Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni
Na zile zilzosemwa kuwa zimefichwa China ni Lissu alisema?.
 
Wewe ni jaji unayeendesha shaurikwahiyo unaitisha ushahidi? Ili uitwe ushahidi una sifa zipi ambazo wewe una uwezo wa kuzitumia kupima na ukaukubali au ukaukataa? Kama habari za uchunnguzi hujazielewa je ushahidi utauelewa na kukubali au utaweka mapenzi mbele?
Gobbledygook.
 
Unanilazimisha NITAKE unachotaka wewe?!!

Nijinyonge kwa kuwa wewe umependekeza mapendekezo yako ?!!

Uzwazwa huo.....

Nchi ni TAKATIFU...tunapanga mazao ,tunavuna na kupata chakula kwa UTULIVU kabisa....tunazaliana....tunajenga makazi ya kuishi....ikiwa huu si UTAKATIFU basi wewe "waumwa fikra koko".....
Hata nchi zenye vita wanalima na kuzaliana. Kama hauamini kaangalie DRC Congo, kisha tazama idadi ya watu na sisi watanzia tunaoongozwa na chama kimoja kwa shuruti.
 
Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.

Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?

Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381

Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.

Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.

Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.

Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.

Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.

If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.

Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.

Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.

Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.

Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.

Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.

Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.

Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.

Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.

Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?

Vigumu sana kuamini hilo.

Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.

La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.
Hilo sio suala la familia ya magufuli ni suala la serikari kutoka hadharani na kusema huo ni uongo na kutowa ukweli juu jambo la watu kupotea na kuuwaa.

Magufuli hakuwa watu akiwa kama raia aliuwa watu akiwa kama raisi . Ni kazi ya serikali kutowa ukweli kwa kufanya uchunguzi kwa kutumia vyombo vya kimataifa vinavyo aminika na kuweka ukweli hadharani. Vinginevya vitabu kama in the name of the president. Vitaandikwa vingi . Na hata movie za Hollywood ziko njiani.
 
Hilo sio suala la familia ya magufuli ni suala la serikari kutoka hadharani na kusema huo ni uongo na kutowa ukweli juu jambo la watu kupotea na kuuwaa.

Magufuli hakuwa watu akiwa kama raia aliuwa watu akiwa kama raisi . Ni kazi ya serikali kutowa ukweli kwa kufanya uchunguzi kwa kutumia vyombo vya kimataifa vinavyo aminika na kuweka ukweli hadharani. Vinginevya vitabu kama in the name of the president. Vitaandikwa vingi . Na hata movie za Hollywood ziko njiani.
Familia inaweza kabisa kumshitaki huyo mwandishi kwa libel.

Mna ujinga wa hali ya juu sana.
 
Rejea ya Qur'an:

Allah anasema katika Qur'an:


(Surat Al-Hujurat: 6)



Aya hii inasisitiza kwamba, kabla ya kuchukua hatua yoyote kwa msingi wa habari zilizopokelewa, inapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha ukweli wake.

Hadithi ya Mtume Muhammad (S.A.W):

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:


(Bukhari na Muslim)



Mtume alisisitiza umuhimu wa kuwa na tahadhari na habari ambazo hazijathibitishwa, kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Mfano wa Tukio:

Katika kipindi cha Mtume, taarifa zililetwa kwake kuhusu baadhi ya watu wa kabila fulani waliodaiwa kusaliti ahadi zao. Mtume hakuchukua hatua ya haraka, bali alituma wajumbe wake kuchunguza ukweli wa madai hayo. Uchunguzi huo ulizuia maamuzi ya haraka ambayo yangeweza kusababisha madhara kwa watu wasio na hatia.

Funzo kwa Jamii:

1. Kujiepusha na haraka: Hakuna maamuzi yanayopaswa kufanywa bila uchunguzi wa kina.


2. Kusikiliza pande zote: Usikivu wa haki unahakikisha kila mtu anapewa nafasi ya kueleza upande wake.


3. Kudumisha amani: Uchunguzi wa habari huondoa fitina na uvumi ambao unaweza kusababisha mtafaruku katika jamii.
Mnaua halafu mnajificha kwa mtume
 
Tungekuwa na polisi wanaojielewa wangekuwa wamemkamata na kuanza kumhoji kuthibitisha ushahidi na kama ni uongo abanwe kende zake Hadi zipasuke.Huwezi kuua mtu ikulu mbele ya umati wa watu.Haya madai anaweza kuyaamini kichaa tu
Magufuli alikuwa muuaje, koma kumtetea
 
Familia inaweza kabisa kumshitaki huyo mwandishi kwa libel.

Mna ujinga wa hali ya juu sana.
Hakuna familia yenye raisi.raisi ni wa nchi sio wa familia. Ndio maana kasema in the name of the president. Kama kuna mkuu wa familia anaitwa president basi familia ya president inaweza kumshitaki.

Na hata hivyo kwa kuwa anayesemwa ni raisi , na walio potea ni watu halisi , basi ili familia iweze kushinda case ni lazima iwe inaweza kudhibitisha kuwa kilicho semwa ni uongo.
 
Naam Magufuli alikuwa katili sana. Afadhari alikufa
 
Zamani nilikuona nikiona mtu kaandika kiingereza nilikuwa najua ni point za maana tupu, kumbe nilikuwa najidanganya.
Hata sijaandika mkuu nimekopy na kupaste baada ya kusoma na kuelewa hicho kilichoandikwa na wengine ambao hata hawajui kama kuna mtu fulani huku Tanzania anapitia hiyo changamoto.

Kabendera nae katumia kiingereza kwenye kitabu chake vp mtazamo wako?
 
Hakuna familia yenye raisi.raisi ni wa nchi sio wa familia. Ndio maana kasema in the name of the president. Kama kuna mkuu wa familia anaitwa president basi familia ya president inaweza kumshitaki.

Na hata hivyo kwa kuwa anayesemwa ni raisi , na walio potea ni watu halisi , basi ili familia iweze kushinda case ni lazima iwe inaweza kudhibitisha kuwa kilicho semwa ni uongo.
Bullshit.
 
Nimecheka 😁😁😁😁 kumbe joni alienda usiku na penzi nyanya Kwa ________ hiking kitabu Noma sana
 
Back
Top Bottom