Familia ya Diamond yatilia shaka mimba ya Zari

Familia ya Diamond yatilia shaka mimba ya Zari

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Familia ya ‘President' wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari' ni ya kwake au magumashi.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli.


"Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari.

"Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake," kilisema chanzo hicho

WALITAKA ATOE MSIMAMO

"Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika mitandao na vyombo vya habari,'' kilisema chanzo hicho.

SABABU ZAZIDI KUANIKWA

Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny' na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga.

"Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi, waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika," kilisema chanzo hicho.

MUAFAKA WA KIKAO

Chanzo hicho kikizidi kumwaga ubuyu mbele ya kinasa sauti chetu kwamba, baada ya Diamond kubanwa na nduguze, alithibitisha kuwa Zari ndiyo kila kitu kwake kwa sasa, hivyo wasiwe na shaka yoyote juu ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa.

"Diamond aliwahakikishia kwamba mzigo ni wake, na msimamo wake ni kufika katika hatua ya ndoa Mungu akijalia.

KUMVISHA PETE

"Kuonesha yupo serious baada ya Diamond kuwatoa hofu ndugu zake, alisema atafanya sapraiz siku ya Mei Mosi katika shoo ya mrembo huyo, All White Party itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar," kilisema chanzo hicho na kudokeza kuwa Diamond atamvisha pete mrembo huyo.

DIAMOND AFUNGUKA

Ili kuweza kupata ukweli, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond ili aweze kuweka wazi juu ya kikao hicho na kama ni kweli anatarajia kumvisha pete Zari. Diamond alifunguka:

"Yeah ni kweli ndugu zangu walikuwa na shaka lakini nimewahakikishia kwamba kiumbe kilichomo tumboni mwa Zari ni mali yangu, kuhusu kumvisha pete ni mapema kidogo kulizungumzia, lakini watu wahudhurie kwa wingi katika shoo ya Zari White Party Ijumaa hii pale Mlimani City kwani nimeandaa sapraizi nyingi sana.
 

Attachments

  • 1430287911816.jpg
    1430287911816.jpg
    60.3 KB · Views: 2,693
Bosheni tupu,wenye mzigo wametulia zao uganda,mtu unaangaika bure wakati penny aliweka mambo wazi, atajibeba
 
kitu unanunua mbuzi ndani ya gunia au unauzia mzigo bosheni wakati wenye mzigo wametulia zao uganda. huyu dogo atakuja kulia ka mtoto nyie subirini tu
 
Wametisha IG wameandika ticket za 3mil na 1mil sold out aisee wako vizuri sio mchezo
 
Bosheni tupu,wenye mzigo wametulia zao uganda,mtu unaangaika bure wakati penny aliweka mambo wazi, atajibeba

Katunzi katulia tulii anasubiria mbegu yake, huyu ngonyani mwache auzie sura mimba za watu maana hana uwezo wa kumpa mwanamke mimb
 
Namuonea huruma dah

mie hata simuonei huruma.....shimo analichimba mwenyewe..asubiri kujidumbukiza...kuna vina vingine sio vya kuogelea..utazama buuure....mi naonaga ka ushamba bado unachangia...yaani kupembua chuya na mchele inakua ngumu
 
Diamond yupo kibiashara zaidi. Utakuta anajua kabisa mimba siyo ya kwake.
 
Jamani mboou hizi, sijui tutazigombea mpaka lini.
warumi nipe yako iwe yangu peke yangu
 
Last edited by a moderator:
Tusubiri mtoto azaliwe basi ndio tutajua moja.Maneno hua mengi wakati wa mimba lakini mtoto akishazaliwa ndipo majibu hupatikana.
 
Back
Top Bottom