ya ndoa Tanzania,
...
CHAPTER 29​
THE LAW OF MARRIAGE
Sepa
ration and Divorce
(ss 99-101

Restriction on petition for divorce during first two years of marriage
(1) No person shall, without the prior leave of the court, petition for divorce before the expiry of two years from the date of the marriage which it is sought to dissolve.(2) Leave shall not be granted to petition for divorce within two years of the marriage except where it is shown that exceptional hardship is being suffered by theperson applying for such leave.

...yaani ndoa haiwezekani kuwa na dosari ya kuachana mpaka imalizike miaka miwili? Chunguza atayekuwa anateseka zaidi hapo. Anyway, haya ni masuala mengine,...nimewekeza tu kujumuishia yale ya kutendeana wema na hisani katika safari nzima kuelekea kwenye fainali za uzeeni...

Hizo baraka zako wazitengenezaje if I may ask Mbu?

Mwj1...suala la 'baraka' ni kiimani zaidi mydear,...'blessings'...
Kumtendea wema mzee/wazee wako na wakakushukuru ndio blessings zenyewe hizo, ninavyoelewa mie.
 
wazee husema ujana maji ya moto

na wataalamu wanasema,ukitaka kuishi vizuri,
yatazame maisha yako kuanzia mwishoni kuja mwanzoni...

weka picha siku unayokufa,nini umeacha,nani atakulilia?
halafu rudi taratiibu mpaka leo ulipo

.........Hebu, hebu rudia tena hapo kwenye red, nami ninaomba niongeze sauti ya Speakers mydia.
 
Vijana wanachana mistari balaa. Nimejikuta napenda miziki yao japo si mshabiki wa miziki ya kufoka. Wanaongelea real life si kupretend. I real like their style watoto wa kiumeni.

yaani hii nyimbo ilipotoka nilikuwa kwenye hard time sana
in a way sometimes nilikuwa nabadili stations nikiisikia
dah......
yaani walikuwa wananigusa vibaya mno
 
So we can get picture that what we think sisi kama sisi, inaweza ikawa tofauti kabisa na wanavyofikiria baadhi ya wazee wetu! What I want to say here ni kuwa kile ambacho sie/wewe unadhani unakitoa kwa moyo wa kujitolea, mzazi anaweza kuinterprete kuwa ni wajibu wako kufanya hivyo......after all amekusomesha na asingekusomesha usingekamata hizo dolari unazozikamata leo!! na they are right!
I think hapa inabidi tufanye mambo within reason kama uwezo upo tunawasaidia wazazi kadri tunavyoweza kama mzazi bado ana akili timamu (as you know binadamu tunavyokuwa ndio na akili zetu zinakuwa za kitoto) basi tutareason nae na kumwambia mzee this is how I can help vingine sina uwezo basi atakuelewa, kama ashakuwa mzee sana basi unaweza kumpiga sound na kumdanganya tu ili roho yake iridhike. Kama ni mzee mbishi asietaka kuelewa inabidi tufanye kila kitu kuonyesha kwamba hatujamdharau.

Pia kama una tabia za kuwasaidia watu na wazee wengine you never know ukizeeka lazima watasema dah yule mwanajamiione alikuwa mtu mzuri sana sasa hivi mzee hana msaada yaani watakuwa willing kukusaidia, tofauti na kama ulikuwa mtu wa majivuno na bila msaada kwa mtu yoyote basi hapo watakucheka na kukukebei
 
Back
Top Bottom