Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe Harry ni mtoto wa marehemu Diana.Unajua harry anaishi kama mama yake. Yani tofauti kabisa na inasemekana jamaa yupo tofauti kabisa na kaka ake . Yani anapenda uhuru sana. Mbaya zaidi kadata kwa light skin woman wa kimarekani. Alaf wamerekan ni watu wa kujiachia sana leo miami kesho LA, keshokutwa paris mala Maldives island ..sasa ajichimbie uingereza kuna nini...
Pia ishu ya rangi somehow inachangia kwa Meghan...though she is half white half black Ila still English people consider her kama black [emoji23][emoji23][emoji23]...
Pia fununu zinasema dogo ana hasira mama yake aliuwawa na MI6 kule Paris kwenye ile ajali ya gari ...
Ila all in all harry kafa kaoza kwa light skin wetu
Hizo story za kuzikwa ulizo nazo ni za kwenye kashata na gahawa kijiweni kwa mandevu.... na hamna kitu kama hicho.Kumbe Harry ni mtoto wa marehemu Diana.
Ahhh mama yake alizikwa eneo makaburi wanakozikwa mbwa wa wafalme na Malkia wa uingereza
Jinga la Kwanza lishajitokezaFalme na mamlaka zoote hapa duniani zitaanguka na kusimama ufalme mmoja tu! "Yesu Kristo"
YaliyompatA Mama mkwe yaweza mpata mkwe any3timeView attachment 1324167
Malkia Elizabeth II ambaye alizaliwa Aprili 21, 1926 anatajwa kuwa mtawala aliyetawala kwa muda mrefu tangu alipochukua nafasi hiyo Februari 9, 1952 kutoka kwa baba yake Mfalme George VI.
Malkia Elizabeth II ndiye kiongozi wa pili kwa umri mkubwa katika viongozi ambao wapo madarakani hivi sasa akiwa na miaka 93 baada ya Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir Mohamed mwenye miaka 94.
Mfalme George VI alizaliwa mwaka 1895 na alifariki dunia 1952 na alimwachia kiti hicho mwanaye Malkia Elizabeth II ambaye aliyeolewa mwaka 1947 mwanamfalme Philip ambapo walipata watoto wawili kabla ya kuwa malkia na wengine wawili baada ya kuwa malkia 1952.
Kati ya watoto wanne aliowazaa mmoja wao ni mwanamfalme Charles ambaye pamoja na mke wake Diana Spencer walipata watoto wawili mwanamfalme William aliyezaliwa mwaka 1982 na Harry aliyezaliwa mwaka 1984 kabla ya kutalikiana naye 1996 na mwaka 2005 alimuoa Camilla Bowles.
Uingereza inaundwa na mataifa ya England, Scotland, Wales na Island ya Kaskazini. Taifa hilo ni la ufalme wa kikatiba linalofuata mfumo wa utawala wa bunge.
Katika kurithi nafasi ya Malkia Elizabeth II hadi sasa kuna orodha ya watu saba wanaotarajiwa ambao ni mwanamfalme Charles akifuatiwa na mwanaye mwanamfalme William na watoto wake watatu ambao ni mwanamfalme, George, bintimfalme, Charlotte na mwanamfalme Louis.
Baada ya hao anayefuatia katika orodha ni mwanamfalme Harry ambaye amegonga vichwa mbalimbali kwa kujiondoa kwenye kazi za kifalme.
Mwanamfalme Harry sio jina geni kwa sababu ya yale yanayoendelea kwenye kasri la Buckingham tangu alipofunga ndoa na mke wake Meghan mwaka 2018.
Harry ambaye amehudumu nafasi mbalimbali Uingereza ikiwemo jeshini na kushiriki vita mara mbili nchini Afghanistan na kuwa mwanamfalme wa kwanza katika familia ya utajiri kwenda vitani ardhini baada ya mjomba wake mwanamfalme Andrew aliyetumiwa helikopta kwenye vita ya Falklands.
Wachambuzi wanadai kuwa mwanamfalme Harry kutokana na kutoona uelekeo wa kuchukua nafasi ya ufalme alifikia maamuzi ya kuachana na familia ya kifalme na kubaki kama watu wa kawaida ila wakiendelea kutoa mchango wao kwa familia hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, familia ya kifalme imeeleza kusikitishwa na maamuzi, ikisema ni kama ndoto huku ikihoji itakuwaje kuhusu suala la ulinzi wao.
Wanandoa hao wamesema sasa wanapanga kutumia muda wao mwingi Amerika ya Kaskazini na kujitegemea kifedha.
Taarifa ya Jumba la Kifalme Buckingham, imeeleza kuwa Harry na Meghan wataendelea kumuunga mkono kikamilifu Malkia Elizabeth II.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya makao makuu ya Malkia mazungumzo yanaendelea kati ya Prince Harry na mkewe kuhusu mipango hiyo.
