Familia ya Membe yamkana aliyejiita daktari wake, yaapa kumpeleka mahakamani

Familia ya Membe yamkana aliyejiita daktari wake, yaapa kumpeleka mahakamani

Hii Familia wanapenda kesi kesi sana aisee,hivi huwa hawawezi kupotezea mambi km haya?.Baba yao alifanya hivyo hivyo kwa Cyprian Musiba,na wao leo tena wanarudia kufanya kitu kilekile.
 
Sijui huwa unafanya makusudi au ni kweli una upeo Mdogo?

Ugonjwa wa mtu ni siri yake na daktari na akifa ni swala la familia.

Mbona wanaokufa kwa ukimwi hamtangazi?
Kwahiyo ugonjwa wa Membe aliovujisha huyo daktari ni upi? Maana hospitali ya Kairuki ndio ilitangaza amefariki kwa kifua, kwanini wasishtaki hospitali?
 
Mkuu unaelewa kwamba madaktari wanakatazwa kutoa taarifa za mgonjwa bila ya idhini ya mgonjwa au mtu wa familia ya mgonjwa mwenye medical power of attorney?
Kwahiyo taarifa za ugonjwa alizotoa huyo daktari ni zipi? Maana hospitali ndio ilitangaza kwamba amefariki kwa kifua, mbona hawajashtaki hospitali kama hoja ni hiyo?
 
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!

Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.

Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.

Familia inataka tena vita na wasiojulikana?
 
Kwahiyo taarifa za ugonjwa alizotoa huyo daktari ni zipi? Maana hospitali ndio ilitangaza kwamba amefariki kwa kifua, mbona hawajashtaki hospitali kama hoja ni hiyo?
Kushtaki au kutoshtaki ni uamuzi wao, hoja ni kwamba hospitali na daktari wamevunja maadili ya kitabibu ya kuvunja faragha za mgonjwa kinyume na matakwa ya familia.

Familia hata isiposhitaki, hilo halibadiliki.

Ni kama familia ikiibiwa na kulalamika kuwa imeibiwa, ikilalamika tu bila kushtaki, kulalamika huko hakuondoi ukweli kwamba wameibiwa.
 
Kwahiyo taarifa za ugonjwa alizotoa huyo daktari ni zipi? Maana hospitali ndio ilitangaza kwamba amefariki kwa kifua, mbona hawajashtaki hospitali kama hoja ni hiyo?
Aliyeongea na tulimsikia alisema yeye ni daktari wa familia hakusem yeye ni hospitali
 
Sema familia wamwachie Mungu tu ila kwa kuwa hiyo familia inapenda kesi wataendelea nae huyo Dr kuongezea Billioni za Musiba inaonekana ni chache...
 
Alionekana ni mtu hakuwa hata na umakini wowote wakati anaongea.

Lugha ya mwili au tuseme mwili wa msemaji ulikuwa very relax as if nothing happened.

Even the doctor ar that hospital where he died yaani aliongea tu hivyo.

Kweli msiba huwa una wenyewe
Huyu Daktari alijitambulisha kuwa anatoka taasisi moja pale Muhimbili lakini cha kushangaza Membe hakufia huko alifia hospitali ya Kairuki!
The probability that Membe did not die a natural death is very high.
 
Kushtaki au kutoshtaki ni uamuzi wao, hoja ni kwamba hospitali na daktari wamevunja maadili ya kitabibu ya kuvunja faragha za mgonjwa kinyume na matakwa ya familia.

Familia hata isiposhitaki, hilo halibadiliki.

Ni kama familia ikiibiwa na kulalamika kuwa imeibiwa, ikilalamika tu bila kushtaki, kulalamika huko hakuondoi ukweli kwamba wameibiwa.
Sasa kama waliotoa taarifa za kufariki kwa kifua ni hospitali ya Kairuki, kwanini anatishiwa kushtakiwa daktari?
 
Back
Top Bottom