Familia ya Mzee Ali Kibao yatuma ujumbe kwa Rais Samia, yaomba uchunguzi wa wazi pamoja na kutoa kauli kali dhidi ya wahusika wa utekaji na mauaji

Familia ya Mzee Ali Kibao yatuma ujumbe kwa Rais Samia, yaomba uchunguzi wa wazi pamoja na kutoa kauli kali dhidi ya wahusika wa utekaji na mauaji

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Familia ya Mzee Ali Kibao kupitia Mohamed Ali Kibao ambaye ni mtoto wa Mzee Kibao, imeomba uwepo wa uwazi na haki katika uchunguzi wa mauaji dhidi ya wahusika wa utekaji na mauaji ya Mzee Ali Kibao huku ikimsihi Rais Samia Suluhu Hassan, kutoa kauli kali dhidi ya wahusika ili kurejesha imani kwa dola na kupunguza hofu iliyotanda nchini.





Soma pia: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Ukivaa viatu vya familia ndipo utajua Maumivu yanafananaje.

Perhaps mama Samia kusema kifo ni kifo inawezekana haikua na Nia mbaya Ila ikatafsiliwa / nukuliwa vibaya
Serikali Ina mkono mpana Sanaa ikitaka kujua ukweli utajulikana TU

Pole zangu za dhati kwa watoto,familia , ndugu jamaa na marafiki walio guswa na huu msiba wa mzee WETU kibao
 
Wao watafute njia zingine za kufatilia waachane na wanasiasa na siasa
Kama wanaamini Mungu atawalipia, wasubiri, au watumie njia zao.
Anaonekana analipeleka kisiasa, sasa na yeye atajibiwa kisiasa, anaonekana ni wa chama cha maandamano, aje polepole
 
Kwanza najuwa maumivu kama familia haijalishi nini nyuma ya pazia ila inaumiza. Mimi ningependa kujuwa tu mimi sikuwahi kumsikia huyu mzee ila baada ya kifo chake kujuwa kuwa alikuwa Chadema kwenye siasa, lakini kuna wengi tunawajuwa wanaharakati matusi kila siku lakini wapo tu sasa kwanini huyu mzee? nini hasa labda alifanya kisiasa likaleta ukakasi ili tu link matukio. Kama ni kweli kauliwa sababu ya misimamo yake, kuna mtu yoyote anajuwa shughuli aliyofanya marehemu kufikia haya. Nia sio mbaya nikutaka harakati zake mpaka kuwa tishio kiasi hicho maana wako wengi wakorofi kweli lakini wanadunda.
 
Back
Top Bottom