Fainali ya Kombe la Dunia Mtibeli nimepata Kadi ya Mwaliko kutoka kwa binti Salher. Imekwisha! Hata siamini

Fainali ya Kombe la Dunia Mtibeli nimepata Kadi ya Mwaliko kutoka kwa binti Salher. Imekwisha! Hata siamini

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Kachezeni mnapochezaga!
Sitaki salamu zenu za kichawi msije nipotezea ndege wangu.

Mlifikiri nimekwama na maisha yangu yataishia hapahapa ndani. Hahaha! Hamtaweza na mmeshindwa kwa jina lile la maajabu.

Oooh! Mtibeli usitoe siri zako kuna watu watakuloga safari utajifia. Thubutu! Kusema nasema na safari ipo na ninatamba nayo.

Tangu mwaka huu umeanza nilikuwa busy na simu yangu hii. Najua sio ya gharama lakini ndio hiihii huwezi amini inanipeleka the State united nation huko Amerika. Basi nilikuwa busy na mitandao ya kijamii huko sio Facebook, sio Instagram, sio tiktok na baadh ya app huko.

Nilikuwa busy kuingia kwenye inbox za profile zilizojionyesha kama zinamilikiwa na wanawake wa kizungu.

Basi kwa siku nilikuwa natuma sms huko inbox zaidi ya mia tatu. Imagine, Unaweza kudhani ni kazi wala sio kazi ngumu. Nilishirikiana na ChatGpt akanitengenezea bonge moja la meseji kwa lugha ya kingereza.
Unajua mimi sio mzuri sana kwenye kingereza. Lakini nataka nikupe moyo hata wewe. Usikate tamaa. Lugha isikukatishe tamaa. Penye nia pananjia.

Hiyo meseji kila siku nikawa naituma kwa vidada huko.
Kabla sijatuma kuna mambo nilikuwa nayazingatia. Sijitumii hovyohovyo.
a) kwanza nilikuwa naangalia picha za nitakayemtumia. Lazima awe mzungu mzuri mwenye sura nzuri na tumwili fulani hivi. Mamaaa! Yaani mpaka nahisi nililogwa hivi.

b) Pili, lazima awe amepiga picha maeneo mazuri.

Nilikuwa sipendi akaunti zilizoblockiwa. Nilikuwa nasonya kama masai mlaugoro.

Baada ya kutuma meseji elfu kumi na miatatu sabini (10370), nikahisi kukata tamaa. Alooh nimepiga kazi aseeh.

Mwezi wa tano napokea ujumbe wa majibu. Tena nilikuwa mwendokasi natoka zangu Kariakoo. Weeeh! Kidogo nipige kelele.

Salher ndiye mwanamke pekee aliyenijibu.
Basi tukaanza kuchat wee. Baada ya siku sita hivi tukapeana whatsapp number.

Tukaanza kuwasiliana kwa whatsapp. Tumiana sana picha na video.
Sasa mimi ili nihakikishe nilikuwa na usongo wa kusikia sauti yake na sura yake kwa njia ya videocall.

Naye akawa ananichelewesha. Mwisho wa mwezi wa tano akanipigia saa tano usiku. Mamaaa! Kumbuka nina familia, wake wawili na watoto. Oooh My God kumbe Robert sio Mwaminifu eeeh!

Sikilizeni. Nyie nisikilizeni tuu. Mengine tutajadili baadaye. Hapa muhimu stori mjue nilipataje invaitasheni

Nikatoka nikaenda sebuleni, lakini sebuleni mtu akiongea wachumbani atasikia. Dadeki sasa nikaongelee wapi. Chooni au bafuni. Mmh! Nikienda chooni au bafuni salher nitampa wasiwasi.

Meseji ikaingie tutu! Inaniaga. Heee! Kwamba nachezea bahati.

Nikatoka nje. Kwa nje kuna bar upande wa pili. Nikatafuta space. Nikajichimbia hapo kwenye kona fulani yenye mwanga. Nikapiga.

Ayaaa! Jamani yule mtoto ni mzuri jamani! Toto la kizungu, haaa! Hapana jini hivi. Zuriiii alafu linamacho ya buluuu hivi.

Nilaliambia mambo, linaniambia what what halielewi. Basi tukazungumza weee. Kama dakika kumi hivi. Toto linatabasamu kama nini sijui. Sitaki hata kukumbuka naweza kupaa.

Ikafika mwezi wa sita tarehe mbili akaniambia vipi ratiba yangu nikamwambia niko fresh. Akaniambia kama nitaweza kombe la dunia fainali niende Marekani. Haaa! Huyu demu vipi unajua alinifanya nipagawe.

Nikamwambia Visa ya Marekani inasumbua, ila passport ipo. Akasema fresha atashughulikia visa kwa kuanza na kunitumia barua ya mualiko. Unajua kama mzaha mzaha leo haukutumbua usaha umetumbua mtima.

Wiki iliyofuata akatuma barua ya mualiko. Kisha akatuma na kiwango kidogo cha pesa. Wala sio pesa nyingi maana nawajua wabongo mlivyo na njaa.

Alipotuma pesa kidogo nikaanza kumuamini.

Hapa nilipo kuanzia tarehe 22 nitakuwa mbele huko. Dadeki! Nitakaa kama mwezi mmoja hivi ndipo nirudi kuwasimulia kinagaubaga.

Nikirudi nitawawekea na picha humu yaani itakuwa fujo fujo fujo tuu.
Maskini akipata matako hulia mbwata. Ndio mtajua hamjui.

Mlio Marekani tuwasiliane kabisa mapema mapema. Wiki ijayo sio mbali.

Kwa mlio Marekani niambieni swaga za huko, nikifika Salher asije niona mshamba fulani hivi, nikaeje kaeje, niongeeje ongeeje, vipi kutembea, kuvaa.
Maana hizi pesa alizonitumia najua alimaanisha nini.

Angalizo, wewe kama hujawahi kupanda ndege huu uzi upite kama unaaga maiti.
Kama unajijua hujawahi miliki pisikali za kizungu kama sisi huu uzi haukuhusu. Tuacheni na maisha yetu.

Ahsanteni sana. Nimemaliza.

Mtibeli Maisha kayaotea. Shwaaah!​
 
Ama kweli MENTAL HEALTH IS REAL.

YOTE HII NI CCM CHANZO
 
Back
Top Bottom