Nimesoma ushauri wa Babu
Asprin na
Transcend, naomba na mimi niongeze kitu kwa moderator
DJ Sepetu;
1. Kwa baadhi ya Members ambao ni either high profile figures au wana muda kidogo unaweza kuweka thread mapema watu wakauliza maswali yao yote halafu baadae ukachagua maswali na kuyapanga kwa mtiririko ili kusiwe na kurudia rudia maswali. Then unafungua thread ya interview maswali yakiwa tayari yameandaliwa.
2. Maswali ya msingi yakishaisha, unaweza ukaruhusu random questions
3. Halafu kabla ya kum-interview mtu vizuri ukapitia profile yake mapema, unaweza kuelewa nini cha kuuliza au cha kuacha, fanya kama wanavyofanya journalists, mfano ukipitia uzi wa
faizafoxy wa
Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa ungeweza kupata ABCs za uanzie wapi kwenye interview
NB: Hii kitu uliyoanzisha imekuwa kubwa tofauti na ilivotegemewa, ilianza kama utani lakini inazidi kukamata, kuna mapokezi ya kila aina kutoka kwenye hadhira, hivyo jipange na uweze kubadilika kulingana na unayemwinterview.