Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Awataje wa nini, yeye amemtaja aliyempiga risasi Ben Saanane. Kama vipi kawasaidie familia ya Magufuli kufungua kesi ya kupinga huo ukweli.
Kuna kitu kinaitwa pandora box, je familia ya jiwe ina ujasiri wa kubariki na kutaka lifunguliwe?

Hiyo kesi haitakuwa tu ya kitaifa, itakuwa ya kimataifa. Dunia yote itafuatilia yanayojiri.

Be careful of what you wish for Nyani Ngabu! Je unajua kwa nini hakuna uchunguzi wowote ule ulifanyika?

Unachowashauri wana familia wakifanye ni ujinga, ndiyo ni ushauri wa kijinga.

Juhudi gani zilifanywa na jemadari mkuu kumlinda raia wake Ben Saanane? Hakuna!
 
Nakubaliana na wewe kwani laiti Serikali ingekubali kuwaomba Scotland Yard au FBI kusaidia upelelezi na mhusika kukamatwa leo hii kashfa hii isingekuwepo.
 
Magufuli alikuwa kichaa na mlevi wa madaraka aliyependa kusifiwa sana. Hizi tuhuma sio mpya na kwa mtu anayemjua vizuri huyo shetani wa Chato, hilo tukio alilifanya na mengine mengi kama hilo
Una maana hata mrithi wake ni kichaa? Mbona naye anapenda kusifiwa hadi kuwaita watu machawa kama mwendaze alivyozoea kuwaita wanyonge?
 
I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.
Kabendera ni Mwandishi , kuna sheria ya kulinda 'source'
Anaweza kushtakiwa kwa 'madai ' aliyotoa siyo 'source'' . Kumbuka alifahamu uzito wa hoja na aliwasiliana na Wanasheria kabla . Kumburuza mahakamani kunaweza kuzua mazito zaidi. Jiulize kwanini ameandika ''boldly''

Jenerali Ulimwengu na gazeti Rai walimtuhumu Hans Kitime kuhusu matibabu ya milioni 60 wakati huo.
Walitakiwa kutoa ushahidi, wakaweka kila kitu hadharani, hawakushinikizwa kutaja ''source''
Mkapa hakuwa na uwezo wa kumshtaki akadai si Raia
 
Akiguswa mtu wenu mnakuja juu,nyie kutwa mnamtukana Samia lakini mbona hamshtakiwi popote?au kwann huwa mnafurahia wapuuzi wakimtusi Samia?unadhani familia ya samia inafurahia?!

Kabendera alichoandika kama kweli au uongo ni haki yake kikatiba uhuru wakutoa maoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…