Fainali ya Ligi kuu ya mbio za mabasi Tanzania (Sauli vs New Force/ Golden Deer) na lori la mafuta, serikali imejifunza nini?

Fainali ya Ligi kuu ya mbio za mabasi Tanzania (Sauli vs New Force/ Golden Deer) na lori la mafuta, serikali imejifunza nini?

LATRA LEO WAMEFURAHI SANA.
KILA wakiambiwa NEW FORCE NI JANGA hawaSIKII, SIJUI KUNA KITU WANAPEWA?
 
Na hapo ndo ujiulize. Toka mida ajali imetokea, hakuna breakdown! Hakuna hata grader au dozer ya kutengeneza njia ya dhalula! Kutoka Kibaha,saa moja na nusu,tupo njia ya Morogoro, hakuna gari iliyopita kutoka njia hiyo au inayopita kwenda.

Jiulize jam hiyo imekaaje! Na ajali imetokea asubuhi tu!!!!

Kwa wanaojua hesabu za kihasibu,wao ndo wanajua hasara taifa liliyopata kwa mda huo.
 
Hilo bus la Sauli nililipanda mara ya mwisho ilikuwa ni 2020 December naelekea Mbeya kwenye msiba wa mzee wake na rafiki yangu, ilikuwa ile Benz DPC dereva dogo mmoja anaitwa Nabii Tito. Niseme tu ule mwendo na hizo overtaking jamaa alikuwa anafanya ilikuwa ni hatari sana niliapa sitakaa nipande tena hilo bus, na sikupanda ten mpka leo hii. Bora mzee Ngalo wa ABC ameingiza bus hiyo njia aokoe jahazi huko, hao New Force nao hata bure sipandi, kila leo ajali
Una bahati sana hujawahi kupanda Matema Beach, Safina, Zainabs, Tawaqal, Sayuni, Mwanahapa a.k.a M Sleeping Coach, ilikuwa ni balaa
 
Na hapo ndo ujiulize. Toka mida ajali imetokea, hakuna breakdown! Hakuna hata grader au dozer ya kutengeneza njia ya dhalula! Kutoka Kibaha,saa moja na nusu,tupo njia ya Morogoro, hakuna gari iliyopita kutoka njia hiyo au inayopita kwenda.

Jiulize jam hiyo imekaaje! Na ajali imetokea asubuhi tu!!!!
Chama Cha Mazezeta
 
Ghafla nimeona taarifa now.kumbe katika Hilo sauli la Leo ndo analofanyia kazi rafiki yangu wa tangu shule..imagine mtu anapiga kazi na afya njema Kisha kesho inatangazwa kafa..ajali hizi

Hiyo ajali watu kibao wamekufa ila wanaficha
Ajali za New Force zinafunikwa funikwa sana
 
Kuna uzi humu ukitabiri maafa yatakayotokea kwa hizo basi kutokana na upuuzi wa kukimbizana huku majitu yakishangilia. Hii nchi ina watu wa hovyo sana
 
Kùjifunza ni kitu kisicho na mwisho wala mipaka. Serikali yetu na watendaji wake hawajàona haja ya muda mrefu kujifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya fainali ya Ligi Kùu ya mbio za mabasi Tanzania kati ya New Force/ Golden Deer vs Sauli.

Maafa tumeanza kuyaona, leo mabasi yamegongana na Lori la mafuta, watu wamekufa, wengine kujeruhiwa. Lakini kesho makosa haya haya yatajirudia na watendaji wa serikali wenye wajibu wa kuwadhibiti wasafirishaji hawa wataendelea kushabikia fainali hiyo.

Polisi wa usalama barabarani na LATRA wanahusika kwa kiasi kikubwa kutokana na udhalimu huu unaoathiri maisha ya abiria wasio na hatia
LATRA WAMEWEZA KUPANGA RATIBA HADI USIKU,UKIONA MTU ANASHABIKIA HAYO MABASI UJUE NI KIMEO,KWANINI UPANDE BASI ZINAKIMBIA HOVYO NAMNA HIYO
 
Back
Top Bottom