Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Tangu alivyokuwa hai JPM mlimchonganisha na mzee Kikwete, amefariki bado hamtosheki tuu? Mwacheni apumzike kwa amani. Lakini Mhe. Kikwete amestaafu bado maneno dhidi yake mengiii huyu atasema vile na huyu hivi. Mwacheni inatosha.

Kuwapenda watu wa Tanga ambao ni raia wake lilikuwa kosa? Hakuna Rais wa nchi hii amewahi kuchukia raia wake kutoka pande zote za Tanzania Bara na Zaznibar. Tulete mada fikirishi kuhusu namna tunavyoweza kuogelea katk dunia hii ambayo ni kijiji. 🙏🙏🙏
Mkapa aliwachukia wamakonde wenziwe.
JPM aliwachukia wachaga na nduguze wahaya
 
Alikuwa mzalendo wa kweli, mola ailaze roho yake mahali pema peponi!
Uzalendo ni kuiba 1.5 trilioni?

Uzalendo ni kuwabambikia watu kesi, kisha kuwapora pesa zao, na baadaye yeye binafsi kuzipora?

Uzalendo ni kuteka, kuua na kupoteza watu wenye kumkosoa?

Hivi kwa tafsiri yako mtu mzalendo ni mtu mwizi na anayeonea watu?
 
Mkuu,hata kama ni Mimi ningefanya hivo hivo,hata siku nikipata fursa ya kupenya mafisadi watakoma sana!!

Nchi hii mlipa kodi wa uhakika ni mtumishi wa umma na wajasiria Mali wadogo wadogo !!

Haiwezekani watz hawafurahii matunda ya NCHI yao full kukandamizwa KWA kodi HUKU mafisadi yakitamalaki

KWA hili I stand with him!

Mungu ibariki nchi yangu Tanzania!
Ukiwa na mawazo hayo huwezi kupata, labda ujifanye fisadi mwenzao halafu ukikalia kiti ndio uwageuke, Ila usisahau kovid ya bagamoyo huenda ikakuhusu
 
Naskia manji alimwambia mi "apana ongea na mbwa,iko ongea na yenye mbwa,!!
Alipobananishwa kupimwa mkojo alikoma!!nafanza nini bana gufuli
Manji hawezi kumsahau Jpm
 
Sasa wamerudi upyaaaaaa!
Sio kurudi upya. Wanarudi kwa nguvu kubwa kabisa. Tena inasemekana gsm anaongeza viwanda vipyaaaaa. Vya vinywaji, mafuta ya kula, sabuni, chuma/nondo na kuongezea malori mengine 🙌🏿🙌🏿🙌🏿🙌🏿

Achana na kitu inaitwa hela. Nasubiria comment ya popoma mwandamizi genta, nimekaa paleee 👉🏿👉🏿
 
Hata mimi ningekuwa na kampuni, halafu kukatokea upenyo wa kukwepa kodi! Aisee ningekwepa kwa moyo mkunjufu kabisa.

Maana hizo kodi zenyewe kwa sehemu kubwa zinawanufaisha watu wachache tu.
Ni kama hao ambao Magufuli aliwabana na kuwatisha, halafu baada kulipa, yeye Magufuli binafsi akaziiba hizo fedha zote.
 
Uzalendo ni kuiba 1.5 trilioni?

Uzalendo ni kuwabambikia watu kesi, kisha kuwapora pesa zao, na baadaye yeye binafsi kuzipora?

Uzalendo ni kuteka, kuua na kupoteza watu wenye kumkosoa?

Hivi kwa tafsiri yako mtu mzalendo ni mtu mwizi na anayeonea watu?
Haya ni maneno wanayokaririshwa watu ili wamchukie JPM, yule jamaa asingekufa hii nchi ingeendelea sana kiuchumi....now hamna namna, tuendelee tu kuongozwa na mifisadi.
 
Haya ni maneno wanayokaririshwa watu ili wamchukie JPM, yule jamaa asingekufa hii nchi ingeendelea sana kiuchumi....now hamna namna, tuendelee tu kuongozwa na mifisadi.
Nchi hii mafisadi wapo kila awamu,ukisoma ripoti ya CAG utashangaa sana ilikuwaje wakathubutu kupiga hela mbele ya JPM,tena walipiga aswaa
 
Uzalendo ni kuiba 1.5 trilioni?

Uzalendo ni kuwabambikia watu kesi, kisha kuwapora pesa zao, na baadaye yeye binafsi kuzipora?

Uzalendo ni kuteka, kuua na kupoteza watu wenye kumkosoa?

Hivi kwa tafsiri yako mtu mzalendo ni mtu mwizi na anayeonea watu?
Isha chuja hiyo 1.5T inayo hit sasa ni tozo maji na umeme kukatika kama kiuno cha mmakonde mwenye shanga.
 
