FaizaFoxy mimi nauliza maswali kadhaa tu ya mwisho kwa kuwa yale mengine umenijibu vyema..Nimevuta subra kama ulivyosema..
Sasa maswali yangu ni haya..
1: Unachukuliaje suala la Malezi ya watoto hasa katika kipindi hiki cha Utandawazi? Uonavyo wazazi wanatimiza wajibu wao ipasavyo??
2: Kuna dhana imejengeka kwenye jamii yetu kuwa Mwanamke akipata elimu anakuwa na kiburi/majivuno na kumuona mumewe hafai, wewe unaonaje hili suala ni sawa au sawa? Je wewe limeshakukuta??
3: Ni kweli kuwa baadhi yenu nyie wanawake hampendani ninyi kwa ninyi?? Nini huchangia hili??
4: Ukipewa nafasi ya kuongeza/kupunguza kitu hapa JF ungeongeza nini au kupunguza nini...je unawashauri nini wamiliki wa mtandao huu pendwa??
5: Unawashauri nini vijana wanaotafuta mafanikio kwa njia za mikato (shortcut)??
Na mwisho kabisa unapendelea kufanya nini upatapo muda wa ziada..
(Mimi maswali yangu ni hayo tu, ukinijibu nitashukuru sana, asante)