Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😆😆😆😆 Hizo kesi wataabika mana hata watu wa mkuranga watakuja kutoa ushahidiFamilia yenyewe wana ushahidi wa kuthibitisha kuwa Magufuli hakuua?.
I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.m
Wanalima halafu WANYAMULENGE wanayachoma moto mazao ....Hata nchi zenye vita wanalima na kuzaliana. Kama hauamini kaangalie DRC Congo, kisha tazama idadi ya watu na sisi watanzia tunaoongozwa na chama kimoja kwa shuruti.
Kama anao ndo vizuri sasa.Ila @ Nyani Ngabu wewe ni nani kutaka Kabendera aburuzwe mahakamani? What if ana ushahidi? Utareconmend auawe?
Wewe ni mtu mwenye heshima zako ndani ya Jf ...tena muda mrefu,hudhani bandiko lako linaweza kumnyima haki anayepaswa na kuyapa majangili ushindi? Magufuli alikua malaika?Kama anao ndo vizuri sasa.
Familia haiwajibiki kuthibitisha hakuua.Familia yenyewe wana ushahidi wa kuthibitisha kuwa Magufuli hakuua?.
Hahahaaa! Mimi nina heshima gani hapa JF jamani? 🤣Wewe ni mtu mwenye heshima zako ndani ya Jf ...tena muda mrefu,hudhani bandiko lako linaweza kumnyima haki anayepaswa na kuyapa majangili ushindi? Magufuli alikua malaika?
Magufuli aliacha Familia!?Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.
Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?
Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381
Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.
Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.
Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.
Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.
Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.
Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.
If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.
Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.
Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.
Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.
Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.
Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.
Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.
Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.
Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.
Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.
Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?
Vigumu sana kuamini hilo.
Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.
La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.
Mzee Kibao aliuawa na Polisi,Nondo alitekwa na polisi...ulitaka waje FBI kuthibitisha tuhuma dhidi ya polisi au ulitaka waliokuwepo kwenye eneo la uhalifu wakahojiwe na waliofanya uhalifu ?Familia haiwajibiki kuthibitisha hakuua.
Mwenye wajibu wa kuthibitisha ni anayetoa tuhuma.
Kuna watu bado mna ujinga wa kutisha na kusikitisha sana.
It strains credulity!Vitu vya kuambiwa sio ushahidi, ninashangaa kusikia msomi wa fani ya sheria anasema "niliambiwa na mtu mkubwa " huo ukubwa sio ushahidi. Fikiria kuwa mtu kuuwawa tena ikulu, ofisi ya serikali, huyu jamaa ana ujasiri gani wa kuchafua ikulu? Sasa tunaomba uchunguzi wa kisayansi kuhusu hilo jambo.
He left your mama’s yellow discharge.Magufuli aliacha Familia!?
Sijaelewa ulichokiandika.Mzee Kibao aliuawa na Polisi,Nondo alitekwa na polisi...ulitaka waje FBI kuthibitisha tuhuma dhidi ya polisi au ulitaka waliokuwepo kwenye eneo la uhalifu wakahojiwe na waliofanya uhalifu ?
Umeshakua na bias utaelewaje?Sijaelewa ulichokiandika.
oKama kweli hiyo picha ipo kwenye hilo cover la kitabu. Huyu jamaa alipaswa sasa hivi awe ameshatiwa nguvuni na vyombo husika na siyo vinginevyo
Keep it movin’.Umeshakua na bias utaelewaje?
Uzushi tu.Informers wa Kabendera wanao ushahidi wa kuona.
Natamani sana waende mahakamani, tutajua wapi panuvuja.Katika watu hao mimi niko msitari wa mbele kabisa. Kwa bahati mbaya sidhani kama yuko mwenye ujasiri wa kufanya hivyo!