Falsafa ya 4R inavyombeba Rais Samia

Falsafa ya 4R inavyombeba Rais Samia

Hayo mambo manne yangekuwa ni murua endapo yangetekelezwa kwa vitendo.

Reconciliation au Maridhiano ni pamopja na kuruhusu wapinzani wafanye maandamano wakiwa huru ili kutoa maoni yao.

Kazi ya polisi katika eneo la maandamano ni kuhakikisha kuwa maandamano hayo yafanyika kwa utulivu na maoni yasikilizwa na yakisha watu hutawanyika na kwenda majumbani kwao.

Maandamano ni haki ya msingi ya kutoa maoni na kuonyesha kuwa demokrasia imekomaa ndani ya jamii na pia huonyesha kwamba serikali ni werevu na wasikivu na wavumilivu.

Resilience au ustahimilivu ni uwezo wa serikali kuendelea na majukumu yake bila kubadili au kutetereka hivyo yale yote yaloachwa na raisi ailetangulia yalipaswa kuendelezwa badala ya kubadilishwa na kupindwapindwa. Miradi mikubwa ya kimkakati bado yasuasua na wizi, ubadhilifu wa fedha za serikali umeshamiri khasa baada ya kauli ya "kula kwa urefu wa kamba".

Rebuilding au ujenzi mpya ni kujenga palipoharibika. Ni kweli huenda kuna maeneo mengi ambayo raisi aliepita alikosea likiwemo suala la uteuzi wa wakurugenzi wa uchaguzi, lakini hili suala laweza kurekebishwa ili kujenga upya usawa, namna haki inavyotendeka na pia ujenzi wa mahusiano mema baina ya wanasiasa. Chadema sasa hivi wadai maandamano na pia umoja wa wapinzani nao wadai hawakushirikishwa na Chadema katika suala la kuandaa maandamano.

Hili laonyesha bado kuwepo kwa nyufa katika siasa hizi za kiafrika na kwamba bado tuna safari ndefu khasa ukizingatia kuwa watu kama Tundu Lissu ameshindwa kuishi Tanzania kutokana na kuwepo kwa makandokando ya hapa na pale.

Reforms au kufanya mabadiliko hili ni jambo muhimu sana kwa nchi yetu. Mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali umekuwa mpana zaidi kiasi cha watu kushindwa kununua sukari na umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara.
Serikali inoongozwa na chama cha mapinduzi yapaswa sasa kubadilika yenyewe ndani yake na kuwa chama chenye mtizamo wa kuwaletea wananchi wote maendeleo.

Mabadiliko yahitajika katika maeneo kama umiliki wa ardhi, makusanyo na udhibiti wa fedha za kodi na vyombo vya serikali, kuamua tuwe na sera zipi za uchumi zinoendana na hali halisi ya dunia kwa sasa.

Kwahiyo, watu wa CCM, mnapokuja hapa na kauli hizi na "statements" ambazo hailingani na hali halisi mwapoteza muda sana.

1. Tendeni Haki

2. Kuweni wazi na dira ya maendeleo ya 2015-2025 ilokuwa ikitekelezwa na hayati JPM.

3. Ruhusu maandamano kwani hayataathiri kitu chochote na sehemu ya haki ya kutoa maoni na kushiriki mikusanyiko.

4. CCM mdhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na mali za serikali.

5. Dhibiti uchumi na mfumuko wa bei.

6. Kamilisheni miradi mikubwa ya kimkakati kama bwawa la Mwalimu Nyerere.

7. Boresheni maisha ya watanzania wanyonge na maskini.
 
Watu wanaongelea haki. Je, tunaweza kujadili ni haki gani inaongelewa?
 
Rebuilding maanake kuna damage ilitokea somewhere mfano ujenzi wa airport vichakati Chato Kitombile na kuvunja mikataba hovyo hado ndege zinakamatwa
 
Zitabaki porojo kama zile sera sijui tuite misemo ya kilimo
Mara uti wa mgongo, mara kufa na kupona na kilimo kwanza
 
Rebuilding maanake kuna damage ilitokea somewhere mfano ujenzi wa airport vichakati Chato Kitombile na kuvunja mikataba hovyo hado ndege zinakamatwa
Mikataba mingi ilikuwa ni ya kinyonyaji na ilikuwa haimfaidishi Mtanzanzania mnyonge na masikini wa chini, ilibidi kuvunja kimabavu ili wazawa waponye rasilimali zao.
 
Mikataba mingi ilikuwa ni ya kinyonyaji na ilikuwa haimfaidishi Mtanzanzania mnyonge na masikini wa chini, ilibidi kuvunja kimabavu ili wazawa waponye rasilimali zao.
Ni kweli tulisaini bogus treaties lakin ni uzembe na uzandiki wa viongozi wetu na mikataba ilitubana hata kuuvunja ilikua kuongeza hasara. Ni bora kunyoosha mikono ila tusirudie kusaini mikataba ya Mangungo
 
Mikatab mfano ya madini ilikuwa inamnufaisha mtanzanania kwa 3% ya mapto, na magufuli akavunja waweke upya mpka ikafika 13% na iikuwa wamepewa kwa miaka 99.
 
Mikatab mfano ya madini ilikuwa inamnufaisha mtanzanania kwa 3% ya mapto, na magufuli akavunja waweke upya mpka ikafika 13% na iikuwa wamepewa kwa miaka 99.
3% ni upuuzi lakin ndio tumejifunga as long as tuliridhia nguvu ya kisheria
 
Back
Top Bottom