Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo ni kweli kuwa Magufuli alimpiga risasi Ben baada ya kumuumbua kuwa ile PhD yake ilikuwa ya mchongo? ??Kuna makosa mtu ukifanyiwa adhabu inayotosha kutoa ni kifo.
Mimi sishangai mtu akiua..!
Kuna kitu kinaitwa pandora box, je familia ya jiwe ina ujasiri wa kubariki na kutaka lifunguliwe?Awataje wa nini, yeye amemtaja aliyempiga risasi Ben Saanane. Kama vipi kawasaidie familia ya Magufuli kufungua kesi ya kupinga huo ukweli.
PhD Tano za Saa100 unazionaje?Kwa hiyo ni kweli kuwa Magufuli alimpiga risasi Ben baada ya kumuumbua kuwa ile PhD yake ilikuwa ya mchongo? ??
Muache baba yangu apumzike kwa amani.Kwa hiyo ni kweli kuwa Magufuli alimpiga risasi Ben baada ya kumuumbua kuwa ile PhD yake ilikuwa ya mchongo? ??
Nakubaliana na wewe kwani laiti Serikali ingekubali kuwaomba Scotland Yard au FBI kusaidia upelelezi na mhusika kukamatwa leo hii kashfa hii isingekuwepo.MTUME KATIKA MASWALA KAMA HAYA
Tukio katika maisha ya Mtume:
Katika tukio moja, kipindi cha Mtume, mtu mmoja kutoka kabila fulani aliuawa bila haki. Mtume aliagiza uchunguzi wa haraka ufanyike na kuhakikisha waliotekeleza mauaji wanawajibika. Katika tukio hili, Mtume aliwaonya viongozi wa jamii dhidi ya upendeleo au kuchelewesha haki, akisema:
(Bukhari, Muslim)
Mtume alisisitiza kuwa kuchelewesha haki au kuzembea katika kushughulikia dhuluma kunaweza kusababisha Mtaarufuku mkubwa katika jamii
Cc
Nyani Ngabu
Nimetembea kwenye kauli yako iliyomaanisha kuwa kama kweli Ben alikuwa mkosaji alistahili kuuwawa.Muache baba yangu apumzike kwa amani.
Semeni make wake achukue hatua!Naunga mkono hoja.hata kama serikali haitachukua hatua basi familia imshtaki huyu mpuuzi
Una maana hata mrithi wake ni kichaa? Mbona naye anapenda kusifiwa hadi kuwaita watu machawa kama mwendaze alivyozoea kuwaita wanyonge?Magufuli alikuwa kichaa na mlevi wa madaraka aliyependa kusifiwa sana. Hizi tuhuma sio mpya na kwa mtu anayemjua vizuri huyo shetani wa Chato, hilo tukio alilifanya na mengine mengi kama hilo
Wewe ni hakimu?.I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.
Na serikali ya imekaa kimya ikikubaliana na Mbowe kumuua Ali Kibao? Umeishakuwa kubwa la majingaMbowe.
Nenda usambaani wakakutibu akili yako ipone umekuwa ni kituko jukwaaniGentleman,
nilidhani mwisho wa mawenge ulikua ni2024, naona umevuka nayo dah!![]()
Haukuwahi kufanyika na hili ndiyo linazidi kutia shaka hadi kupelekea wengi kuamini hiki alichoandika Kabendera.Hivi Uchunguzi wa kifo chake ulisha kamilika?
Kuna tuhuma zinatolewa kimtego sana ili watu wajae wazimawazima kudai ushahidi ndipo yafumuliwe madudu, ndiyo maana walengwa huchagua kupiga kimya
Kabendera ni Mwandishi , kuna sheria ya kulinda 'source'I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.
VaticanPapa kiongozi wa nchi gani
Akiguswa mtu wenu mnakuja juu,nyie kutwa mnamtukana Samia lakini mbona hamshtakiwi popote?au kwann huwa mnafurahia wapuuzi wakimtusi Samia?unadhani familia ya samia inafurahia?!Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.
Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?
Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381
Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.
Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.
Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.
Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.
Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.
Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.
If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.
Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.
Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.
Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.
Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.
Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.
Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.
Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.
Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.
Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.
Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?
Vigumu sana kuamini hilo.
Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.
La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.