Familia tata

5 iliyopita
Mzee Komba na familia
yake walishiriki kila hatua
ya tukio lile na mzee Linus
na familia yake nao
hawakuonyesha kinyongo
chochote, wote waliamini
kilichotokea ilikuwa ni
mipango ya Mungu.
SASA ENDELEA...
Juddy alizikwa siku nne
baada ya kufariki katika
tukio lililokusanya umati
mkubwa wa watu, kwenye
makaburi ya Nakasangwe!
Watoto wa familia zote
mbili walishiriki kikamilifu
shughuli ile ya msiba na
walikaa nyumbani kwa mzee
Linus kwa siku zote, hadi ya
saba, wakati walipokaa kikao
cha pamoja kujadili
kilichotokea na mzee Komba
ndiye alikuwa mwenyekiti wa
kikao kile.
“Rafiki, kaka yangu, shemeji
yangu na wanangu wote wa
nyumba hii, kwa niaba ya
familia yangu, tunaomba
kuwaomba radhi kwa yote
yaliyotokea, lakini tunaamini
ni kazi ya Mungu ambayo
siku zote haina makosa,”
Mzee Komba alisema huku
akijifuta machozi, kitendo
ambacho pia kilifanywa na
watu wote, hasa Asfat,
aliyesafiri kutoka Ulaya kuja
kuhudhuria mazishi ya rafiki
yake mkubwa!
“Usijali kaka, rafiki, jirani na
wanangu wote. Kama
ulivyosema, hili ni tukio
ambalo hakuna
aliyelitegemea, huu msiba
ni wetu wote kama ambavyo
tumeshuhudia, wote
mmeshiriki kikamilifu tokea
mwanzo hadi sasa. Nyinyi ni
sisi na sisi ni nyinyi, haya
yamepita, sasa tujitahidi
kumnusuru Tonny, ni kijana
mdogo aliyetaka
kuwachekesha wenzake
lakini matatizo yakatokea,”
Mzee Linus naye alisema,
huku watu wote wakiendelea
kujifuta machozi!
Walijadili mambo mengi
sana kama familia marafiki
na hatimaye baadaye
wakakubaliana kuondoa aina
yoyote ya chuki baina yao.
Wakasimama na kushikana
mikono. Wakati wa tendo
hili, wote waliendelea
kutokwa na machozi.
Tonny alikaa polisi kwa siku
tatu, baadaye akapelekwa
katika mahakama ya watoto
Kisutu jijini Dar es Salaam
ambako alisomewa shtaka la
mauaji ya bila kukusudia. Na
baada ya kusomewa
mashtaka yake ambapo
hakutakiwa kujibu chochote
kwa kuwa mahakama ile
haikuwa na uwezo wa
kusikiliza kesi hiyo,
akapelekwa Segerea.
Wazazi walimtafuta
mwanasheria aliyekuwa
akitamba sana jijini Dar es
Salaam, Bennedict ili aweze
kumsimamia Tonny. Kazi
hiyo hata hivyo haikuwa
ngumu sana kutokana na
wazazi wa marehemu nao
kupigana kwa nguvu zote
kuhakikisha kijana huyo
anaachiwa!
Tonny aliachiliwa huru
baada ya miezi mitatu tu na
alipotoka mahakamani,
alikwenda moja kwa moja
nyumbani kwa akina Juddy
akiwa analia!
Kilio chake kiliashiria majuto
aliyokuwa nayo. Hata hivyo,
wote walionyesha moyo wa
huruma dhidi yake na
akaomba apelekwe kaburini
kwa Juddy ili akaweke shada
la maua.
Ombi hilo likakubaliwa na
familia zote zikapanga
kitendo hicho kifanyike
kesho yake ambayo ilikuwa
ni Jumapili ili wengine pia
wahudhurie.
Makaburini, Tonny alipiga
magoti katikati ya kaburi la
Juddy, akachukua mshumaa
na kuuwasha, akalibusu
shada lake la maua na
kuliweka, kisha machozi
yakaanza kumtoka.
Wanafamilia wengine
waliomsindikiza nao
waliweka mashada yao na
kupiga magoti. Mwishowe
wote kwa pamoja walisali na
kuondoka!
Asfat akarejea zake shuleni
Ulaya na ndugu wa familia
zingine wakaendelea na
maisha yao ya kila siku.
Hakukuwa na tofauti yoyote
kati ya familia hizi kwa
kipindi kirefu.
Mwaka mmoja na miezi sita
baada ya kifo cha Juddy,
maisha yalikuwa katika
mtindo wake wa kawaida
kabisa kwa familia hizi
rafiki.
Baptist, ambaye alimuachia
ziwa Juddy, alikuwa akitoka
mjini kutengeneza gari lao
lililokuwa limeharibika
mfumo wake wa umeme
eneo moja la Gerezani, jijini
Dar es Salaam. Wakati
akirejea nyumbani alikuwa
na mawazo mengi.
Katika umri wake wa miaka
25, alikuwa mtu wa
kujirusha sana katika
maeneo ya starehe. Ilikuwa
ni lazima aende klabu kila
mwisho wa wiki na hii
ilimfanya kuwa na marafiki
wengi wa kike na kiume.
Lakini sifa yake kubwa
ilikuwa ni tabia yake ya
kuendesha gari kwa mwendo
kasi. Hata kama alikuwa
akienda sehemu ya karibu,
alipenda kulikimbiza...
Je, kitu gani kilitokea?
Usikose kufuatilia simulizi
hii ya kusisimua katika
toleo lijalo.
 
