Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Mimi ninavyodhani kumpendekeza JPM wakati ule ilikuwa zaidi kutafuta imani ya Wananchi kwa Chama, maana ilishapungua sana wakaona walau huyo Jamaa atarudisha hali kwenye mstari.

Na huenda ilikuwa ni maamuzi ya Mtu au Watu wachache sana na ni baada ya kushauriana sana, bila shaka wapo walioiona hatari ya Jamaa kuwageuka.

Ambacho hawakutarajia Wakubwa hao ni kwamba Jamaa kweli atatoka kwenye mstari....ndio maana kukazuka lile jina "Mshamba". hopefully na kila walipokutana walimtambulisha kama "ona sasa huyu Mshamba.....".

Kuhusu Wafanyabiashara wao kupata matumbo joto kwa JPM kuingia kwenye usukani sidhani, maana utaogopaje kitu kabla ya kukijua? labda useme wasiwasi tu wa kuona huyu kweli ataendelea kutulinda ama?.

Ingekuwa inatokea kwa situation kama ile ya Marehemu Mzee Mrema wakati ule angepata kushika hatamu na kuipiga chini CCM hapo sasa lazima na wa kukimbia nchi wangekimbia...lakini hii ya kukabidhiana kwa amani wengi hutarajia mambo yataenda kama kawa, maana wanaona Kanzu ndio mpya ila Sheikh ni yule yule.

Mimi nadhani kilichowatokea ilikuwa ni suprise kwa kila mmoja ingawa walihisi ingeweza kutokea, kuanzia kwa waliompa kijiti, Wafanya Biashara n.k.
 
Ungeenda shule na ungekuwa na uzalendo pia shule yako ingekusaidia ungeelewa.

Ukweli ni kwamba sio Matajiri wanachukiwa... tatizo wengi wenu ni wajinga wajinga sana! Anyways... kama hapa umeshindwa kuelewa hutaelewa tena baki na ujinga wako na wewe jipendekeze kwao
Sikiliza nikuambie kitu kijana kutumia jina feki haimaanishi ukose adabu,kwataarifa yako nina elimu ya uhakika kuliko wewe ila hauwezi hata siku moja najisifu mbele za watu kwasababu katika harakati zangu za maisha nimekutana na watu wenye uelewa wa hali ya juu mno ila hawakwenda shule kama mimi, kwahiyo nikajifunza kumbe kwenda shule sio kujua kila kitu
 
Tunaendelea na visa na mikasa ya hayati JPM..

Hakuna siri JPM hakuwa chaguo la wana CCM mwaka 2015, hata mwenyekiti wa chama hakumtaka awe Rais bali alizidiwa na nguvu ya asili.

Mwenyekiti alimkusudia kumrithisha kijiti rafiki yake wa kitambo Bernard Membe,lakini wana CCM walimtaka Edward Lowassa.

Baada ya jina la Magufuli kuibuka kidedea kuna watu hawakulala siku hiyo. Tena sio wapinzani, bali wafanyabiashara na mafisadi ndani ya CCM, walijua kiama chao kimefika.

Mojawapo wa wafanyabiashara hao ni familia ya Bwana Ghalib almaarufu kama GSM.

Tukirudi nyuma kidogo hii familia ina asili ya mkoa wa Tanga na mzee wao marehemu Said Mohamed ambaye alifariki mapema mwaka huu alihamia huko Kusini mwa Tanzania na kujikita na kilimo na biashara ya korosho, alipozeeka akawaachia biashara vijana wake waziendeleze.

Pia hii familia imekuwa na ukaribu na familia ya mstaafu JK kwa miaka mingi.
Tufahamu kuwa JK aliwapenda sana watu wa mkoa wa Tanga kuliko watu wa mkoa wowote uli, labda ni kwa sababu alisoma Tanga School au kwa sababu wilaya anayotokea iko jirani na mkoa wa Tanga sielewi.

Nikikupa hapa orodha ya watu wa mkoa wa Tanga ambao walibebwa na JK kipindi cha utawala wake utashangaa,wengine hakuna aliyekuwa akiwafahamu wakalama post kubwa za ukuu wa mkoa,wilaya hata uwaziri ,achilia mbali post zingine za juu.

Kipindi hiki cha JK ndipo familia hii ya GSM nayo ikaibuka kama uyoga, kupitia kampuni zao za HSC na Silent Ocean wakaigeuza Kariakoo kuwa Dubai ya Afrika au China ya Afrika, wafanyabiashara toka nchi jirani wakawa hawaendi tena China kufuata mzigo mambo yote yaliiishia kariakoo.

Umafia wa kiwango cha juu uliofanyika bandarini na TRA na kampuni hizi ulivutia wateja wengi, mzigo ulikombolewa bandarini fasta na kwa gharama ndogo.

Kumbe nyuma yake kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za bandari na kodi za TRA, mabilioni ya shilingi yalihujumiwa na hii familia.

Baada ya hii jina la JPM kupenya sasa ikawa patashika nguo kuchanika wakawata na kuwazua wakaamua kuiua kampuno ya HSC wakijua tu ikibaki hewani JPM atowaacha salama.

Kupitia kampuni ya Law Domain Adocate tarehe 19 oct 2015 siku chache kabla ya uchaguzi mkuu,wakafile A notice of resolution to wind up voluntarily. Hii kwa wasiojua sheria, wind up ni kusimamisha shughuli za kampuni kisheria.

