Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Kabendera ni Mwandishi , kuna sheria ya kulinda 'source'
Anaweza kushtakiwa kwa 'madai ' aliyotoa siyo 'source'' . Kumbuka alifahamu uzito wa hoja na aliwasiliana na Wanasheria kabla . Kumburuza mahakamani kunaweza kuzua mazito zaidi. Jiulize kwanini ameandika ''boldly''

Jenerali Ulimwengu na gazeti Rai walimtuhumu Hans Kitime kuhusu matibabu ya milioni 60 wakati huo.
Walitakiwa kutoa ushahidi, wakaweka kila kitu hadharani, hawakushinikizwa kutaja ''source''
Mkapa hakuwa na uwezo wa kumshtaki akadai si Raia
Hiyo sheria ya kulinda source inasomekaje? Niwekee hapa.

Naamini, kama ipo kweli, hairuhusi watu kuitumia kama kichaka cha kuzushia watu mambo.

What’s next? Mwandishi mwingine kudai Magufuli alimlawiti Maria Nyerere na kutumia hiyo sheria kujificha chini yake?
 
Magufuli alikuwa mtu wa kuendeshwa na hisia sana kuna uwezekano hilo jambo likawa lina ukweli ndani yake.
Mbona Kuna Uzi uliletwa miaka ya 2021, na ule Uzi uliandikwa kimafumbo kwamba bwana mkubwa alichafukwa sana ...Hasira sanaaa
Sasa akiwa kwenye jumba jeupe akawa anamtishia dogo kwamba unaona hii..(mguu wa kuku)..akiwa na jazba sana ..akimuuliza nani anamtuma Hadi UDSM kufuatilia machapisho yake ..
Sasa ghafla ..akisema unaona hii ..kitu kikachomoka kutoka chamber ...

Wale jamaa wakamwambia boss inatoshaaa...wakachukua mwili na Kwenda kutupa majini ...ule Uzi haukufafanua majini wapi ...
Wadau wakahisi labda Bahari ya hindi
 
Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.

Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?

Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381

Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.

Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.

Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.

Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.

Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.

If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.

Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.

Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.

Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.

Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.

Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.

Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.

Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.

Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.

Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?

Vigumu sana kuamini hilo.

Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.

La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.
Jamaa kwenye kitabu chake kaandika ujinga wa hali ya juu.
Daah
 
Exactly! Publisher aliona hili jambo na anajua madhara yake. Kabendera ni Mwandishi wa Kimataifa anajua madhara yake. Watu waliofanya review ni wenye weledi wanajua madhara yake. Wanasheria wa Kabendera wanajua madhara yake. Yote hayo bado imendikwa ''Boldy''

Nina uhakika kuna watu wanatamani na kuomba hili suala liende mahakamani!
Kuna waandishi wa kimataifa wengi tu ambao waliandika mambo ya uongo na wakashitakiwa na kuamrishwa kulipa fidia na kuomba radhi.

Kabendera is not above lying, is not above calumnies.

George Stephanopolous juzi hapa kaamrishwa kuomba radhi.

Hata BBC waliwahi kumlipa fidia Salmin Amour.
 
Wakati mwi
Ng
Wewe nawe, umeanza kuwa kituko. Unafikiri Familia haijui kwamba Jpm alikuwa muuaji? Wewe ndio umekuwa family advisor?
Ushahidi uko wapi kuwa Magufuli alimuua Ben?

Naona wengi mnaongozwa na hisia tu.
 
Niliandika mara nyingi sana humu kuwa Magufuli ni muuaji. Chawa wake mkawa mnatukana.

Sasa badala ya kuandika uzi (thread) kimeandikwa kitabu.

Nakazia: Magufuli ni muuaji, mporaji na mekaji.
Where’s the proof?
 
Hiyo sheria ya kulinda source inasomekaje? Niwekee hapa.

Naamini, kama ipo kweli, hairuhusi watu kuitumia kama kichaka cha kuzushia watu mambo.

What’s next? Mwandishi mwingine kudai Magufuli alimlawiti Maria Nyerere na kutumia hiyo sheria kujificha chini yake?
Kabendera kasema Magufuli alimzukia Samia na pajama akitaka kumbaka.

Samia akataka kujiuzulu u Makamu wa Rais.

Mshitakini Kabendera mahakamani amuite Samia kutoa ushahidi tujue ukweli.
 
Wapi ushahidi Magufuli alimuua Ben kwa kumpiga risasi?