Kazi kweli kweli Kama ndio mambo haya!
 
6 Ilipoishia:
Lakini sifa yake kubwa
ilikuwa ni tabia yake ya
kuendesha magari kwa
mwendo kasi. Hata kama
alikuwa akienda sehemu
ya karibu, alipenda
kulikimbiza...
Sasa Endelea...
Mama yake Tonny alikuwa
uani kwake akifua nguo za
mtoto wake wa mwisho,
Subby wakati akitaniana na
kaka yake Tonny aliyeitwa
Santo. Santo alikuwa
akisoma darasa la saba
katika Shule ya Msingi
Bunge na siku hiyo ya
Jumamosi, hakwenda shule.
Mama Tonny alikuwa
akimpenda sana Santo na
mara nyingi walikuwa
wakitaniana. Leo, wakiwa
hapa, mama alikuwa
akimshambulia Tonny
kwamba ni lazima atafeli
kwa sababu ya kupenda
sana filamu. Na kweli, Santo
alikuwa shabiki mkubwa wa
filamu, hasa za Kizungu,
ingawa pia alivutiwa na zile
za Kihindi na Kibongo.
Baada ya kuzidiwa utani na
mama yake, Santo akaamua
kuondoka lakini akamvizia
akiwa amejisahau,
akamtekenya kwenye mbavu.
Mama alipata mshtuko
mkubwa na akiwa na hasira,
aliinuka na kuanza
kumfukuza kijana wake
aliyekuwa anakimbilia nje ya
geti!
***
Baptist alikuwa anakata kona
maarufu mtaani kwao
iitwayo Kwa Kipira, akiwa
katika mwendo wa kasi kama
kawaida yake. Mtaa ulikuwa
kimya na hakukuwa na mtu
barabarani. Akiwa anakaribia
kwenye geti la nyumba ya
Mzee Komba, ghafla
akamuona mtu akitokeza
kwa kasi na kuingia
barabarani.
Hakuweza kujizuia,
hakuweza kulizuia gari,
kishindo kikubwa kikasikika
na mtu mmoja alionekana
akirushwa juu na
alipoanguka chini, akabakia
kuwa mtulivu pale chini
alipofikia.
Alikuwa ni Santo!
Kishindo kile kilileta kelele
kubwa mtaani na mara
moja, kila mtu aliyekuwepo
alitoka nje ya nyumba ili
kushuhudia kilichotokea.
Bap alifanikiwa kusimamisha
gari mita chache mbele,
akatoka nje ya gari na
kumkimbilia mtu
aliyemgonga!
Kishindo kile kilikuwa kama
nyundo iliyopiga katika
kichwa cha mama yake
Tonny, alitambua kabisa
kwamba aliyegongwa ni
mtoto wake. Naye pasipo
kutarajia alianguka na
kupoteza fahamu muda
uleule mwanaye
alipogongwa.
Ndani ya dakika moja, watu
wengi walijazana pale
alipokuwa amelala Santo,
mwili wake ulijaa damu na
watu wakawa kama
waliochanganyikiwa. Kwa
muda wakawa hawajui
wafanye nini hadi akili
zilipowarejea.
Baptist alikuwa wa kwanza
kumshika Santo, akamgeuza
vizuri na kumtazama, akatoa
ishara kwa wenzake
wambebe, wakampakia
kwenye gari alilomgonga
nalo. Watu wengine wawili
wakaingia ndani ya gari lile,
kwa kasi ya ajabu,
likaondoka kuelekea
hospitalini!
Watu wengine nao mtaani
wakawasha magari yao na
kulifuatilia gari lililombeba
Santo. Baptist aliendesha
gari kwa kasi hadi alipofika
katika Hospitali ya Mico
iliyopo Tegeta Basihaya.
Madaktari wakampokea
haraka mgonjwa na moja
kwa moja akapelekwa
chumba cha upasuaji!
Nyumbani kwa akina Santo,
baadhi ya majirani
walishtuka baada ya
kumuona mama yake Santo
akiwa amelala chini, tena
kwa namna ya kutisha.
Walipomchunguza,
wakagundua kwamba
alikuwa amepoteza fahamu.
Wakamfanyia huduma ya
kwanza, kisha wakambeba
na kumwingiza ndani kwake.
Alirejewa na fahamu baada
ya nusu saa, akashangaa
kuona watu wamemzunguka
sebuleni alipolala kwenye
kochi.
“Vipi?” aliwauliza wanawake
wawili waliokuwa karibu
yake, akiwemo mama yake
Juddy.
“Tulia, tuliza akili kwanza,
upo salama?” mama Juddy
alimwambia mwenzake huku
akimtengeneza vizuri kanga
zake alizojifunga.
“Kuna nini kimetokea dada,
niambie haraka,” mama yake
Santo alimwambia mama
Juddy huku akimshika
mikono yake kwa nguvu
kubwa.
“Tumekukuta umeanguka
pale mlangoni kwako, ndiyo
tukakubeba na kukuingiza
ndani,” alijibiwa!
“Mnenikuta nimeanguka?”
aliuliza tena na kuanza
kuvuta kumbukumbu.
Je, nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii
katika toleo lijalo.
 
