Familia sita zavamiwa, wanne wajeruhiwa kwa mapanga Dar

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Dar es Salaam.

Familia sita zinazoishi mtaa wa Kwembe Mpakani jijini hapa, zimevamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu, wakiwa na mapanga nondo na mawe kisha kuwajeruhi watu wanne na kupora vitu mbalimbali.

Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia juzi ambapo vijana zaidi ya kumi, walivunja mlango mmoja baada ya mwingine na kuamuru kupatiwa fedha na simu.

Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Mei 20, 2022 wananchi hao waliojeruhiwa wamesema, majira ya saa tisa usiku vijana hao wakiwa na mapanga, nondo na mawe walivunja milango na kuamuru kupewa fedha na simu.

Godfrey Kimaro aliyejeruhiwa kichwani amesema, usiku wa kuamkia juzi wakiwa wamelala, alishtuka kusikia mlango wa jirani ukigongwa kwa nguvu, lakini alijua ni mwenzao anawaamshwa wakalinde.

Amesema kabla hajakaa sawa alisikia kishindo cha nguvu, lakini wakati anataka kutoka nje, mke wake alimkataza na ndipo aliposogeza kitanda mlangoni kisha kupanda juu na kuchungulia na kuona kundi la vijana zaidi ya kumi.

“Nilisikia wakisema toa hela na wakati huo watu wanalia, walipomaliza waliingia chumba kingine ndipo niliposikia mmoja wao akisema, bado chumba hiki (cha kwangu) walivunja mlango na mimi nilijaribu kuzuia lakini ilishindikana,”amesema Kimaro.

“Baada ya kuingia ndani walinipiga panga la kwanza kichwani, kisha wakanivuta nje na kunipiga panga la pili, walifanikiwa kuchukua simu mbili, flashi mbili, waleti iliyokuwa na kitambulisho na kadi ya benki pamoja na Sh 50, 000,”amesema.

Akisimulia mkasa huo majeruhi mwingine, Ismail Mande amesema akiwa amepumzika baada ya mihangaiko ya kutwa nzima alisikia kelele jirani, ndipo alipoamua kuamka na kuchukua panga kama shemu ya kujihami.

Amesema akiwa anasikiliza kinachoendelea alisikia mlango ukigongwa na kitu kizito, ndipo walipofanikiwa kuingia akiwa ametaharuki alisikia kitu kimemgonga kichwani lakini hakujua kama ameumia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhani Kingai amesema, tukio hilo ni la kiuhalifu kama yalivyo matukio mengine na halihusiani na Panya Road.

“Tusizue taharuki kwa wananchi, sio kila tukio la kihalifu ni panya road kilichotokea Kwembe ni watu kuvunja nyumba, kujeruhi na kuiba,” amesema Kingai.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi mtandaoni
 
Yaan ni kutaka kusema vyombo vya ulinzi vimeshindwa kulinda raia wake na mali zao ? Hili jambo lina sikitisha sanaa
 
Kwani wakisema ni panya road shida iko wapi
 
Yale maeneo ya pembezoni ambayo watu hukaa mbalimbali, Serikali iangalie namna ya kufanya kwa kuhakikisha doria za mara kwa mara hasa kwa kutumia vijana wa JKT...

Yale maeneo ambayo kuna makazi ya watu wengi wanaokaa karibu karibu kama Goba, Bunju, Madale, Boko...nk huko Serikali ifanye uchunguzi kwa watu na kuwapa silaha mfano kila nyumba kumi basi kunakuwa na silaha za moto nyumba hata tano..... Wajumbe wa hiyo mitaa na wenyeviti wanakuwa na kamati zao za ulinzi na usalama na kufanya doria za mara kwa mara mitaano..
Wenye mitaa inayojiweza waajiri vijana na makampuni binafsi ya ulinzi kulinda mitaa yao..

Polisi kwa upande wao, mchana na usiku wadeal na hawa vijana na wakiwatia mkononi ni kutoa roho zao tu kinyama..
 
Back
Top Bottom