Familia ya Membe yamkana aliyejiita daktari wake, yaapa kumpeleka mahakamani

Hana mamlaka hayo unless kwa kibari cha familia.

Hii hata akishtakiwa kwenye bodi ya yao atafungiwa Leseni yake.
Yule jamaa sio Dr wa mchezo mchezo nasikia kasoma Havard wakimfungia bongo anaruka zake Marekani akale Bata, inasemekana JK ndio alimleta bongo kutoka US alipokuwa anafanya kazi.
 
Hana mamlaka hayo unless kwa kibari cha familia.

Hii hata akishtakiwa kwenye bodi ya yao atafungiwa Leseni yake.
Familia ndio inamiliki hospitali anayofanya kazi?, yeye katoa waTz hofu, kaapishwa kuhudumia wa Tz, na leseni kapewa na serikali ya watz anaowahudumia.
 
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!

Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.

Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.

Huyo aliyesema ni Dr wa familia ya Membe jina lake nani?
Mimi nashauri Musiba na huyo Dr bora waondoke nchini waende nchi ambayo wenye hasira hawana ushawishi hadi hali itulie laa sivyo wata leftishwa bila hiari.
 
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!
Nami nilishangaa, iweje siri ya mgonjwa na daktari ianikwe bila ridhaa ya familia
 
Yeye kaapishwa kuhudumia waTz, na kawatoa hofu, hana haja ya ruhusa kufanya kazi yake
Sijui huwa unafanya makusudi au ni kweli una upeo Mdogo?

Ugonjwa wa mtu ni siri yake na daktari na akifa ni swala la familia.

Mbona wanaokufa kwa ukimwi hamtangazi?
 
Mimi pia nilishangaa kuona daktari anatoa habari za faragha za mgonjwa vile.

Nikafikiri labda amepata ruhusa ya familia.

Hawa madaktari wetu wanakuwa hawajui miiko ya utabibu kuhusu faragha ya mgonjwa?

Mbona haya ni mambo ya kawaida tu ambayo hata sisi tusio madaktari tunayafahamu?
 
Tena ni daktari bingwa, hilo ndio linazusha maswali kuliko majibu.
 
Familia ndio inamiliki hospitali anayofanya kazi?, yeye katoa waTz hofu, kaapishwa kuhudumia wa Tz, na leseni kapewa na serikali ya watz anaowahudumia.
Mkuu unaelewa kwamba madaktari wanakatazwa kutoa taarifa za mgonjwa bila ya idhini ya mgonjwa au mtu wa familia ya mgonjwa mwenye medical power of attorney?
 
Huyo anajizima data tu, hata mpendwa wao alivyokufa ni Rais ndiye aliyetangaza kifo chake na sababu za kifo chake na ana mandate hiyo kikatiba.
 
Back
Top Bottom