Familia ya Membe yamkana aliyejiita daktari wake, yaapa kumpeleka mahakamani

Familia ya Membe yamkana aliyejiita daktari wake, yaapa kumpeleka mahakamani

Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!

Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.

Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.

Hawa akina Membe wanapenda sana ligi za kijinga.., sasa mtu katoa watu hofu, shida ipo wapi?
 
Tangu siku ile niliposikia habari ya huyo daktari binafsi bila kupepesa macho na kuwaza mara mbili nilijua kabisa yule Daktari ni muongo, katumwa na watu fulani wasiojulikana na ule ulikuwa ni mpango kamili wa kucheza na akili za watu.

Soon mbichi na mbivu zitajulikana.
 
Minong'ono ndo imepata lift sasa.

Familia ya Membe wana haki ya kuwa na mashaka na dokta huyo aliyejipa jukumu la kuonge kuhusu kifo cha Membe.

Mimi naona kuna kitu nyuma ya pazia
 
Kwanza kiutaratibu dajtari hawezi kueleza maradhi ya mgonjwa au marehemu bila idhini ya mgonjwa mwenyewe (kama yupo hai na ana ufahamu) au familia (kama mgonjwa hana ufahamu au mgonjwa amefariki).

Kama daktari hakuwa na mamlaka ya familia, ashtakiwa na awe suspect wa kwanza, kama itaonekana kifo cha Membe hakikuwa natural. Huenda daktari kwa kupitia fani yake, alitumika na wabaya wa Membe kummaliza marehemu.

Yawezekana daktari alikuwa anafahamu kuwa marehemu atakwenda hospitali kwa checkup ya kawaida, na hivyo alivyoenda kwenye uchunguzi wa kawaida, alipandikizwa mwilini vitu vya kuundoa uhai wake, maana tunaambiwa tatizo lilianza baada ya yeye kwenda kwenye checkup ya afya yake ambayo huifanya kila mwaka.
Wewe ni miongoni mwa wanachadema ambao Nawaelewa sana na michango yako naiheshimu japo huwa tunakwaruzana sana tu!
 
Na sisi kama SG tunasema huyo hajafa natural death, maelezo zaidi karibuni Tocha.
 
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!

Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.

Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.

Wamdai 2Bs waunganishe na ile ya Musiba
 
Hiii familia imeachiwa Laaana ya kesi kesi na watakufa wote kwa misingi ya kesi zisizo na kichwa wala miguu. Shame on them.
Baba kafa kwa masimango ya kesi hata hajaoza Mitoto nayo inafungua kesi kwa Daktari na yenyewe inaweza kuondoka kwa kesi. Acha Mungu aamue ugomvi bahari itulie
 
Back
Top Bottom