Ironbutterfly
JF-Expert Member
- Feb 5, 2023
- 3,042
- 8,227
Habari za eid pili waungwana,
Iko hivi, nimejaliwa kuzaa watoto wawili wa kiume na bwana mmoja. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo, hatukuoana na huyo bwana. Watoto wote nilikuwa naishi nao kwangu, huku tukisaidizana malezi. Yeye alishaoa kama miaka mitatu nyuma.
Kama miaka miwili nyuma nilipata changamoto kazini na mambo mengi yalitokea upande wangu hivyo sikuwa stable kuendelea kuishi na watoto. Tulipojadiliana pande zote, wazazi wake wakasema niwakabidhi watoto wawalee hadi hapo nitakapo kuwa sawa.
Basi watoto nikawapeleka kwao, nikawa na still huwa naenda kuwatembelea pindi nipatapo nafasi pamoja na kuchangia gharama za ada na mahitaji mengine ya watoto.
Muda umeenda, nimerudi kwenye fomu, na nimeona nahitaji kuwachukua watoto niwalee sasa, yaani niishi nao huku nilikohamia kikazi. Wazazi wake bwana yule wamekuja na wazo kuwa, familia yao imeamua jamaa anitolee mahari kwa mujibu wa mila zao, so wamenambia niifahamishe wazee wangu ili taratibu zifanyike.
Binafsi sijaafiki suala hilo, kwani jamaa alishaoa na kashazaa watoto wengine wawili kwa mkewe. Hata mila za kwetu haziafiki jambo hilo, isitoshe mimi niko na mtu wangu ambaye tuna plan zetu za hapo baadae kidogo, naona kama ni mbinu ya kunizuia kuchukua wanangu.
Hebu mnipe ushauri wadau, namna gani naweza kuwachukua watoto bila kuleta mikwaruzano?