Walisahau kitu kimoja ila wakaja kukikumbuka baadae kuwa jinai huwa haifi, pamoja na kuwind up HSC kisheria bado wangekamatwa na kujibu tuhuma hata kama kampuni haipo.

Ile Silent Ocean ilibaki kuoparate kwa sababu inasemekana haikusajiliwa Tanzania japo iliwakenga wafanyabiashara wa Tanzania.

Sasa basi baada ya JPM kuingia madarakani, naweza kusema mwezi mzima alikuwa akishinda kama sio bandarini basi ni TRA, mabosi wa taasisi hizo mbili vitambi viliporomoka.

Vijana wake wakamletea ripoti ya wakwepa kodi maarufu,jina la HSC na Silent Ocean likiwa kidedea pale juu.

Matumbo moto wakajua hapa Segerea inawahusu, kama Manji alilala Segerea who is GSM?

Kwa kutumia ushawishi wa vijana wa mstaafu wakaomba apointment mara kadhaa kuonana na JPM.

Appointment ikawa approved wakaitwa Ikulu, kwa makosa yao walitembea kwa magoti kwenye korido mpaka ofisini kwa JPM. Akiwa na sura iliyokasirika akawaambia sitaki maelezo lipeni hizo arreas au Segerea inawasubiri

Yakalipwa mabilioni kimyakimya GSM dhambi zao zikasamehewa.

Plea bargain kwa wasiojua ilianza na hawa mabwana ila yao ilikuwa ya kimya kimya.

Kuanzia siku hiyo JK na JPM wakawa watu wa kutupiana vijembe hadharani kama utani vile kumbe wanajua kinachoendelea, ukitaka kula lazima uliwe.

Ikulu kutamu jamani
Sasa yanakula kujigalagazaaa
 
Huku mwakibuga, Bariadi tuna msamiati,, unaitwa...
IMALASEKO,,, kwa english,, "WHO LAUGHS LAST...
 
akalipwa mabilioni kimyakimya GSM dhambi zao zikasamehewa.
Halafu wakatokea wapuliza filimbi wakisema kuwa JPM anachukua mitaji ya wawekezaji anaua sekta binafsi,kumbe watu walikuwa wanatoa voluntarily baada ya jamaa kuwabana.

Rest EASY JPM
 
Alikuwa mzalendo wa kweli, mola ailaze roho yake mahali pema peponi!
Chukulia ni kweli kilichondikwa, mzalendo gani anakiuka sheria na kutoa maamuzi mwenyewe tena Ikulu? Huoni alifanya makosa makubwa na sasa hivi ndiyo wamerudi upya? Angesema sheria ichukuwe mkondo wake huoni tatizo lingekuwa limeisha? Magufuli tatizo lake, miongoni mwa madhambi mengi ni kuwa alikuwa anaendesha nchi kama familia binafsi. Alikuwa anaamua nani akamatwe, nani asamehewe, nani auawe na nani afungwe. Wazalendo hawako hivyo.
 
Mimi ninavyodhani kumpendekeza JPM wakati ule ilikuwa zaidi kutafuta imani ya Wananchi kwa Chama, maana ilishapungua sana wakaona walau huyo Jamaa atarudisha hali kwenye mstari.

Na huenda ilikuwa ni maamuzi ya Mtu au Watu wachache sana na ni baada ya kushauriana sana, bila shaka wapo walioiona hatari ya Jamaa kuwageuka.

Ambacho hawakutarajia Wakubwa hao ni kwamba Jamaa kweli atatoka kwenye mstari....ndio maana kukazuka lile jina "Mshamba". hopefully na kila walipokutana wlimtambulisha kama "Mshamba".

Kuhusu Wafanyabiashara wao kupata matumbo joto kwa JPM kuingia kwenye usukani sidhani, maana utaogopaje kitu kabla ya kukijua? labda useme wasiwasi tu wa kuona huyu ataendelea kutulinda ama?.

Ingekuwa inatokea kwa situation kama ile ya Marehemu Mzee Mrema wakati ule angepata kushika hatamu na kuipiga chini CCM hapo sasa lazima wa kukimbia nchi wangekimbia...lakini hii ya kukabidhiana kwa amani wengi hutarajia mambo yataenda kama kawa, maana wanaona Kanzu ndio mpya ila Sheikh ni yule yule.

Mimi nadhani kilichowatokea ilikuwa ni suprise kwa kila mmoja, kuanzia kwa waliompa kijiti, Wafanya Biashara n.k.
Umesema kweli. Magufuli hakuna CCM aliyetarajia atafikia kiwango kile. Ilikuwa ni shock na kitu kama ambush fulani. Kosa lake kubwa ni kutowamalizia kabisa kama unavyoua nyoka kwa kukata kichwa na badala ytake akaona wapinzani ndiyo wakumaliza.
 
Umesema kweli. Magufuli hakuna CCM aliyetarajia atafikia kiwango kile. Ilikuwa ni shock na kitu kama ambush fulani. Kosa lake kubwa ni kutowamalizia kabisa kama unavyoua nyoka kwa kukata kichwa na badala ytake akaona wapinzani ndiyo wakumaliza.
Huwezi kuwamakiza viroboto kwa siku moja,wako wengi sana bandani
 
Back
Top Bottom