Dah,hizo familia tata kweli wanaweza teketezana hawa tusipowasaidia kwa kuhamisha familia moja.
 
Itaendelea lini? Kama majirani zako nakushauri hama mtaa huo!
 
7 iliyopita
“Tumekukuta umeanguka
pale mlangoni kwako,
ndiyo tukakubeba na
kukuingiza ndani,”
alijibiwa!
“Mmenikuta
nimeanguka?” aliuliza
tena na kuanza kuvuta
kumbukumbu…!!!
Sasa endelea...
Baada ya kumfikisha
hospitalini alikopokelewa,
Baptist akachukua simu yake
na kumpigia baba yake
mzazi, mzee Linus.
“Shikamoo baba,” Baptist
aliongea mara tu
ilipopokelewa.
“Marahaba, tunakaribia hapa
hospitali, vipi hali yake,”
mzee Linus alijibu, kauli
ambayo ilimshangaza sana
Baptist, hakutegemea kama
mzee wake alishataarifiwa.
Ukweli ni kwamba mama
yake, alimpigia simu na
kumweleza kilichotokea
mara tu walipoondoka
nyumbani kuelekea
hospitali.
Naye mzee Linus
aliwasiliana na rafiki yake.
Bahati nzuri, mzee Komba
alikuwa Bahari Beach Hotel
alikokuwa na kikao cha
kikazi na washirika wake
kibiashara, wakati mzee
Linus alikuwa akirejea
kutoka shambani kwake
Mapinga, alikuwa akikaribia
Bunju, njia ya kuelekea
Bagamoyo!
Wakakubaliana kukutana
hospitali.
***
Mama Tonny alivuta
kumbukumbu zake vizuri
akiwa amejiinamia chini.
Kwa mbali akakumbuka
kuhusu kilichotokea.
Kishindo cha kugongwa na
gari mtoto wake kikajirudia
tena akilini mwake, akapiga
ukulele..
“Mamaaaaaa!”
Watu wote waliokuwa
sebuleni hapo wakashtuka,
mama yake Juddy akawahi
kumshika mkono na
kumtuliza.
“Vipi mwenzangu?” aliuliza
“Santoo, Santooo,
mwanangu Santooo jamani,”
mama Tonny alianza
kuangua kilio, Mama Juddy
akamshika vizuri na
kumtuliza, akazidi kupiga
kelele na kuuliza alipo
mwanae.
“Amepelekwa hospitali.”
“Wamempeleka yeye au
maiti yake?” aliuliza huku
akiuma meno kwa uchungu,
hakuamini kama mwanae
alikuwa mzima.
“Mzima kabisa dada, wala
usiogope,” mama Juddy
alijitahidi kumfariji.
“Nataka kwenda, nataka
kwenda, sasa hivi,” alisema
na kuinuka, wanawake
wenzake walijaribu kumzuia,
lakini akawashinda nguvu,
asijue hospitali
waliyokwenda, akatoka nje
ya geti na kuanza kutimua
mbio akiwa pekupeku bila
viatu.
Bahati nzuri kulikuwa na
