Familia yangu Mke na Mtoto wangu Mkubwa wamepata tatizo la Akili naomba ushauri wakuu

Familia yangu Mke na Mtoto wangu Mkubwa wamepata tatizo la Akili naomba ushauri wakuu

Umesema mtu akidai jambo fulani ni kweli na uhakika unamdai uthibitisho, sasa ajabu unadai uthibitisho wa Mungu na majini tu mbona hudai uthibitisho kwa vitu vyengine ambavyo watu hudai ni kweli na uhakika ila bila uthibitisho?

Ndio maana nasema hakuna haja ya kuthibitisha uwepo wa Mungu kama ambavyo ilivyo kwa mambo mengine hatuoni watu kudai uthibitisho na maisha yanaendelea. Sasa kwa sababu wewe una mtazamo wako wa kudai hakuna Mungu ndio maana unashughulishwa na kudai uthibitisho wa kuwepo Mungu.

Vitu vyengine simple tu wewe kama haukubaliani na habari za uwepo wa Mungu unaachana nazo haina haja ya kutaka kulazimisha watu et wathibitishe.
Hakuna siku nimeangaika na uwepo wa Mungu ila wewe ukileta uwepo wake nitadai uthibitisho wake kwa hili ni haki yangu wala usinipangie
 
Yani waganga wako wengi sana siku hizi wapo hadi mitandaoni hivyo ukiona mtu anakwambia akupeleke kwa mganga basi maana yake anamjua huyo mganga si tapeli na fundi hasa.
Kama Umesha Wahi Kukutana Na Mtu Mwenye Matatizo Utamtambua Kwa Jambo Dogo Tu

Mtu Anajitokeza Na Kutaka Kukupa Msaada Tena Bure Na Wewe Unakataa Jua Kabisa Huyo Mtu Haitaji Msaada Ukiona Mtu Anahitaji Msaada Alafu Yeye Ndo Anapanga Masharti Ya Jinsi Ya Kusaidiwa Huyo Sio Muhitaji.

Huyu Mleta Mada Ana Shida Ya Michango Ya Pesa Hicho Ndo Anachokihitaji Ila Sio Kutatua Tatizo Linalomkumbu La kuuguliwa Na Wana Familia.
 
Kabla Ya Kutaka Kuthibitisha Uwepo Wa Mungu Anza Kuthibitisha Hapa Jukwaani Kwamba Unazo Akili.
Hapo haujathibitisha uwepo wa huyo Mungu zaidi ya blabla zako tu za kijinga.
 
Hakuna siku nimeangaika na uwepo wa Mungu ila wewe ukileta uwepo wake nitadai uthibitisho wake kwa hili ni haki yangu wala usinipangie
Unangaika mkuu ndio maana nimekuuliza mbona haujawahi kumdai mtu uthibitisho wa wazazi wake kama kweli ni wazazi wake waliyomzaa ukaniambie mie ndio nifanye hivyo kwa maana wewe unangaika na habari za uwepo wa Mungu na majini ila madai mengine yasio na uthibitisho huangaiki nayo kudai uthibitisho wake.

Hakuna aliyekushikia bunduki wala kukunyima haki zako za msingi kwa kukulazimisha kukubali uwepo wa Mungu, sasa mtu akisema Mungu yupo kiuhakika wewe unapungukiwa nini? Potezea kama unavyopotezea madai mengine yasio na uthibitisho, mbona simple wala usingekuwa unabishana na watu.
 
Habari wanaJF .

Kiufupi Mimi Baba wa watoto watatu ambao wote ni wa kike.

Naishi nao pamoja na Mama yao .

Tumefanikiwa kuishi miaka 12 mpaka sasa katika ndoa yetu.

Changamoto kubwa ambayo ninaipitia ni hii hapa.

Mimi kazi yangu kubwa ambayo huwa nafanya ni kuuza mazao , kuku wa kienyeji huwa naenda kijijini naangalia bei ndogo ya bidhaa Kama mahindi au kuku nanunua na kuja kuuza mjini.

Kiufupi Mimi ni mjasiriamali wa kiwango cha chini ambaye bado napambana.

Jambo Ambalo limenifanya nije ni changamoto iliyompata mke wangu na watoto.

Familia yangu ilikuwa vizuri Ila ilianza kuingia changamoto ambazo zimeniumiza Sana Akili na kunipa mawazo.

Mwezi wa kumi Mke wangu alianza kuumwa kawaida kabisa nikampeleka hosptali kumpima ikaonekana hana tatizo .

Ila nikikaa nae usiku halali anaongea mambo Kama ya kuchizika Anapasua vitu ndani .

Sasa nikaona hii hali itakuwa mbaya nimempeleka hosptali zote za mkoa Government na private Ila tatizo lipo pale pale .

Napoandika hapa mke wangu amefungiwa ndani , sasa hii hali Kama ya Mke wangu imeanza kumungia mtoto wangu wa kwanza Ana umri wa miaka 10 anaongea peke yake anaharibu vitu ndani .

Akikaa kidogo na wadogo zake wanapigwa kipigo kikali Sana hivyo mtoto na mama yao ambaye ni mke wangu ni Kama wanaumwa ugonjwa unaofanana.

