Familia ya Hans Poppe kutinga kwa Rais Samia kudai mabilioni ya baba yao yaliyoporwa na Hayati Magufuli kwenye ‘plea bargain’

Pia ni vzr pesa zote za Plea bargaining zijulikane zipo account gan na kiasi gan, achilia mbali walinda legacy watalalamikia utawala huu ama la! Pia walinda legacy warudie kauli yao ileeeee... Msema kweli ni mpez wa.........
 
Kila shetani na mbuyu wake .
Pope kwa hapo alionewa ila naye ana madhambi yake mengi .

Tujikumbushe mtafaruku wake na boss wa keko juu ya kuficha sukari na mwisho mzee wa watu akaishia kupigwa risasi .

Dunia ya wananzengo wa keko ikasimama Pope akahudumia msiba mwanzo mwisho kwa vyakula na safari mpaka Moshi kumuhifadhi mtesi wake .

Waswahili na wahuni wa keko wakanywea naye akapita kimya kimya kama hakuna lililotokea .

Dereva wa boss wa Keko akaeleza A--Z uvamizi mpaka risasi kupigwa kwa boss wake na wahusika akawataja kuwa aliwaona na Pope akiwepo .

Dereva yule mhaya wa watu akachimbwa mkwara mnene akaona cha kufia nini ?

Akaondoka zake Dar es salaam sasa ni dereva Halmashauri moja huko Lindi anausukuma uzee kwa sasa .

Keep in resting easy Pope the real hustler japo ulipita kushoto sana japo sio kote ila baadhi ya sehemu [emoji24]
 
Pia ni vzr pesa zote za Plea bargaining zijulikane zipo account gan na kiasi gan, achilia mbali walinda legacy watalalamikia utawala huu ama la! Pia walinda legacy warudie kauli yao ileeeee... Msema kweli ni mpez wa.........
CCM wote wezi tu, Kwaiyo unafikiri yeye Mama siyo mwizi,izo pesa ata zikipatikana watagawana wakubwa.
 
CCM wote wezi tu, Kwaiyo unafikiri yeye Mama siyo mwizi,izo pesa ata zikipatikana watagawana wakubwa.
Punguza kasiriko mlinda legacy! Kikubwa ijulikane pesa ipo account gan na kiasi gan cha pesa, hayo mengine unayolialia hayaondoi ukwel!! Hii inatakiwa idhihirishe kua hakujawa kua na uzalendo awamu ile kama walivyojinasibu!!!
 
Mtaangaika kumchafua JPM ila bado mtashindwa,jamaa keshakufa ila bado mnaleta visa na chokochoko kila siku ila bado mnashindwa,Huyu jamaa angekuwepo heshima ingekuwepo.
MAREHEMU ANASHINDANA NA WALIO HAI NA BADO ANAWABULUZA TU.
 
Poppe alikuwa mafia sana yule
 
Fedha zake kivipi? Fedha za kifisadi kwa kuwaona watanzania mambumbumbu ndio zake? Aliitwa aeleze alikozitoa aliweza? Nyie mafisadi kiboko yenu alikua mchato tu, pesa iliyochumwa kikanjanja lazima itapikwe, ngoja kije chuma kingine pale ikulu muendelee kupelekewa moto
 
Asante Mungu kwa kutuongezea jizi katili kutoka Chato
 
Wenye nchi wanajuta hawatapitisha tena mtu mwenye kariba ya hayati kuwania nafasi za juu katika nchi hii
 
Kuna Dereva wake ( wa Familia ya Marehemu Hanspoppe ) Mmoja 'Mpenda Mbunye' Kawe aliniambia kuwa Boss wake Hanspoppe ameacha Pesa za Kula Wake zake Lukuki, Watoto na Wajukuu zake kwa miaka 100 ijayo.

Hivyo nimeshangaa leo kusikia kuwa Familia yake inapanga Kudai tena Pesa Serikalini wakati alishasamehewa na Hayati Dk. Magufuli ( kwakuwa tu alikuwa ni Mwana Simba SC Mwenzake ) Kesi yake Kubwa ya Uhujumu Uchumi kwa Kuingiza nchini Meli yenye Shehena ya Sukari Mbovu ( Feki )
 
Hawa hawawezi kupata fedha hizo kwa vile Baba aliyekufa ndiyo anazo facts za kuestablish kiasi alichotoa. Watoto kila watakachodai itakuwa ni rumours tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…