Familia ya kifalme imesema inaelewa kuhusu nia yao, lakini masuala hayo kwa sasa ni magumu na itachukua muda kuyafanyia kazi.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), lilibainisha kuwa si Malkia wala mwanamfalme William au waandamizi wengine katika falme walijulishwa kuhusu hatua hiyo na kwamba uongozi wa juu wa ufalme umepata pigo.
Kasri ya kifalme limesema suala hilo imelipokea kwa mshtuko mkubwa.
Katika maelezo yao, Harry na Meghan walisema walifikiria uamuzi huo kwa muda mrefu na kufanya maamuzi hayo miezi mingi iliyopita.
Wanandoa hao wamepanga kugawa muda wao kwa nusu kuishi Marekani na nusu Uingereza, kuendelea kumtumikia Malkia na kujihusisha na shughuli za kifalme.
Msemaji wa zamani wa Malkia aitwaye Dickie Arbiter alisema kuwa hafahamu ni namna gani wataweza kugeuza mipango yao.
"Hii ni kama ndoto. Kuna suala la usalama, nani atatoa ulinzi kwao?
"Je, ni nchi gani itawapa ulinzi wa kifalme? Je, ni Canada au? Na nani atagharamia?"
Oktoba mwaka jana Harry na mkewe walilalamika kuingiliwa maisha yao kwa kufuatwa na vyombo vya habari kwa kivuli cha kutoka katika familia ya kifalme.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Harry na mkewe wametoa utetezi wao kuhusu tangazo lao kwamba, wameifikia hatua hiyo baada ya kuwa na majadiliano ya ndani ya nyumba yao wao wawili kwa miezi kadhaa.
Hata hivyo, maamuzi yao yamepingwa kwa kudaiwa kuwa walistahili kupewa idhini ya jambo hilo na kutoa taarifa kabla.
Malengo yao mengine ya kujiondoa katika shughuli za moja kwa moja za kifalme ni kutaka kufanya kazi za kawaida katika kuendesha maisha yao ya kila siku badala ya kutegemea mapato yatokanayo na nafasi zao za kifalme.
Chanzo: Mwananchi
Dogo kaona hana nafasi ya kuwa mfalme hivyo kabinti ka kimarekani kamemchochea! Maana ukiangalia ile lineage ya ufalme yuko nje kabisa! Sasa hivi anayefuata ni baba yao Prince Charles, anafuta Prince Bill, anafuata Prince George na wadogo zake! Anapigwa gap mpaka na kale kabinti ka Prince Bill, Charlotte! Hivyo atembee tu!Dogo kaingiwa Mtima nyongo kitambo tu na Familia ya kifalme,Kuna matukio makubwa tu sema yanafichwa,Ukiacha kuwa wao ndiyo Wamemuua bi Mkubwa wake,Nani kama Mama?Dogo kawapa Shit.
Aliyekwambia Queen ni head of government uingereza ni nani?Ufalme una tofauti gani na udikteta, nchi ipo mikononi mwa koo fulani, mwendo wa kurithishana.
Ha ha ha nimecheka kwa sauti kubwaHizo story za kuzikwa ulizo nazo ni za kwenye kashata na gahawa kijiweni kwa mandevu.... na hamna kitu kama hicho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Prince Bill* prince WilliamDogo kaona hana nafasi ya kuwa mfalme hivyo kabinti ka kimarekani kamemchochea! Maana ukiangalia ile lineage ya ufalme yuko nje kabisa! Sasa hivi anayefuata ni baba yao Prince Charles, anafuta Prince Bill, anafuata Prince George na wadogo zake! Anapigwa gap mpaka na kale kabinti ka Prince Bill, Charlotte! Hivyo atembee tu!
Hamna aliyeniambia ni vipi hicho kiti kikaliwe na koo moja tu?Aliyekwambia Queen ni head of government uingereza ni nani?
Wasabato mtupishe kwanzaFalme na mamlaka zoote hapa duniani zitaanguka na kusimama ufalme mmoja tu! "Yesu Kristo"
Queen wa uingereza haongozi serikali....yeye yupo kiutamaduni zaidi... Na waingereza wanarespect culture yao...Tangu kuanza kwa taifa la uingereza mambo yapo hivyo ni kwa familia teule tu.... And to avoid the so called dictatorship, the queen or king is the head of state and not the government... Hivyo hakuna dictatorship yoyote hapo.Hamna aliyeniambia ni vipi hicho kiti kikaliwe na koo moja tu?
Haha wewe ndiye Diana Spencer mwenyewe
Yaani eti wanalazimishwa mpaka kutabasamu, maisha gani hayo ?Uhuru mzuri sana! Ukiupoteza ndio utaona uthamani wake.
Ndiyo ufupisho wa jina lake, hiyo inatumiwa sana na Wamarekani!