Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Huwezi kuwamakiza viroboto kwa siku moja,wako wengi sana bandani
Ukifukazana na mmoja mmoja hawataisha. Alichotakiwa kufanya ni kuufumua mfumo wa uongozi wa nchi na 2020 tuwe tumeanza na mfumo mpya. Viroboto wangekufa kifo kwa kukosa mazalio.
 
Ukifukazana na mmoja mmoja hawataisha. Alichotakiwa kufanya ni kuufumua mfumo wa uongozi wa nchi na 2020 tuwe tumeanza na mfumo mpya. Viroboto wangekufa kifo kwa kukosa mazalio.
Sio rahisi kihivyo maana ni process ya miaka mingi,kabla hujatimiza azma wanakuwahi wewe labda uwe mafia kwelikweli kama Kagame au Putin
 
Sio rahisi kihivyo maana ni process ya miaka mingi,kabla hujatimiza azma wanakuwahi wewe labda uwe mafia kwelikweli kama Kagame au Putin
Kabisa. Ni process ndefu ndiyo maana nimesema alitakiwa aanze mapema kwa kuufumua mfumo. Rais huwezi kufanya haya kwa awamu moja ila ukifanya vizuri wakati wa awamu yako unakuwa umeweka msingi imara kwa awamu inayofuata.
 
Sasa wamerudi upyaaaaaa!
Na Yanga juu, ukiona raisi au kiongozi mkuu ana urafiki mkubwa na wafanyabiashara jua huku nyuma kuna kitu, namkubuka baba wa taifa alisema Ikulu isigeuzwe pango la Wafanyabiashara enzi za mzee rukhsa wafanyabiashara hasa hawa wasio wamatumbi walikuwa wanaenda kumsalimia mzee na vifuko vya sandarusi, duniani kote wafanyabiashara wakubwa na wadogo, magenge ya maharamia wanataka kuwa karibu na viongozi wakuu ili wafanye mambo wanvyotaka, si tunawakumbuka akina Zuma, ndio shida ya hizi banana republic ,waacha niishie hapa nisijesekwa ndani kwa kudai naichonganisha serikali na wananchi, wakubwa hawataki na hawapendi kuambiwa ukweli wa madudu wanayoyafanya. Tutamkumbuka sana JPM
 
I doubt kama kuna ukweli wowote katika hili....

1. Ambao walikumbana na mkono wa JPM ama hawakuinuka tena au wali-struggle sana kuinuka!

Kinyume chake, GSM hawakutetereka kabisa... na hata kama watu mnajisahaulisha, GSM waling'ara zaidi kipindi cha JPM pengine kuliko hata wakati wa JK!

Minoti ya GSM ikaanza kuonekana wazi wazi hadharani kipindi cha JPM pale walipoanza kujihusisha moja kwa moja na Yanga!!

2. Ukimhusisha GSM na JK hapo ndo unavuruga kila kitu!!

Pamoja na mambo yake yote, JPM aliwakumbatia sana Vigogo wa CCM na Watendaji Wakuu wa Serikali.

Ni kutokana na ukweli huo, ndo maana hadi siku Mwenyezi Mungu anamchukua, JPM hakuwahi kumgusa any high profile CCM Politician and Top Govt Executive!

JPM alisimamisha miradi mingi ya ujenzi kama sio yote ya NSSF kwa madai kwamba kuna ufisadi mkubwa!

Kama kuna ufisadi mkubwa, vipi kuhusu wahusika wa huo ufisadi?! DG wa NSSF akampa Ubalozi Malaysia!!!

Hata hasimu wake mkuu Bernard Membe, aliishia tu kuongea kwa mafumbo kwamba "...kule Lindi watu wametafuna Sh 20B" lakini hakumtaja hata kwa jina!

And guess what... mwaka jana nilienda nyumbani kwao Membe! Kwa hali niliyoikuta pale, kuna kila dalili kwamba Magu aliongea ukweli kuhusu "watu kutafuna 20B kule Lindi"!

Je, alimfanya nini?!

Sasa ikiwa hata Membe hakumfanya kitu zaidi ya kumwadhibu kisiasa, ndo aguse maslahi ya JK?! Au hizi habari za JK na GSM hazina ukweli wowote?

3. Hivi mlilifuatilia vizuri Sakata la Makinikia? Wakati mambo yapo HOT, watu wakanza kumhusisha JK na mikataba ya madini wakati akiwa waziri Wizara ya Nishati na Madini!

