Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Mimi ninavyodhani kumpendekeza JPM wakati ule ilikuwa zaidi kutafuta imani ya Wananchi kwa Chama, maana ilishapungua sana wakaona walau huyo Jamaa atarudisha hali kwenye mstari.

Na huenda ilikuwa ni maamuzi ya Mtu au Watu wachache sana na ni baada ya kushauriana sana, bila shaka wapo walioiona hatari ya Jamaa kuwageuka.

Ambacho hawakutarajia Wakubwa hao ni kwamba Jamaa kweli atatoka kwenye mstari....ndio maana kukazuka lile jina "Mshamba". hopefully na kila walipokutana walimtambulisha kama "ona sasa huyu Mshamba.....".

Kuhusu Wafanyabiashara wao kupata matumbo joto kwa JPM kuingia kwenye usukani sidhani, maana utaogopaje kitu kabla ya kukijua? labda useme wasiwasi tu wa kuona huyu kweli ataendelea kutulinda ama?.

Ingekuwa inatokea kwa situation kama ile ya Marehemu Mzee Mrema wakati ule angepata kushika hatamu na kuipiga chini CCM hapo sasa lazima na wa kukimbia nchi wangekimbia...lakini hii ya kukabidhiana kwa amani wengi hutarajia mambo yataenda kama kawa, maana wanaona Kanzu ndio mpya ila Sheikh ni yule yule.

Mimi nadhani kilichowatokea ilikuwa ni suprise kwa kila mmoja ingawa walihisi ingeweza kutokea, kuanzia kwa waliompa kijiti, Wafanya Biashara n.k.
 
Sikiliza nikuambie kitu kijana kutumia jina feki haimaanishi ukose adabu,kwataarifa yako nina elimu ya uhakika kuliko wewe ila hauwezi hata siku moja najisifu mbele za watu kwasababu katika harakati zangu za maisha nimekutana na watu wenye uelewa wa hali ya juu mno ila hawakwenda shule kama mimi, kwahiyo nikajifunza kumbe kwenda shule sio kujua kila kitu
 
Sasa yanakula kujigalagazaaa
 
Huku mwakibuga, Bariadi tuna msamiati,, unaitwa...
IMALASEKO,,, kwa english,, "WHO LAUGHS LAST...
 
akalipwa mabilioni kimyakimya GSM dhambi zao zikasamehewa.
Halafu wakatokea wapuliza filimbi wakisema kuwa JPM anachukua mitaji ya wawekezaji anaua sekta binafsi,kumbe watu walikuwa wanatoa voluntarily baada ya jamaa kuwabana.

Rest EASY JPM
 
Alikuwa mzalendo wa kweli, mola ailaze roho yake mahali pema peponi!
Chukulia ni kweli kilichondikwa, mzalendo gani anakiuka sheria na kutoa maamuzi mwenyewe tena Ikulu? Huoni alifanya makosa makubwa na sasa hivi ndiyo wamerudi upya? Angesema sheria ichukuwe mkondo wake huoni tatizo lingekuwa limeisha? Magufuli tatizo lake, miongoni mwa madhambi mengi ni kuwa alikuwa anaendesha nchi kama familia binafsi. Alikuwa anaamua nani akamatwe, nani asamehewe, nani auawe na nani afungwe. Wazalendo hawako hivyo.
 
Umesema kweli. Magufuli hakuna CCM aliyetarajia atafikia kiwango kile. Ilikuwa ni shock na kitu kama ambush fulani. Kosa lake kubwa ni kutowamalizia kabisa kama unavyoua nyoka kwa kukata kichwa na badala ytake akaona wapinzani ndiyo wakumaliza.
 
Umesema kweli. Magufuli hakuna CCM aliyetarajia atafikia kiwango kile. Ilikuwa ni shock na kitu kama ambush fulani. Kosa lake kubwa ni kutowamalizia kabisa kama unavyoua nyoka kwa kukata kichwa na badala ytake akaona wapinzani ndiyo wakumaliza.
Huwezi kuwamakiza viroboto kwa siku moja,wako wengi sana bandani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…