Can you prove???au ndio zile propagandq za cdm ,muacheni mzee baba apumzike alikuwa mzalendo wa kweli kazi yake imeonekana sio hao walamba asali
Sent using
Jamii Forums mobile app
Propaganda gani wakati ni vitu dhahiri. Wakati wa utawala wake hakuna watu aliobambikia kesi? Hakuna watu waliokuwa wakitekwa baada ya kumkosoa? Hakuna watu waliokuwa wanapotezwa, na wengine kuteswa baada ya kuhoji matendo yake? Report ya CAG haikusema kuwa 1.5 trilion hazikuonekana mahali popote kwenye matumizi wakati zilikuwa zimechotwa hazina, na yeye akawa mkali na kumtishia CAG, baadaye kumwonfoa kwa kukiuka katiba?
Ni mambo gani makubwa aliyoyafanya kwenye uchumi?
Kudondosha thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo kwa 50%, ndiyo unasema mambo makubwa aliyoyafanya ya kuonekana?
Kuporomosha ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4% ndiyo mambo makubwa unayosema aliyafanya ya kuonekana?
Au ni kule kufifisha ukuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%?
Au makubwa unayoongelea ni yale yaliyothibitishwa na CAG aliyeteuliwa na yeye mwenyewe, kuwa aliiba pesa yote waliyolipa aliobambikia kesi za uhujumu uchumi?
Hakika mema aliyoyafanya ni machache sana ukilinganisha na uharibifu alioufanya.
Unadhani Mwalimu Nyerere, Mkapa, Mwinyi na Kikwete hawakufanya makosa wakati wa utawala wao? Sidhani, lakini makosa yao ni machache sana ukilinganisha na mazuri yao. Mathalani, Mwalimu Nyerere, sijui utakuwa mtu wa namna gani kama utasimama hadharani na kumnenea vibaya. Yeye alikuwa mzalendo hasa, na maisha yake yote yalipambwa na uzalendo wa kweli, siyo uzalendo magumashi kama wa huyu mwenzetu wa karibuni. Huwezi kuwa mzalendo halafu unaiba hela ya Taifa au unaua watu wanaokemea maovu yako, au unawabambikia kesi wenzako ili watoe pesa yao uipore wewe. Mtu wa namna hiyo ana tofauti gani na jambazi anayekuja amekushikia bunduki halafu anakuambia, nipe pesa?
Wakati wa uhai wake isingewezekana kuunena uovu wake na bado ukaendelea kuwa hai. Kwa sababu aliwazuia watu kuunena uovu wake akiwa hai, atasemwa sana wakati akiwa hayupo nasi ili pia wale waovu wenzake ambao bado tunao hadi leo, wanaotetea maovu yake wapate la kujifunza.