Katika kutekeleza "mahaba" ya JPM kwa Wastaafu kwamba waachwe wapumzike, Ripoti ya 2 ya Makinikia (Ripoti ya Profesa Oroso) ikaja na hili:-


Kwa wasiofahamu, huyo Waziri anayetajwa kwenye Ripoti ya Makinikia 2 kwamba "alipambana kwa jasho na damu kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa" ni Jakaya Kikwete!

Ukiisoma ripoti ile, utaona mikataba YOTE ya madini ambayo ilisainiwa tangu enzi za Mwinyi ilikuwa na kasoro EXCEPT, mikataba iliyosainiwa na JK!!

Na kule bungeni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu akapiga marufuku mijadala ya kibunge iliyokuwa inataka wastaafu wahojiwe!

Magu alimaanisha alipokuwa anasema waacheni wazee wapumzike!

Hakutaka kabisa kuwagusa Vingunge wa CCM! Ni kutokana na ukweli ndo maana napata shaka sana kuamini haya unless kama HAKUNA UKWELI wowote kuhusu JK kuhusika na GSM!

4. JK pamoja na tuhuma zake nyingi lakini mwishowe akaona Rostam Azizi na Swahibu ake Lowassa ni liability!!

Baada ya JK kuasisi "Kujivua Gamba", RA akasusa siasa za Bongo na akapotea kabisa kwenye mainstream politics!

Hivi nchi hii kuna mtu alikuwa na tuhuma nyingi kumzidi RA?!

Je, RA alifanywa nini zaidi ya kuanza tena kujipenyeza serikalini kipindi cha JPM?! Au pia tukumbushane kwamba ni JPM ndie--



Narudia, JPM aliwalinda sana Vigogo wa CCM, na kama mnaamini GSM ni mkono wa kuume wa JK, basi JPM asingewagusa!

5. Watu mnadanganyana kwamba JK hakumtaka JPM bali alimtaka swahibu ake Membe!

Ukweli ni kwamba, ni janja janja ya Membe ndiyo iliwafanya watu waamini yeye ndo chaguo la JK! Membe ni mpole lakini ni mjanja sana! Kama umepata kukaa pamoja na Membe na kuongea nae utalifahamu hili!

Binafsi, nimewahi kukaa na Membe face to face, tena at a comfort zone, living room kwake! The guy is CLEVER!

Ni ujanja ujanja wake huu akafikia hadi kuaminisha watu kwamba yeye ndo Chaguo #1 la Mr. President! Watu wakafikia hadi kusema eti Membe na JK ni ndugu wa damu wakati hakuna ukweli wowote!!

Na wengi mnaaminishana ni Mkapa ndie ka-influence JPM kuwa Rais kinyume na matakwa ya sitting president!

Hapa nawakumbusha tu kwamba kutokana na mifumo mibovu, nchi hii Rais ndo kila kitu! Kama Jk angemtaka Membe basi hakuna ambae angemzuia!

Rais: Yeye ndo Mwenyekiti wa Chama Tawala! Yeye ndo Amiri Jeshi Mkuu, yeye ndo Mwenyekiti wa Baraza la Usalama, yeye ndo "Jaji Mkuu", yeye ndo "Askofu Mkuu", yeye ndo "Mufti na Kadhi" etc etc etc!

Atakacho, HAKUNA WA KUMZUIA!

Mambo nyeti yanajadiliwa kwenye National Security Council ambayo, unless Sheria ya 2010 iwe imebadilishwa, Rais Mstaafu sio Mjumbe wa NSC ingawaje anaweza kuwepo kwenye kikao kwa MWALIKO!

Sasa huyo Rais Mstaafu influence ya kuweka rais amtakaye yeye ataitoa wapi?!

Kikao pekee nyeti ambacho Rais Mstaafu ni mjumbe ni Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM! Hiki ndicho kikao ambacho, kinadharia, ndicho kinafanya mchujo!

Nasema kinadharia kwa sababu, practically, sitting president anaenda kwenye hicho kikao akiwa tayari na watu wake.

Anaenda pale kutetea tu wale alioona wanastahili kuingia kwenye Top 5!

Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 Mark Mwandosya aliwahi kulalamika kwamba "Mwenyekiti alikuwa anatembea na majina yake mfukoni"!

He's damn right!

JK alifika kwenye Kamati ya Maadili na Usalama akiwa na majina yake 5 huku EL na wenzake wakiwa wamekatwa juu kwa juu, na sio kwamba walikatwa na Kamati...

...kamati ili-rubber stamp tu maamuzi ya rais!

JK alivyo mjanja, akampeleka Membe Top 5 huku akiwa amemchinja EL! Unadhani JK ni stupid na hakufahamu kwamba hasira za Watu wa Lowassa zingekuwa ni kutompa kura Membe?!

