tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe halafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!
Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.
Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.
Nawaunga mkono 100% lakini familia inapaswa iwe makini isije ikawa huyo daktari alitumwa na Musiba ili kuwapotezea focus wasimfilisi. Kwanza wamuulize ni nani kamtuma kuudanganya umma kuhusu kifo cha Membe. Kama atasema alitumwa na Musiba, haraka waachane naye wamshughulikie Musiba kwanza. Kesi zikiwa nyingi zitawatoa kwenye reli ya kumfilisi Musiba.