Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!


Nna uhakika Rais ana nia njema kabisa. Kinachotustua ni style yake ya kuongoza.

Elewa kuwa Magufuli anasimamia na kutekeleza ilani ya CCM. Magufuli anatekeleza ilani ya CCM to the dot.

Mapungufu ya ilani hiyo hayakufafanua itekelezwe vipi, imeainisha tu ya kufanyiwa kazi, vipi yatafanyiwa kazi haikuwekwa.

Kuna daladala moja niliisoma imeandikwa "chizi kapewa rungu", ikanifikirisha sana. Nikacheka.
 
Hongera sana Bibi.

Bora unyamaze kutoishabikia maana ina mapungufu kama ulivyosema huku M/kiti hataki kushauriwa
 
Maswali yako yote nimeyajumuisha kwenye jibu moja...

Hapana, niliamua mwenyewe kuoana na Mume wangu, huku nikijiuliza ntaendelea kusoma kweli? Nikajikuta katika dilemma "niolewe nisiolewe niendelee na masomo? ". Mahaba niue nikaamua ndoa.

Kwa bahati nzuri kabisa nikajikuta nimeoana na mtu ambae from day one ameni encourage kuendelea na masomo na akawa msaada mkubwa kwangu kimasomo.

Hakukuwa na sababu yoyote ya uwezo. Kwani nilibahatika kusomeshwa bure na serikali ya huko nilipoishi (si Tanzania) kwa wakati huo.

Changamoto hazikuwa nyingi kwa sababu mume wangu alikuwa akifanya kazi za kwenye visima vya mafuta, kurudi kwangu kusoma ilikuwa faraja kwangu na kwake maana alikuwa anafanya kazi nchi tofauti tofauti na kulikuwa na gap ya kuonana. Masomo yakani keep busy.

Sikuolewa mdogo sielewi hilo umelitoa wapi? Nimeolewa umri wa halali kuolewa kidini na kiserikali.

Kumbuka nimeolewa tayari nikiwa Chuo Kikuu.
 
Shukrani Bibi
 
Nadhani sijachelewa sana.Naomba niingie kwenye maswali tangy
1)Hali ya sasa ya kisiasa nchini una lipi la kusema?
2)Katika tukio hili lililotokea la Mb Tundu lissu la kupigwa risasi una mtizo gani kwa upande wako?.
3)Tumeshuhudia wananchi wakikosa imani kwa vyombo vya ulinzi na usalama je hali ikiendelea haiwezi kupelekea machafuko?
4)Nini kifanyike kukombowa wimbi la vijana wasio na ajira?
Shukrani.
 
Mie nataka nijue mama hilo jina la faiza foxy ni jina lako halisi na hiy avatara ni wew na kama sio wew huyo mama ulomuweka kweny avatari unajifunza nin kutoka kwake
Kuhusu jina, jibu lake ni hili...

Kuhusu avatar huyo si mimi huyo ni Lisa Valentine kisa chake kilinifanya nimkubali sana. Kisome kisa chake hapa: US judge jails Muslim woman over head scarf - World News - SINA English
 
1) Sijaajiriwa, naajiri.

2) Kuulizana umri ni ubaguzi, AlhamduliLlah wanangu wote ni watu wazima na shughuli zao.

3) AlhamduliLlah, nimebahatika kusafiri sana tena sana. Zaidi ya nchi 100 duniani.

4) Mimi ni Muislam, Waislam hatuna "fungu la kumi" Waislam tuna Zaka. AlhamduliLlah natoa Zaka.

5) Ban zingezidi kwa members wasio na heshima. Ningehakikisha JF inakuwa "cited" bila mtu kuona haya kuwa ni member wa JF.

5) Siku zangu hazilingani kila siku, itakuwa ngumu kuweka ratiba. Siishi kwa ratiba ispokuwa kuna mambo muhimu ambayo siyakosi kila siku. Kuswali na kuongea na wanangu wote. Labda nisiwapate kwenye simu.
 
Asante My friend Transcend!
Kuhusu kupunguza siku za interview nitalifikiria kuanzia wiki ijao,maana itabidi kurekebisha ratiba yangu ambayo kwa kweli imejaa.

Ushauri kwa members wengine wameusikia
Regard
DJ sepetu.
Mkuu ungejaribu kuziyanya interviews kuanzia mida ya saa kumi ivi, watu wengi wanakuwa flexible, binafsi ile ya miss natafuta ilinipita
 
Shukrani Bibi
 
Umekielewa ulicho kikwoti?

Au umeamua kukwoti kila bandiko lililo mbele yako ili tujue uwepo wako?

[emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]
Ili iweje? Ungeona humu kila post nai-quote kama ufanyavo wewe wengine hatupendi kucomments hovyo, kusoma tu comments za watu inatosha ila jamaa unaharibu mtiririko kuna vitu ambavyo unakuta mtu unasubiria vijibiwe na bibie wewe ushadakia na kuchafua mazngira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…