Anyway, Rais Mstaafu pekee ambae alikuwa na ubavu wa ku-influence maamuzi ya sitting president ni Nyerere ambae alimtaka Mkapa awe Rais, na akawa!

But look... huyo huyo Nyerere baada ya kumpa urais Mkapa, baada ya hapo akashindwa kumdhibiti coz' Rais ndo kila kitu!

Siku NBC inaingizwa mnadani Nyerere alibaki kunung'unika tu lakini hakuwa na ubavu wa kumzuia Mkapa!!

So, always JPM alifahamu kama JK asingetaka, basi hata yeye huo Urais asingeupata! Na ni kutokana na hilo, ndo maana mara zote JPM alikuwa anasisitiza "waacheni wazee wapumzike"!

Hapo aliyekuwa analengwa aachwe apummzike ni JK kwa sababu ndie alikuwa anaandamwa sana!

Sema ndo vile tu, zikifika siku za mwezi mchanga, unakuta JPM huyo huyo anapiga vijembe wazee!

JPM aliendelea kuwabeba hata watu wa JK. Mchukulie Said Mtanda kwa mfano! Yule alikuwa hafahamiki kabisa kwenye system.

Lakini kwavile babake Said Mtanda alistaafia B'moyo na kuishi jirani na familia ya JK, bond kati ya JK and Mtanda Family ikaanza hapo!

Said Mtanda na Rizimoko na wenyewe wamekua pamoja!

So, kwavile Said Mtanda hakuwa na issue ya maana mjini, Membe na JK wakampeleka Mchinga kugombea ubunge in 2010 lakini 2015 akatoswa na Wananchi!

JPM hadi anaingia kaburini hakumtupa Said Mtanda! "Mtu wa JK" ambae alimpiga chini ni yule ambae alikuwa DC wa Geita enzi za JK!

Huyu alipigwa chini na Magu kwa sababu basically, hakuwa mtu wa JK bali alikuwa mtu wa Membe!!

Hivi tukumbushane kwamba hata Salma alipewa ubunge kwa heshima ya Mstaafu!!
 
Aliyeenda shule hachangiagi udedere kama wewe bogus! Walioenda shule maoni na michango yao inaonekana tu na hata kwa kusoma na kuchambua kwa haraka haraka utajua ni mtu wa aina gani... we bogus!
 
Na ndo uongozi wa Dictatorship unataka hivyo... tulipofikia tunataka dictatorship mambo yaende sio usengeusenge tu
 
Sasa mbonq singer hakufungwa na Rugemalila?,, Tatizo wabongo mna mentality za kijamaa,, kila tajiri mnamuona bepari,, huu ujinga na majungu dhidi ya watu matajiri huwezi kuuona katika nchi zilizostaarabika kama kenya😂.
Nchi zinafight kutengeza mabilionea ili watoe ajira, kwa bongo matajiri ni wahaini,, huu ni ufala
 
JPM alikua komesha. Mungu amlaze pema
 
Aliyeenda shule hachangiagi udedere kama wewe bogus! Walioenda shule maoni na michango yao inaonekana tu na hata kwa kusoma na kuchambua kwa haraka haraka utajua ni mtu wa aina gani... we bogus!
Waswahili kwakweli mna kazi sana nikwamba wewe haunizidi chechote kile maishani kuanzia pesa,elimu na mafanikio kiujumla.........mitandaoni kuna mambo sana eti nawewe una elimu ya hgk ambayo unakaa unajisifia tena kwa mtu ambaye usikute ni umri wa baba yako
 
Na ndo uongozi wa Dictatorship unataka hivyo... tulipofikia tunataka dictatorship mambo yaende sio usengeusenge tu
Umaskini unakusumbua sana na pia kutokana tangu jana upo period basi unachangia kwahasira mno hebu nikuambie kitu kimoja hamna uzalendo unaofundishwa darasani ila uzalendo unaanzia moyoni bila kujali dini,kabila wala elimu.....ewe mwanamke wa kisukuma fikiria kauli ya mumeo magufuli alipokiwaambia watu kuwa jimbo fulani sileti maendeleo kwasababu mumemchagua mbunge wa upinzani je hii ni sawa? Fikiria wale waliokavunjiwa nyumba dar halafu na mwanza nao wakaachiwa kwa kauli kuwa walimchagua je kwako ni sawa hata kama magufuli alikuwa mumeo?
 
Hadithi bila picha hainogi. Hebu weka picha tuone jinsi GSM alivyotembea kwa magoti ikulu.
 
Lengo sio kufa kwa ajiili ya nchi yako
Bali kuua kwa ajiili ya nchi yako

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…