Nimefatilia Sana katika familia zetu kujua Kama kuna mtu amewahi kupitia hali Kama hii sijafanikiwa kupata majibu.

Baada ya yote haya nimeamua nisafiri nimpeleke hosptali inaitwa milembe ipo Dodoma nimpeleke Mama na mtoto wawafanyie uchunguzi.

Wakuu naumia Sana Kazi haziendi mtaji umekata .

Ikiwa kuna wadau wanaweza nisaidia 400K nikapata nauli na kumsafirisha huyu Mama na binti yetu nitashukuru , Endapo nikifika Dodoma gharama zikahitajika zaidi nafikiria pia kuuza kiwanja ambacho nilikinunua Kwa ajili ya ujenzi.

Mrejesho

Wakuu nashukuru Kwa ushauri wenu mpaka sasa niseme nitaufanyia Kazi kadri nitakavyojaliwa.

Pia nimeona nianze na hii hatua ya maandalizi ya kumpeleka mgonjwa Dodoma yeye na Binti yetu pale Milembe , nitafanya huduma za hosptalini Ila pia sitoacha kumuombea kila siku.

Ikiwa unataka kuwasiliana na Mimi au Kwa chochote Ni-PM.

Pia nina kiwanja Heka moja ni kiwanja kipo katika muundo wa shamba ninakiuza ili pia kinisaidie katika hiki kipindi .

Gharama ya kiwanja ni maelewano kipo Katoro Bukoba Vijijini (Kagera)

Mungu awabariki nyote.🙏🏽
Watu 1000 tukikuchangia 1000 unapata MILION Moja ongea na Mshana alikandalasi hili suala mara moja
 
Kama Umesha Wahi Kukutana Na Mtu Mwenye Matatizo Utamtambua Kwa Jambo Dogo Tu

Mtu Anajitokeza Na Kutaka Kukupa Msaada Tena Bure Na Wewe Unakataa Jua Kabisa Huyo Mtu Haitaji Msaada Ukiona Mtu Anahitaji Msaada Alafu Yeye Ndo Anapanga Masharti Ya Jinsi Ya Kusaidiwa Huyo Sio Muhitaji.

Huyu Mleta Mada Ana Shida Ya Michango Ya Pesa Hicho Ndo Anachokihitaji Ila Sio Kutatua Tatizo Linalomkumbu La kuuguliwa Na Wana Familia.
Halafu hasemi anapoishi.
 
Unangaika mkuu ndio maana nimekuuliza mbona haujawahi kumdai mtu uthibitisho wa wazazi wake kama kweli ni wazazi wake waliyomzaa ukaniambie mie ndio nifanye hivyo kwa maana wewe unangaika na habari za uwepo wa Mungu na majini ila madai mengine yasio na uthibitisho huangaiki nayo kudai uthibitisho wake.

Hakuna aliyekushikia bunduki wala kukunyima haki zako za msingi kwa kukulazimisha kukubali uwepo wa Mungu, sasa mtu akisema Mungu yupo kiuhakika wewe unapungukiwa nini? Potezea kama unavyopotezea madai mengine yasio na uthibitisho, mbona simple wala usingekuwa unabishana na watu.
Sitapotezea mkuu 😁
 
Athibitishe ili iweje ili akuridhishe wewe? Vitu vyengine havina hata maana.
Hili ni jukwaa huru nina haki ya kuhoji chochote bila matusi ndio maana unaona sijawahi kupigwa ban🤣🤣🤣😅
 
Sitapotezea mkuu 😁
Ndio maana nasema unangaika na habari za Mungu, na hakuna mwenye kulazimika kukuthibitishia chochote kila mtu anatumia uhuru wake hakuna aliyekulazimisha ukubali uwepo wa Mungu.
 
Hili ni jukwaa huru nina haki ya kuhoji chochote bila matusi ndio maana unaona sijawahi kupigwa ban🤣🤣🤣😅
Na hakuna mwenye kulazimishwa kukujibu wala kukuthibitishia chochote kila mtu anatumia uhuru wake.
 
Ndio maana nasema unangaika na habari za Mungu, na hakuna mwenye kulazimika kukuthibitishia chochote kila mtu anatumia uhuru wake hakuna aliyekulazimisha ukubali uwepo wa Mungu.
Hata mimi sijalazimisha uthibitishe uwepo wake, wala sijakushikia bunduki kama haujui unaweza kuvunga tu
 
Wapi nimelazimisha?
Kama haulazimishi mbona haupotezei tu kama unavyopotezea mengine yasio na uthibitisho? Au haki yako wewe ni kudai madai ya uthibitisho wa uwepo wa Mungu tu ila madai mengine yasio na uthibitisho hauna haki ya kuhoji?
 
😁😁😁😁 mkuu nikisema nisikujibu nitakua nakosea?
 
Hata mimi sijalazimisha uthibitishe uwepo wake, wala sijakushikia bunduki kama haujui unaweza kuvunga tu
Hakuna huo ulazima watu kuthibitisha uwepo wa Mungu ila unapinga bado unataka uthibitishiwe unasema ni haki yako.
 
Back
Top Bottom