Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!

Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!

Neno kuabudu lina maana pana sana.

Kuabudu si kuswali pekee kama wengi wanavyofikiria.

Ibada ni kufanya yote ya halali na kuwacha yote ya haramu.

Ni mada kamili yenye mengi sana. Maisha anayoishi mwanadam huwa na mambo mengi, moja linaweza kuwa ni haramu kwa Muislam lakini si haramu kwa asiye Muislam likaleta utata.

Ndiyo maana tunaamrishwa tukumbushane mema na tukatazane mabaya.

Kuna kisa kimoja cha Sheikh mkubwa wa AL Azhar, Misr, alienda kutembea nchi za Magharibi kwa ziara ndefu. Aliporudi Misr, aliulizwa umekuta nini huko? Akajibu huko "nimekuta Uislam lakini Waislam hakuna, hapa kwetu Waislam wengi Uislam hakuna".
Bibi umerusha jiwe gizani
 
Nimesoma ushauri wa Babu Asprin na Transcend, naomba na mimi niongeze kitu kwa moderator DJ Sepetu;

1. Kwa baadhi ya Members ambao ni either high profile figures au wana muda kidogo unaweza kuweka thread mapema watu wakauliza maswali yao yote halafu baadae ukachagua maswali na kuyapanga kwa mtiririko ili kusiwe na kurudia rudia maswali. Then unafungua thread ya interview maswali yakiwa tayari yameandaliwa.

2. Maswali ya msingi yakishaisha, unaweza ukaruhusu random questions

3. Halafu kabla ya kum-interview mtu vizuri ukapitia profile yake mapema, unaweza kuelewa nini cha kuuliza au cha kuacha, fanya kama wanavyofanya journalists, mfano ukipitia uzi wa faizafoxy wa Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa ungeweza kupata ABCs za uanzie wapi kwenye interview

NB: Hii kitu uliyoanzisha imekuwa kubwa tofauti na ilivotegemewa, ilianza kama utani lakini inazidi kukamata, kuna mapokezi ya kila aina kutoka kwenye hadhira, hivyo jipange na uweze kubadilika kulingana na unayemwinterview.
[emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419]
Nakazia
 
Hapana, sijaolewa.

AlhamduliLlah mimi na Mume wangu tumeoana kwa zaidi ya miaka 35 sasa.

Tuna watoto 5 nilipoteza wawili. La haula wala quwatta ila bi Llah.
Hapana hujaolewa ila umeishi na mumeo kwa miaka 35 mbona sijakuelewa hapo
 
Ipo inaitwa Abdul - badry kama hujasoma dini kaa kimya mkuu .inasoma kwakuwataja mashwahaba wamwenyezimungu .Nailisomwa kwenye vita ya badry .so Abdul badry so shirki .
Hakuna maswahaba wa mwenyezi MUNGU kuna maswahaba wa mtume. Pia ni ahlul -badry sio abdul
 
Hahahah

Hahahahah umenifanya nicheke, kwamba wakati mwingine huvai nguo!!! do you fly at night? Sometimes uwa una michango ya maana sometimes not, The problem I see in you, you are too emotional. You do not need to use offensive language against those asking irrelevant questions. You can opt to ignore their questions.
Akiwa na mumewe havai ndo mana akasema inategemea na situation. Acha uvivu wa kufikiria
 
kwa nini unatumia jina FaizaFoxy?
Ulisoma telecom, umeisaidiaje jamii yako kwa elimu yako hiyo?
unaushauri gani kwa vijana katika suala zima la kutafuta kipato ktk mazingira magumu ya ajira na ugumu wa kibiashara
 
Nadhani sijachelewa sana.Naomba niingie kwenye maswali tangy
1)Hali ya sasa ya kisiasa nchini una lipi la kusema?
2)Katika tukio hili lililotokea la Mb Tundu lissu la kupigwa risasi una mtizo gani kwa upande wako?.
3)Tumeshuhudia wananchi wakikosa imani kwa vyombo vya ulinzi na usalama je hali ikiendelea haiwezi kupelekea machafuko?
4)Nini kifanyike kukombowa wimbi la vijana wasio na ajira?
Shukrani.
1) Sasa hivi siioni siasa.
2) Hili tatizo tusilichukulie kisiasa na jazba. Uchunguzi wa kina ufanyike na kila muhusika achukuliwe hatua kali za kisheria.
3) Kuna fitna kubwa sana kwenye mali. Tusikurupuke.
4) Waelimishwe ajira si kuajiriwa tu.
 
Umekuwa na mtazamo hasi sana kwa Mwl Nyerere na nchi ya Marekani,sababu ni nini?
Si kweli.

Ukweli hatuupendi. Niliishi wakati wa Nyerere nauelewa utawala wake. Hakuwa mtawala mzuri kwa namna yoyote ile. Tulikuwa masikini wa mwisho duniani wakati wake. Tulikaa foleni za chakula wakati wake.

Kwanini hatusemi ukweli?
 
Hahahah

Hahahahah umenifanya nicheke, kwamba wakati mwingine huvai nguo!!! do you fly at night? Sometimes uwa una michango ya maana sometimes not, The problem I see in you, you are too emotional. You do not need to use offensive language against those asking irrelevant questions. You can opt to ignore their questions.
I fly at night in the real sense, you can never avoid that when you travel a lot by air. But I never fly in the nude.

I do prefer my baths in the nude. What about you?
 
Back
Top Bottom