Naona watu mnapenda tu sensationalism.
Wewe ni jaji unayeendesha shaurikwahiyo unaitisha ushahidi? Ili uitwe ushahidi una sifa zipi ambazo wewe una uwezo wa kuzitumia kupima na ukaukubali au ukaukataa? Kama habari za uchunnguzi hujazielewa je ushahidi utauelewa na kukubali au utaweka mapenzi mbele?
 
Hakuna nchi takatifu hapa boss. Usitake uchafu wa viongozi ufichwe kwa kusaka sifa zisizokuwepo. Kama kiongozi ni mchafu huyo ni mchafu, na uchafu wake utawekwa wazi peupe. Hutaki jinyonge.
Unanilazimisha NITAKE unachotaka wewe?!!

Nijinyonge kwa kuwa wewe umependekeza mapendekezo yako ?!!

Uzwazwa huo.....

Nchi ni TAKATIFU...tunapanga mazao ,tunavuna na kupata chakula kwa UTULIVU kabisa....tunazaliana....tunajenga makazi ya kuishi....ikiwa huu si UTAKATIFU basi wewe "waumwa fikra koko".....
 
Na familia ambazo Magufuli amesababisha wabaki yatima na wajane nao wamshtaki nani? Yani watu waliouwawa na serikali ya magufuli nyie mnaona yeye ndo ana haki ya kupiganiwa tu.

Hii nchi viazi ni wengi sana. Kwanza mimi nilivyosikia magufulia amefariki usiku ule niliamka hapo hapo nikaenda bar kujipoza kidogo. He was rude.

Ameiharibu nchi mpaka sasa hawaoni shida kuua, yani mpaka hotuba ya juzi ya mama yenu anatoa hotuba alaf haoni kama utekaji na mauaji kwa mwaka 2024 ni tatizo. Yani anaona kama waliokufa ni kuku tu au panzi vile
yaani afadhali umesema saa100 aliniacha hoi pale ambapo hajagusia utekaji na mauaji ya raia,nikahesabu tunaraisi waajabu sana haijawahi tokea
 
Ww unajuaje km sio kweli? Maana mpaka mtu kuandika ana infomation
Jinga na pumbavu kabisa wewe.

Kisa tu jambo limeandikwa hilo halimaanishi kwamba ni la kweli.

Waandishi wangapi na vyombo vya habari vimekuwa sued kwa kuandika habari za uongo?

The level of stupidity is breathtaking. Good grief.

Maandishi ya mwandishi wa habari siyo gospel truth.

So dumb!
 
Hate can negatively affect the body by triggering the release of stress hormones, leading to increased inflammation throughout the body, which can manifest in various physical symptoms like headaches, digestive issues, high blood pressure, weakened immune system, and even increased risk of heart disease, all due to the chronic stress associated with harboring hatred; it can also contribute to mental health problems like anxiety and depression.
Zamani nilikuona nikiona mtu kaandika kiingereza nilikuwa najua ni point za maana tupu, kumbe nilikuwa najidanganya.
 
Lakini tayari yeye kashadanganya uraia tutajuaje kama anaendelea kudanganya na hayo mengine?
Sijali uraia wake, najali ukweli alioongea. We fuatilia nchi anayotoka, mimi nafuatilia ukweli aliosema kuhusu dhalimu magu.
 
Sku izi namuona mjane kanenepa hana stress
Ww unakuja mshauri ujinga mjane ebu muache mama apumzike ni mengi kapitia uko nyuma, saiv ni muda wake wa kuenjoy pensheni za jiwe
 
Mkuu NN aliyetuhumiwa ni Rais John Magufuli, kwamba tuhuma hizo zimeelekezwa kwa mtu aliyekuwa na madaraka ya uRais na sio John Magufuli aliyekuwa mtu tu asiye na cheo cha kitaifa kwamba familia yake imburuze bwana Kabendera kwa mizania hiyo...

Nadhani kama kuna kupelekana mahakamani basi ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ndio wataohangaika na bwana Kabendera...
You are splitting hairs.

John Magufuli Rais na John Magufuli aliyekuwa baba, mume, nk., ni mtu huyo huyo.

Unless unionyeshe sheria inayokataza kabisa familia yake kumshitaki huyo mwandishi, hoja yako haina mashiko.

Familia inaweza kabisa kumshitaki huyo mwandishi, civilly.

Serikali ndo inaweza kumshitaki criminally.

Umechanganya mambo hapo.
 
Back
Top Bottom