Familia yake wanataka kunitolea mahari

Familia yake wanataka kunitolea mahari

Je umeshazungumza na mzazi mwezio kuhisiana na hilo swala la ndoa?
Watoto wanahitaji malezi ya pande zote mbili.
Nini msimamo wako?
Simamia msimamo wako ambao unaona ni sahihi,sisi tuko na wewe.
Furaha yako kwanza.
Mapenzi hayashauriwi.
 
[emoji1787][emoji1787] Ahh gily kuzaa na bwana yule haikuwa bahati mbaya si unajua mambo ya ujana na ,mbingu tu hazikupanga tuoane[emoji120]
Wamenambia nikiwachukua watoto bwana yule atawasusa,ndo wakaja na wazo hilo la mahari.
Wewe nani kakuambia mbingu hazikupanga muonane,vitu vya kuongozwa na hisia vikishaletaga matokeo ndio mnasingizia ni mbingu zimetaka....kaa kwa kutulia hapo inaonesha umeanza kupata ka kiburi ili ukazalishe mikwaruzo kwenye ndoa mpya....maana humpendi huyu bwana mpya bali unataka ukajistiri kwa jina la ndoa,
 
Ohhh fidia ndio inakuwaje?
Alikuwa awe mke wa ndoa ndio watu wanasemaga ila hajawa anamtoto wako tu,basi mnapiga mahesabu kuanzia elimu yake aligharimu kiasi gani,na kubeba mimba hadi kujifungua alitumia how much na mpaka mtoto alipo Sasa analitumia how much kumtunza mtoto wako,basi navingine wazazi watakachodai so mtoto ni wako tayari ukimuhitaji unasepa naye Sasa .
 
Waache watoto waendelee kulelewa na Bibi yao..Wabibi ni Walezi wazuri sana..utakapowachukua means watalelewa na Dada utakapokua kazini of which they will be in highly risk of facing abuse unless otherwise you’re a PROUDLY HOUSEWIFE

HAKUNA MWANAUME ANAEPENDA KULEA WATOTO WA MWANAUME MWENZIE HUSUSANI AKIJUA KABISA MWANAUME MWENZIE YUKO HAI ..YAAN MWANAUME HUYO HAYUPO 🔨

Cases nyingi za Child abuse zinafanywa na Baba wa Kambo..don’t dare I repeat don’t dare
 
Usikubali hautawapata hao watoto. Hilo wazo wangekupa wakati ukiwapeleka wakaishi nao. Kama kweli hawana nia ya kuwang'ang'ania watoto wakupe kwanza uishi nao kisha waendelee na mipango yao
 
Wanaume gani hao wasiopenda watoto wa kambo...hiyo sample size Yako ndogo mno...labda ni wewe! Wanaume wakipenda wanapenda mazima!
 
Kwa upande wangu itaniharibia,we mtu wangu akijua nimetolewa mahari na baby dady atajisikiaje?
Suala si kumuonea huruma mtu wako. Msimano wako kuhusu mwanaume uliyezaa nae usimuhusishe uliye naye sasa, angalia thamani yako na unachotaka.

Huyo mtu wako kuamua kuwa na mwanamke aina yako ametake risk, huenda na yeye yupo mguu ndani mguu nje akisubiri umprove kuwa alifanya makosa hivyo usichukue maamuzi kwa kumuonea huruma.

Kama thamani yako ni kutolewa mahari na wazazi wa mume wa mwingine nenda katolewe lakini usiseme hukufanya sababu mtu wako angejisikia vibaya.

Kama hufanyi sababu iwe ni wewe na thamani yako na utu wako na heshima yako na sio mpenzi uliye naye. Yaani hata usingekuwa na mtu still ungeamua hilo uliloliamua.
 
Usikubali hautawapata hao watoto. Hilo wazo wangekupa wakati ukiwapeleka wakaishi nao. Kama kweli hawana nia ya kuwang'ang'ania watoto wakupe kwanza uishi nao kisha waendelee na mipango yao
ivi ni kwa nini watu hung'ang'ania watoto
 
Maslahi. Mfano misibani,ndugu wanang'ang'ania watoto ili waipate mirathi yao. Kwa kesi ya mleta mada hapo wanapata posho ndogo ndogo toka kwa Baba yao. Hivyo mleta mada kuwachukua watoto atakua kakata mirija yao ya posho

aisee kuna mambo yanashangaza sana ,ila hakuna kitu kibaya kama mwanamke afahamu unampenda sana mtoto wako atamtumia kukutesa sana usipokuwa makini
 
Sasa kwa mila za kwetu mahari inapokelewa kwaajil ya ndoa tu🙏hivyo hapaswi kutoa hiyo mahari,yeye anatambulika nyumbani Kama mzazi mwenzangu tu.
Mwambie atoe fidia kuwakomboa watoto watambulike ubabani na sio mahari.
Mahari ya kuhalalisha watoto sijawahi kuisikia!
 