vijana wa kiume mtaani
hapo ambao bado walikuwa
katika vikundi wakijadili
tukio hilo, wakaambiwa
wamkamate asije kupata
madhara zaidi.
Zoezi lile halikuwa kubwa,
vijana kadhaa wenye ubavu
walimkimbiza mama kidogo,
na kumkamata na kumsihi
atulie, kwani tayari akina
baba walikuwa wameshafika
hospitalini, na taarifa
zilizoletwa muda huo
zilisema Santo alikuwa bado
chumba cha upasuaji.
Kwa unyonge mama
akakubali kurudi nyumbani,
lakini akiwa anatoa kilio
kikubwa. Vijana wale
walimuongoza nyumbani
wakijaribu kumpa
matumaini.
***
Baptist aliwafuata mzee
Komba na baba yake
waliokuwa wamekaa kwenye
benchi wakizungumza kwa
huzuni.
“Inabidi niende polisi kutoa
taarifa za ajali,” aliwaambia
huku naye akionekana kuwa
mwenye huzuni kubwa.
“Sawa, nenda kituo cha
Wazo, halafu kitakachotokea
utatuambia,” alisema mzee
Linus.
Baptist akaendesha gari kwa
kasi kama kawaida yake hadi
Kituo Kidogo cha Polisi
Wazo. Alijua haitakuwa
rahisi kutoka wakati ule,
akatafuta sehemu nzuri na
kuegesha, akasogea kaunta
ya polisi na kueleza tatizo
lake kwa askari aliyekuwa
zamu.
“Zunguka, vua viatu, saa,
mkanda, afande, mfungulie
mlango huyu, kaua,” askari
aliyekuwepo kaunta alisema
kwa sauti kubwa, hali
iliyosababisha watu wote
waliokuwa jirani kumtazama
Baptist aliyekuwa sasa
anazunguka kuingia kaunta.
“Kwani imekuaje?” alisema
askari mwingine aliyekuwa
ndani, ambaye alionekana
kama ndiye mkubwa, kuliko
yule aliyekaa kaunta. Akataka
kijana yule aingie ofisini
kwake.
Baptist akaingia,
akakisogelea kiti kilichokuwa
kinatazamana na kile cha
ofisa wa polisi, akakaa.
Ofisa huyo akataka kupata
maelezo ya nini hasa
kimetokea.
Baptist akamuelezea kuanzia
mwanzo hadi mwisho.
Askari akatingisha kichwa.
Akachukua mkono wa simu
ya mezani, akabonyeza
namba kadhaa kisha
akauweka sikioni.
Je, nini kitatokea? Usikose
kufuatilia simulizi hii ya
kusisimua katika toleo
lijalo.
 
Reactions: amu
Mkuu Luthar kulikoni kahadithi ketu bhana au mmewahamisha hao wazee!
 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha sana. Nahisi kwanza ndo story inaanza na makubwa zaidi yaja.
 
