Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Picha ilianza na Mimi. Nilibahatika ya kufaulu na kwenda shule nzuri tu ya sekondari ambako pia nilifauli kwenda masomo ya juu. Nikiwa nimekomaa na masomo ya biashara, ndoto kuu ilikuwa kuja kuwa mfanyakazi wa taasisi flani za kifedha.
Tena huko zinakotokea. Leo hii ni mwalimu ninayefundisha Jiografia na Kiingereza, mwaka zaidi ya wa 10 kazini, hakuna gari hakuna nyumba hakuna heshima nyumbani.
Ndugu yangu, akiwa ameyashika vizuri masomo ya Sayansi hadi kidato cha tano na kuwa na ndoto lukuki za kuwa daktari. Ghafla bin vuu nae Sasa huu mwaka wa 5 anasotea kazi tu ya ualimu bila mafanikio. Ni ualimu wa shule ya msingi nauzungumzia ndugu wanaJF
Ndugu mwingine baada ya kufika kidato cha nne alikuwa na ndoto ya kuwa askari. Sasa hivi anakesi mahakamani baada ya kumgonga mtu akiwa katika shughuli zake za bodaboda.
Dada zangu wote wapo nyumbani, shuleni hata somo la kirai kwao halikupanda. Wapo tu nyumbani wanachoma mkaa.
Binti yangu, nikiwa nimejaribu kuweka nguvu nyingi sana na kwa muda mrefu Kwakweli Ili asome, tena masomo haya ya sayansi (kutokana na uelekeo wa Dunia kwa Sasa); hajui hata 1 + 1 jibu ni ngapi, hajui Archimedes principle Wala Newtown's 1st law of motion.
Nikiwa mfariji na mtegemewa mkuu wa familia yetu hii, najihisi kuchanganyikiwa. Wanaotegemea pia nao wanachanganyikiwa siku baada ya siku. Tuko vururu vururu, hakuna ndoto tena.