Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 12,576
- 14,522
Familia ya marehemu Bernard Membe kupitia mwana familia anayeitwa Steven Membe wamemkana aliyejitambulisha kama daktari wa familia ya Membe alafu akaanza kuwatoa hofu wananchi kwa kuelezea namna marehemu Membe alivyofariki kwa kifo cha kawaida tu cha kubanwa na kifua hivyo wasiwe na wasiwasi!
Steven Membe amesema kama familia hawamjui huyo daktari na hawakumpa ruhusu kusema hayo aliyokuwa anayasema mbele ya watanzania.
Familia ya marehemu Membe wamempa siku saba daktari huyo kuomba radhi au wamburuze mahakamani.
Kwa hii style sioni unafuu wa case ya Musiba hata baada Membe kufariki!