Kwahiyo lengo lilikuwa kutaja ugonjwa wake au kuondoa wananchi hofu? Maana huyo alikuwa kiongozi wa umma, kwanini ungekufa wewe kuna mtu hata angeuliza umekufa na nini? Ukishaamuwa kuishi kwa public intrest (kiongozi) kuna Sacrifices unakuwa umezifanya tayari. Mfano mimi nikienda gesti hakuna mtu atakuwa na muda na mimi. Ila waziri mkuu akiingia tu gesti, waandishi wote wa habari watakuwa nje ya geti kumsubiri akitoka wamhoji, kwanini? Kwa sababu kuna maslahi ya umma ndani yake, huweZi kupenda asali halafu uking’atwa na nyuki kidogo uanze kulia lia.
Kilichofanyika ni kwa maslahi mapana ya taifa, kuna watu huvunjiwa nyumba zao kupisha barabara, kwa sababu maslahi ya umma huwa yanaanza kwanza.