Tunaendelea na visa na mikasa ya hayati JPM..

Hakuna siri JPM hakuwa chaguo la wana CCM mwaka 2015, hata mwenyekiti wa chama hakumtaka awe Rais bali alizidiwa na nguvu ya asili.

Mwenyekiti alimkusudia kumrithisha kijiti rafiki yake wa kitambo Bernard Membe,lakini wana CCM walimtaka Edward Lowassa.

Baada ya jina la Magufuli kuibuka kidedea kuna watu hawakulala siku hiyo. Tena sio wapinzani, bali wafanyabiashara na mafisadi ndani ya CCM, walijua kiama chao kimefika.

Mojawapo wa wafanyabiashara hao ni familia ya Bwana Ghalib almaarufu kama GSM.

Tukirudi nyuma kidogo hii familia ina asili ya mkoa wa Tanga na mzee wao marehemu Said Mohamed ambaye alifariki mapema mwaka huu alihamia huko Kusini mwa Tanzania na kujikita na kilimo na biashara ya korosho, alipozeeka akawaachia biashara vijana wake waziendeleze.

Pia hii familia imekuwa na ukaribu na familia ya mstaafu JK kwa miaka mingi.
Tufahamu kuwa JK aliwapenda sana watu wa mkoa wa Tanga kuliko watu wa mkoa wowote uli, labda ni kwa sababu alisoma Tanga School au kwa sababu wilaya anayotokea iko jirani na mkoa wa Tanga sielewi.

Nikikupa hapa orodha ya watu wa mkoa wa Tanga ambao walibebwa na JK kipindi cha utawala wake utashangaa,wengine hakuna aliyekuwa akiwafahamu wakalama post kubwa za ukuu wa mkoa,wilaya hata uwaziri ,achilia mbali post zingine za juu.

Kipindi hiki cha JK ndipo familia hii ya GSM nayo ikaibuka kama uyoga, kupitia kampuni zao za HSC na Silent Ocean wakaigeuza Kariakoo kuwa Dubai ya Afrika au China ya Afrika, wafanyabiashara toka nchi jirani wakawa hawaendi tena China kufuata mzigo mambo yote yaliiishia kariakoo.

Umafia wa kiwango cha juu uliofanyika bandarini na TRA na kampuni hizi ulivutia wateja wengi, mzigo ulikombolewa bandarini fasta na kwa gharama ndogo.

Kumbe nyuma yake kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za bandari na kodi za TRA, mabilioni ya shilingi yalihujumiwa na hii familia.

Baada ya hii jina la JPM kupenya sasa ikawa patashika nguo kuchanika wakawata na kuwazua wakaamua kuiua kampuno ya HSC wakijua tu ikibaki hewani JPM atowaacha salama.

Kupitia kampuni ya Law Domain Adocate tarehe 19 oct 2015 siku chache kabla ya uchaguzi mkuu,wakafile A notice of resolution to wind up voluntarily. Hii kwa wasiojua sheria, wind up ni kusimamisha shughuli za kampuni kisheria.

Walisahau kitu kimoja ila wakaja kukikumbuka baadae kuwa jinai huwa haifi, pamoja na kuwind up HSC kisheria bado wangekamatwa na kujibu tuhuma hata kama kampuni haipo.

Ile Silent Ocean ilibaki kuoparate kwa sababu inasemekana haikusajiliwa Tanzania japo iliwakenga wafanyabiashara wa Tanzania.

Sasa basi baada ya JPM kuingia madarakani, naweza kusema mwezi mzima alikuwa akishinda kama sio bandarini basi ni TRA, mabosi wa taasisi hizo mbili vitambi viliporomoka.

Vijana wake wakamletea ripoti ya wakwepa kodi maarufu,jina la HSC na Silent Ocean likiwa kidedea pale juu.

Matumbo moto wakajua hapa Segerea inawahusu, kama Manji alilala Segerea who is GSM?

Kwa kutumia ushawishi wa vijana wa mstaafu wakaomba apointment mara kadhaa kuonana na JPM.

Appointment ikawa approved wakaitwa Ikulu, kwa makosa yao walitembea kwa magoti kwenye korido mpaka ofisini kwa JPM. Akiwa na sura iliyokasirika akawaambia sitaki maelezo lipeni hizo arreas au Segerea inawasubiri

Yakalipwa mabilioni kimyakimya GSM dhambi zao zikasamehewa.

Plea bargain kwa wasiojua ilianza na hawa mabwana ila yao ilikuwa ya kimya kimya.

Kuanzia siku hiyo JK na JPM wakawa watu wa kutupiana vijembe hadharani kama utani vile kumbe wanajua kinachoendelea, ukitaka kula lazima uliwe.

Ikulu kutamu jamani
Jk ni share holder kwenye gsm, hawa ni majambazi wanaolindwa na dola
 
Back
Top Bottom