Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!

Faiza foxy ni wakati wake kujibu maswali ya audience.
Sawa mkuu.

Ila nina machache nataka niyaseme tuu, just for good

1. Nakushauri upunguze hizi interview za kila siku. Wakati mwingine inakuwa kama ni mazoea na watu wanashindwa kuzipa attention vizuri. Leo umefanya interview 2

2. Pili, Chagua Muda ambao watu wengi wanakuwa online, kati ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku. Interview kama ya miss natafuta wengi wameikuta imeisha tayari.


3 . HUU NI USHAURI WA MEMBERS WENGINE

Naomba tuwe na NIDHAMU ya interview kama tunataka kweli tujifunze, hizi interview sio kwa ajili ya kufurahisha tuu ila kuna mambo mengi ya kujifunza. Kwenye interview mtu anaweza kushare kitu adimu sana lakini kama kila mtu anauliza maswali tena bila mpangilio lazima tupoteze point na mengine hayatajibiwa kabisa.

Sehemu b, wasomaji tuache kupiga stori kwenye interview ya mtu. Hii kiti kinakera sana kwenye interview watu wanapiga stori kama wako pm...sio ishu naomba tuache wakuu.
Tuwe na ustaarabu ili tufaidi hizi interview. Nimesema hili na mimi nikiwa ni mmojawapo ya watu wenye hiyo tabia.

Kuna watu wanapenda kuingilia na kuaribu thread , tutakuombea BAN tuu. No way.

MIMI NIMEACHA HII TABIA. LEO MWISHO.


4 . Madhumuni ya interview ni mengi sana, tofauti na kujifunza watu wanataka kufurahi .

Hili nalisema kwa wale wanaokuwa interviewed wawe SERIOUS na wajibu maswali yote kwa ajili ya watu wanaospend time kusoma comments zao. Kukimbia maswal sio ishu wakuu.


5. Nawashukuru wale wote watakao soma hii comment na kuelewa maana yangu na pengine kuifanyia kazi.



Asanteni wakuu.
 
....Ukipata muda jibu na hili

[emoji116] [emoji116]
Kwanini tunatakiwa kuwa waislamu
 
0.Mtazamo wako vitabu vina uwezo wa kubadilisha maisha?
1.Unasoma vitabu vingapi kwa mwaka?
2.Aina gani ya vitabu unapenda kusoma?
3.Tupe majina ya vitabu vyako kumi bora ulivyowai kusoma?
4.Kwa mtu ambaye anataka kuanza kusoma vitabu,aanze na kipi?
0. Sana tu.
2. Vichache sana bila kusahau nnapendelea sana kusoma "scholarly papers", magazeti, majarida na variety ya "encyclopedias".

"Style" yangu ya kusoma si kusoma kwa kumaliza vitabu vingapi, "style" yangu ya kusoma ni nimejifunza kipi. Sijapata kukosa kusoma hata siku moja toka nilipoanza kusoma.
3.
I. Qur'an, hii nnaisoma kila siku na sijakosa kujifunza kipya kila nnapoisoma.

Vingine vingi sana na nimeweka hapa not in order.

II. The Great Gatsby.

III. The Elements of style.

IV. How to win friends and influence people.

V. Anna Karenina.

VI. Empires of The Monsoon.

VII. One Hundred Years of Solitude.

VIII. One Thousand and One Nights (Alf Lela u Lela).

IX. The Perfumed Garden.

X. The Guide

Kila nikiandika nakumbuka kingine.

4. Qur'an.
 
Ahsante Bibi.

Hopely umeamka salama.

Twende sambamba kabla naisubiri Subhi hapa.
 
Asante My friend Transcend!
Kuhusu kupunguza siku za interview nitalifikiria kuanzia wiki ijao,maana itabidi kurekebisha ratiba yangu ambayo kwa kweli imejaa.

Ushauri kwa members wengine wameusikia
Regard
DJ sepetu.
 
Asante My friend Transcend!
Kuhusu kupunguza siku za interview nitalifikiria kuanzia wiki ijao,maana itabidi kurekebisha ratiba yangu ambayo kwa kweli imejaa.

Ushauri kwa members wengine wameusikia
Regard
DJ sepetu.
Poa mkuu.

Bibi yupo ulingoni sasa.

Nimetega sikio hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…