...Genius!...maswali yako yamekaa kimtego mtego,...mtu akikurupuka na jibu la hovyo hovyo anakuwa amejichongea.
Mwj1...katika suala hili, naomba Nyumba ndogo/Serengeti Boys/Vidumu etc vilaaniwe kwa nguvu zote!
Hamna kitu mbaya kama kwenye old age unajikuta moyoni una madonda ya 'mke wangu/mume wangu' alini cheat na fulani...hiyo ni sumu...ndio maana binafsi sitaki hata kuifikiria hiyo scenario. Madhali umeiulizia, naomba kukujibu kwamba...hali hiyo hata kama mtakuwa mmesameheana, bado itakuwa ni kovu pale watoto watapokuja kuwataka ushauri wa ndoa zao zitapokuwa zimekubwa na misuko suko ya aina hiyo. Old memories zitajirudia tu...
Sidhani kama itakuwa rahisi ku list down mambo mnayostahiki kuyajengea msingi wa maisha yenu (mpaka kifo kitapowatenganisha) kwani mambo yenyewe ni haya haya kila siku mnayofanyiana. Kuheshimiana, kusaidiana, kuoneana huruma, kupendana, kusameheana, kuongea, kusikilizana na kuelewana, kukubaliana, kupeana subira,...kujaliana,...nk nk nk...
Iwapo maishani mwenu mtajijengea hayo tajwa, na mkafanikiwa kuendelea hivyo hivyo mpaka uzeeni, wallahi maisha hayatakuwa na regrets. Maisha na mtu mnayesikilizana na kuheshimiana ni yenye heri kulikoni maisha yenye utajiri wa kupindukia (lakini ndani ya nyumba ni viburi, dharau, kuvunjiana heshima na taka taka nyingine tosha!)
Correct me if am wrong...