Transcend
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 20,548
- 63,038
Sawa mkuu.Faiza foxy ni wakati wake kujibu maswali ya audience.
Ila nina machache nataka niyaseme tuu, just for good
1. Nakushauri upunguze hizi interview za kila siku. Wakati mwingine inakuwa kama ni mazoea na watu wanashindwa kuzipa attention vizuri. Leo umefanya interview 2
2. Pili, Chagua Muda ambao watu wengi wanakuwa online, kati ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku. Interview kama ya miss natafuta wengi wameikuta imeisha tayari.
3 . HUU NI USHAURI WA MEMBERS WENGINE
Naomba tuwe na NIDHAMU ya interview kama tunataka kweli tujifunze, hizi interview sio kwa ajili ya kufurahisha tuu ila kuna mambo mengi ya kujifunza. Kwenye interview mtu anaweza kushare kitu adimu sana lakini kama kila mtu anauliza maswali tena bila mpangilio lazima tupoteze point na mengine hayatajibiwa kabisa.
Sehemu b, wasomaji tuache kupiga stori kwenye interview ya mtu. Hii kiti kinakera sana kwenye interview watu wanapiga stori kama wako pm...sio ishu naomba tuache wakuu.
Tuwe na ustaarabu ili tufaidi hizi interview. Nimesema hili na mimi nikiwa ni mmojawapo ya watu wenye hiyo tabia.
Kuna watu wanapenda kuingilia na kuaribu thread , tutakuombea BAN tuu. No way.
MIMI NIMEACHA HII TABIA. LEO MWISHO.
4 . Madhumuni ya interview ni mengi sana, tofauti na kujifunza watu wanataka kufurahi .
Hili nalisema kwa wale wanaokuwa interviewed wawe SERIOUS na wajibu maswali yote kwa ajili ya watu wanaospend time kusoma comments zao. Kukimbia maswal sio ishu wakuu.
5. Nawashukuru wale wote watakao soma hii comment na kuelewa maana yangu na pengine kuifanyia kazi.
Asanteni wakuu.