Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

😀😀😀😀 alikuwa na sababu gani ya kuficha kama alikwenda kumfanyia duaa ya mwisho?...si ingempa political and social milage kwa watanzania?
script ya hii movie inaandikwa nusu nusu. Kipindi cha mahojiano ilikuwa kipande cha maombezi hakijaandikwa bado.
 
Angewaomba na msamaha wote aliowakosea.
Toba ni kwa Mungu. Msamaha wa binadamu kwa binadamu kwa mujibu wa mafundisho ya maandiko ni muhimu zaidi kufanywa na aliyekosewa.
Ndio maana wafuasi wa Kristu waliomba na wakafundishwa na Yesu kumuomba Mungu awasamehe kwa kipimo cha wao wanavyosamehe wenzao.
 
Kuna makosa aina mbili katika imani;

1) Kumkosea Mungu.

2) Kumkosea Mwanaadamu.

Kuna baadhi ya makosa mungu hasamehi mpaka ukamuombe msamaha uliemkosea kwanza, mfano Kulala na Mke/Mume Wa Mtu. Hapa kwa mungu kosa ni kuzini, kwa mwanaadamu umemchafulia haki yake inayotambulika mpaka mbinguni.

Msamaha kwa mungu unakubalika kwa kuapa kutokurudia tena kosa, sambamba na kurekebisha ulipo kosea (Mfano umefunga mtu gerezani kwa chuki, unapaswa kumwachia huru kwanza na kumpa fidia stahiki kwa kifungo ulichompa, halafu ndio unaomba msamaha kwa mungu na kuapa kutokurudia tena kufunga mtu asie na hatia - Ukiua mtu asie na hatia, unapaswa kukiri kosa na kuwaomba msamaha wana familia kwanza then unarudi kwa mungu kutubia na kuapa kutokurudia tena kuua).

Then walio dhulumiwa na kufungwa magerezani kwa chuki basi aliwaachia kabla ya kutubia dhambi zake?

Alikwenda kuwaomba msamaha familia za waliopoteza maisha yako kwa kivuli cha watu wasiojulikana?

Alirudisha haki za watu waliopewa kesi za uhujumu uchumi ili walipishwe fidia?

Alirudisha haki za watu waliobambikozwa KODI na MAKOSA iwe ya trafik barabarani n.k?

Wakristo kwani mna hiyo?
 
Msemaji wa familia ya hayati Magufuli amesema mpendwa wao kabla ya kufa alibahatika kuongoza sala ya maombi ya kumuombea pamoja na nyimbo.

Pia alipata sakramenti ya toba na mafuta matakatifu.

Kadhalika Mufti wa Tanzania sheikh Zubeir alimuombea.

Katika maisha ya binadamu hii ni neema kubwa ambayo watu wengi huikosa wawapo kufani.

Binafsi sitaomboleza kwa kuvaa nguo nyeusi bali nitavaa nguo nyeupe kwa ajili ya shukrani kwa Mungu kwa maisha ya John hapa duniani.

Maendeleo hayana vyama!
Walitaka Lissu asipate hii bahati, Azory, Mawazo nna wengine
 
Uamuamini Sheikh muongo muongo kama huyo? Zubeir akikwambia yeye ni mwafrika kataa mpaka uone rangi yake.
Na rangi yenyewe unaeza kukuta amejipaka tu... Andaa maji na steel wire umsugue hadi upate rangi ojirino
 
Tuoneshe ni vifungu gani vya kwenye Biblia vinavyotetea hoja yako.
35 Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Mathayo 22:35-40
 
script ya hii movie inaandikwa nusu nusu. Kipindi cha mahojiano ilikuwa kipande cha maombezi hakijaandikwa bado.
Hii ya Shekh ilikuwa Mubashara Mkuu!...kama ni movie hilo jipya sasa!...lakini Shekh alisema kwa siku za karibuni mpaka amefariki, hakupata nafasi ya kumtembelea iwe hospital au Kwake/Ikulu!
 
Back
Top Bottom