Habari za eid pili waungwana,

Iko hivi, nimejaliwa kuzaa watoto wawili wa kiume na bwana mmoja. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo, hatukuoana na huyo bwana. Watoto wote nilikuwa naishi nao kwangu, huku tukisaidizana malezi. Yeye alishaoa kama miaka mitatu nyuma.

Kama miaka miwili nyuma nilipata changamoto kazini na mambo mengi yalitokea upande wangu hivyo sikuwa stable kuendelea kuishi na watoto. Tulipojadiliana pande zote, wazazi wake wakasema niwakabidhi watoto wawalee hadi hapo nitakapo kuwa sawa.

Basi watoto nikawapeleka kwao, nikawa na still huwa naenda kuwatembelea pindi nipatapo nafasi pamoja na kuchangia gharama za ada na mahitaji mengine ya watoto.

Muda umeenda, nimerudi kwenye fomu, na nimeona nahitaji kuwachukua watoto niwalee sasa, yaani niishi nao huku nilikohamia kikazi. Wazazi wake bwana yule wamekuja na wazo kuwa, familia yao imeamua jamaa anitolee mahari kwa mujibu wa mila zao, so wamenambia niifahamishe wazee wangu ili taratibu zifanyike.

Binafsi sijaafiki suala hilo, kwani jamaa alishaoa na kashazaa watoto wengine wawili kwa mkewe. Hata mila za kwetu haziafiki jambo hilo, isitoshe mimi niko na mtu wangu ambaye tuna plan zetu za hapo baadae kidogo, naona kama ni mbinu ya kunizuia kuchukua wanangu.

Hebu mnipe ushauri wadau, namna gani naweza kuwachukua watoto bila kuleta mikwaruzano?
Kutolewa mahari maanabyake si ndo kuolewa ama mm ndo nafikiria vibaya
 
Kubali watoe mahari then chukua watoto wako . Itasaidia baadae hao watoto kupata haki kwa baba yao. Ieleweke kuwa huyo bwana uliyenaye si baba wa hao watoto na hata siku moja hawatakuwa na furaha na huyo baba wakambo as long as baba yao anaishi
 
ndo wakaja na wazo hilo la mahari.
Washirikishe wazee upande wako pia,

Pia neno "mahari" sio sahihi kutumika, sababu huto olewa na huyo baba watoto.

Pande zote mbili za wazazi wako(mama watoto) na wazazi wake mwanaume(baba watoto), wakubaliane na watafute msamiati sahihi usio na ukakasi hasa atakapo julishwa huyu mume wako mpya,

Walio tangualia kuchangia wamependekeza neno kama | "Gharama za kukomboa watoto" ili watambulike rasmi ukoo wa mwanaume , au "Fidia kwa familia yako", ili kuziunganisha hizi familia mbili, kwa sababu ya kuzaa watoto ambao wao tayari wamewatambua pasipo wewe kuolewa baba husika wa watoto ambaye tayari ana familia nyingine.

Familia zote mbili zikifikia muafaka, mapema kabisa mueleze mume wako mpya bila kufichwa Jambo lolote,

Kitu muhimu kwa sasa weka "haki na maslahi ya watoto kwa siku za usoni", wote hatujui nani atatangulia kufariki kati ya wewe na huyo baba wa watoto, Na je hatima ya watoto ni ipi?
 
Kubali watoe mahari then chukua watoto wako . Itasaidia baadae hao watoto kupata haki kwa baba yao. Ieleweke kuwa huyo bwana uliyenaye si baba wa hao watoto na hata siku moja hawatakuwa na furaha na huyo baba wakambo as long as baba yao anaishi
Na ieleweke kwamba hakuna baba wa kambo atarithisha mtoto si wake, na mkishaoana ndio inaanza ile migogoro ya kwa nini mtoto wangu humthamini kama wako etc.
 
Back
Top Bottom