samahani wajameni twaweza kuendelea wazeeya
 
Ilipoishia wiki iliyopita…
Baptist akamuelezea
kuanzia mwanzo hadi
mwisho. Askari akatingisha
kichwa. Akachukua mkono
wa simu ya mezani,
akabonyeza namba kadhaa
kisha akauweka sikioni.
Sasa endelea...
“ Hebu askari watatu waje
ofisini mara moja,
wanatakiwa kwenda kupima
ajali Nakasangwe na halafu
kuangalia maendeleo ya
majeruhi hospitalini
haraka..,” ofisa yule wa
polisi aliongea kwenye simu
na kisha kurudisha mkonga
sehemu yake.
Dakika moja baadaye, askari
watatu, akiwemo mwanamke
mmoja walikuwa ofisini
hapo, wakapewa maelekezo,
kisha wakainuka pamoja na
Baptist na kuelekea kwenye
gari la Polisi aina ya Toyota
Land Cruiser, maarufu kama
Difenda. Wakakanyaga moto
hadi eneo la tukio.
Wakachukua vipimo pamoja
na kupata vidokezo kutoka
kwa majirani ambao sasa
walikuwa wengi
wamejikusanya ilipotokea
ajali na nyumbani kwao
mzee Komba, wengi
wakiulizia maendeleo ya
majeruhi.
Baada ya kumaliza shughuli
hiyo, wakawasha gari
wakiwa na Baptist na
kuondoka kuelekea hospitali
alikolazwa majeruhi.
Wakaomba kukutana na
daktari aliyempokea
mgonjwa na kutaka kujua
hali yake.
“Ana hali mbaya sana
afande, sidhani kama
atapona,” daktari
aliyempokea na
kumshughulikia Santo
aliwaambia askari wale
alipowakaribisha ofisini
kwake na wao
kujitambulisha.
“Ameumia kwa kiasi gani,?”
askari kiongozi wa msafara
aliuliza. Kabla daktari huyo
hajajibu chochote, simu
yake ya mezani ikaita.
Akatoa ishara ya kumtaka
radhi, akainua mkonga wa
kuongelea na kuuweka
sikioni, alisikiliza kwa
sekunde chache kabla ya
kuurudisha mahali pale.
“He is dead (amefariki),”
alisema huku akitoa miwani
yake na kuifuta kwa
kitambaa chake cheupe!
***
Vilio viliripuka nyumbani
kwa mzee Komba mara tu
taarifa za kifo hicho
zilipopelekwa. Alikuwa ni
mzee huyo aliyempigia simu
mtoto wake mkubwa wa
kiume, akimfahamisha tukio
hilo la kusikitisha. Mama
yake Tonny alipoteza
fahamu mara tu alipofuatwa
na mtoto wake na
kumweleza kuwa kule
hospitalini, Santo amefariki
dunia!
Taarifa za kifo hicho
zilisambaa kwa kasi kubwa,
ndugu mbalimbali wa ndani
na nje ya nchi waliarifiwa na
zilipomfikia Asfat, ambaye
sasa alikuwa ameshamaliza
masomo na akijiandaa kwa
safari ya kurejea nyumbani
Tanzania, hakuamini.
“What?” aliuliza wakati
alipopokea simu ya kaka
yake, Amani, aliyemtaarifu
juu ya msiba huo.
“Ndiyo hivyo sista, bahati
mbaya,” Amani alisema kwa
upole.
Asfat hakutaka kuamini
kirahisi kama kifo kile
kilikuwa bahati mbaya,
akilini mwake aliona huenda
kilikuwa ni kisasi, hivyo
akataka maelezo ya kutosha
kutoka kwa kaka yake.
“Kaka Amani, slowly please
(taratibu tafadhali), hebu
niambie vizuri, una uhakika
kaka Baptist kamgonga
Santo kwa bahati mbaya?
Sitaki kuamini, naona kama
kisasi fulani hivi, wewe
unaonaje?” Asfat aliongea
huku akiwa ameuma meno.
“Hapana dada Asfat, ni ajali.
Santo alikuwa na mama
uani, wanataniana, si
unawajua walivyo, sijui
ilikuwaje wakaanza
kufukuzana, Santo
akakimbilia nje, sasa ile
anatokeza tu mlangoni na
Baptist anapita, si unajua
anavyoendeshaga, hakujua,
hakumuona, hakuna hata
mtu mmoja anayemlaumu
Bap, ni ajali dada, amini
ninachokuambia, ambacho
najua hata mama
atakuambia hicho hicho,”
Amani alijaribu kumtuliza
dada yake.
Asfat akakubali, lakini
hakuridhika!!!!…
...Baptist akaondoka na
askari wale kurejea kituoni
Wazo, ambako aliwekwa
mahabusu na baadaye
kufunguliwa jalada la ajali
iliyosababisha kifo.
Pale hospitalini, mzee
Komba na mzee Linus
wakaanza taratibu za kuutoa
mwili ili uende kuhifadhiwa
hospitali yenye majokofu ya
kuhifadhia maiti. Majirani
wengine kadhaa nao
walikuwa wameshawasili
hospitalini hapo kwa
msaada wowote unaoweza
kuhitajika.
Mzee Komba akashauriwa
kurejea nyumbani ili aweze
kupumzisha akili sambamba
na kupokea wageni, kazi ile
ya kushughulika na mwili wa
marehemu ikaachwa
mikononi mwa mzee Linus,
akishirikiana na vijana wa
familia zote mbili.
Je, nini kitaendelea?
Usikose kusoma sehemu
inayofuata ya simulizi hii
ya kusisimua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…