Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msemaji wa familia ya hayati Magufuli amesema mpendwa wao kabla ya kufa alibahatika kuongoza sala ya maombi ya kumuombea pamoja na nyimbo.

Pia alipata sakramenti ya toba na mafuta matakatifu.

Kadhalika Mufti wa Tanzania sheikh Zubeir alimuombea.

Katika maisha ya binadamu hii ni neema kubwa ambayo watu wengi huikosa wawapo kufani.

Binafsi sitaomboleza kwa kuvaa nguo nyeusi bali nitavaa nguo nyeupe kwa ajili ya shukrani kwa Mungu kwa maisha ya John hapa duniani.

Maendeleo hayana vyama!
===

Msemaji wa familia ya Hayati Magufuli Ngusa Samike amesema "kabla ya kifo chake Rais Magufuli aliongoza sala na nyimbo akiwa na Madaktari na Wauguzi wake."

Alisema kabla ya kifo pia, "Mwadhama Polycap Kardinali Pengo na Paroko wa Parokia ya St. Peter Padre Alister Makubi walimpatia Rais Magufuli huduma ya kiroho ya mpako mtakatifu,"

"Pia Shekhe Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zubeir naye alimfanyia maombi kabla ya kifo chake."
 
Kuna makosa aina mbili katika imani;

1) Kumkosea Mungu.

2) Kumkosea Mwanaadamu.

Kuna baadhi ya makosa Mungu hasamehi mpaka ukamuombe msamaha uliemkosea kwanza, mfano Kulala na Mke/Mume Wa Mtu. Hapa kwa mungu kosa ni kuzini, kwa mwanaadamu umemchafulia haki yake inayotambulika mpaka mbinguni.

Msamaha kwa mungu unakubalika kwa kuapa kutokurudia tena kosa, sambamba na kurekebisha ulipo kosea (Mfano umefunga mtu gerezani kwa chuki, unapaswa kumwachia huru kwanza na kumpa fidia stahiki kwa kifungo ulichompa, halafu ndio unaomba msamaha kwa mungu na kuapa kutokurudia tena kufunga mtu asie na hatia - Ukiua mtu asie na hatia, unapaswa kukiri kosa na kuwaomba msamaha wana familia kwanza then unarudi kwa mungu kutubia na kuapa kutokurudia tena kuua).

Then walio dhulumiwa na kufungwa magerezani kwa chuki basi aliwaachia kabla ya kutubia dhambi zake?

Alikwenda kuwaomba msamaha familia za waliopoteza maisha yao kwa kivuli cha watu wasiojulikana?

Alirudisha haki za watu waliopewa kesi za uhujumu uchumi ili walipishwe fidia?

Alirudisha haki za watu waliobambikozwa KODI na MAKOSA iwe ya trafik barabarani n.k?
 
Lakini jana wakati anahojiwa na UTV Shekh Mkuu Zuberi alipoulizwa kwamba alipomtembelea wàkati anaumwa Mh. Hayati Rais Magufuli, Shekh alijibu kwamba kwa siku za karibuni toka kuugua kwake sijawahi kumtembelea..."

Hili la wanafamilia kwamba aliombewa na Shekh Zuberi wamelitoa wapi?
 
Lakini jana wakati anahojiwa na UTV Shekh Mkuu Zuberi alipoulizwa kwamba alipomtembelea wàkati anaumwa Mh. Hayati Rais Magufuli, Shekh alijibu kwamba "....kwa siku za karibuni toka kuugua kwake sijawahi kumtembelea..."

Hili la wanafamilia kwamba aliombewa na Shekh Zuberi wamelitoa wapi?
Maombi siyo lazima amtembelee!

Anaweza kumuombea huko huko aliko.
 
Back
Top Bottom