Familia nyingine ni za ajabu sana

hakuna balaa yoyote ni mipangilio tu MAAMUZI
 
Kuuza nyumba sio sawa wazee unajua wame hangaika vip mpaka imepatikana
 
Daah..mkuu nina masikitiko ila imebidi nicheke😂😂😂😂😂
 
Ameeni hata mimi naunga mkono.
Huenda Baba alikuwa anapata pesa zisizo halali huwezi jua.

Kumbuka kuna watu wanapata pesa kwa kushiriki mauaji, utekaji ujambazi.

Hawa watu hata kama unaona wana hela mwisho wa siku hawana furaha. Kama ambavyo mleta mada ameelezea baba yake alikuwa mtu wa huzuni tu.
 
Ndio maana mnaambiwa zaa Watoto Kwa wanawake tofauti tofauti ni likely ukapata waelewa kuliko kuzaa Kwa mwanamke mmja kama kwao Kuna laana Watoto wote wanaweza kuwa hivyo hivyo.

Alternative two zaa Watoto wengi hata kama ni Kwa mwanamke mmja hawatafanana tabia tofauti na kuzaa wachache wakaishia kuwa mataahira kama hao ndugu zako.
 

Hawawezi kuwa na Mabalaa yote haya.
 
Pole sana,ni kama mimi Upande wa mama....wao wamezaliwa 9 lakini wanaomtazama na kumkumbuka bibi ni mama na uncle tu....saba wako busy na mambo yao.sometimes kuzaa watoto wengi ni kujitwisha mzigo wa kaburi la mapema
Kabisa mkuu yani hawa mabro ndio wamemuwaisha mshua kaburini inasikitisha sana halafu mshua aliwalea kishua maana wao wamemkuta mshua bado akiwa kijana na ananguvu za utafutaji
 
Kama kuna uwezekano, mchukueni bi Mkubwa muishi nae alaf nyumba pangisheni. Haya majamaa yaachieni chumba kimoja.

Hakikisheni hati na documents muhimu za nyumba mnazitoa hapo home. Baada ya hapo, hakuna tena sababu ya kuwatumia hela ya matumizi
Na hili ndio suluhisho, sema namuelewa jamaa changamoto anazopitia, ndani ya hizi familia zetu na ukoo kuna mambo sana. Ni basi tu kuta za nyumba zetu zinahifadhi mengi.

Pole sana mtoa mada, ushauri wangu endelea kujitoa kwa mama, kila unachofanya chukulia unakitoa kwa ajili ya mama, au fanya kama alivyoshauri hapa juu.

Usisikitike sana unajizibia baraka kwa Mungu sadaka yako inakuwa ngumu kupokelewa, unachokitoa kitoe kwa moyo huku unachukua hatua kulikabili. Ndio ukubwa
 

vijana wanaishi kwenye nyumba za kupanga dar wamchukue mama yao kutoka mkoani ambae yupo kwenye 70s waje waishi nae Dar kwenye nyumba ya kupanga?

Are u serious?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…