Familia yangu Mke na Mtoto wangu Mkubwa wamepata tatizo la Akili naomba ushauri wakuu

Waganga wapo wengi sana mkuu ila tatizo kupata mganga sahihi.
Sio Kazi Yake Jamaa Kasema Anajitolea Kumpeleka Bure Wasiwasi Wa Nini?

Ninachohofia Isije Jamaa Anataka michango Badala Ya Tiba.
 
Duh!! Pole Sana mkuu.

kama ulivyosema anzia hosptali na Endelea kumuomba Mungu .

Leo siko vzuri Ila kuna kitu kidogo Sana nitajaribu kukutumia .

Mambo ya Waganga usithubutu kwenda huko sio tu utatapeliwa Ila unaweza kuharibu kila kitu.

Nenda Hosptali na Mungu wako inatosha nothing impossible.

Nakuombea uinuke tena .
Kwa Hiyo Dr Hapa Duniani Kuna Wema Tu ? Ubaya Hamna ? Kuna Mamia Ya Watu Wamefia Hospitalini Baada ya Tiba Kushindikana Na Kuna Mamia Ya Watu Wameinukia Kwa Waganga

Kama Kuna Mungu Juwa Kwamba Pia Kuna Shetani .
 
Habari wanaJF .

Kiufupi Mimi Baba wa watoto watatu ambao wote ni wa kike.

Naishi nao pamoja na Mama yao .

Tumefanikiwa kuishi miaka 12 mpaka sasa katika ndoa yetu.

Changamoto kubwa ambayo ninaipitia ni hii hapa.

Mimi kazi yangu kubwa ambayo huwa nafanya ni kuuza mazao , kuku wa kienyeji huwa naenda kijijini naangalia bei ndogo ya bidhaa Kama mahindi au kuku nanunua na kuja kuuza mjini.

Kiufupi Mimi ni mjasiriamali wa kiwango cha chini ambaye bado napambana.

Jambo Ambalo limenifanya nije ni changamoto iliyompata mke wangu na watoto.

Familia yangu ilikuwa vizuri Ila ilianza kuingia changamoto ambazo zimeniumiza Sana Akili na kunipa mawazo.

Mwezi wa kumi Mke wangu alianza kuumwa kawaida kabisa nikampeleka hosptali kumpima ikaonekana hana tatizo .

Ila nikikaa nae usiku halali anaongea mambo Kama ya kuchizika Anapasua vitu ndani .

Sasa nikaona hii hali itakuwa mbaya nimempeleka hosptali zote za mkoa Government na private Ila tatizo lipo pale pale .

Napoandika hapa mke wangu amefungiwa ndani , sasa hii hali Kama ya Mke wangu imeanza kumungia mtoto wangu wa kwanza Ana umri wa miaka 10 anaongea peke yake anaharibu vitu ndani .

Akikaa kidogo na wadogo zake wanapigwa kipigo kikali Sana hivyo mtoto na mama yao ambaye ni mke wangu ni Kama wanaumwa ugonjwa unaofanana.

Nimefatilia Sana katika familia zetu kujua Kama kuna mtu amewahi kupitia hali Kama hii sijafanikiwa kupata majibu.

Baada ya yote haya nimeamua nisafiri nimpeleke hosptali inaitwa milembe ipo Dodoma nimpeleke Mama na mtoto wawafanyie uchunguzi.

Wakuu naumia Sana Kazi haziendi mtaji umekata .

Ikiwa kuna wadau wanaweza nisaidia 400K nikapata nauli na kumsafirisha huyu Mama na binti yetu nitashukuru , Endapo nikifika Dodoma gharama zikahitajika zaidi nafikiria pia kuuza kiwanja ambacho nilikinunua Kwa ajili ya ujenzi.

Mrejesho

Wakuu nashukuru Kwa ushauri wenu mpaka sasa niseme nitaufanyia Kazi kadri nitakavyojaliwa.

Pia nimeona nianze na hii hatua ya maandalizi ya kumpeleka mgonjwa Dodoma yeye na Binti yetu pale Milembe , nitafanya huduma za hosptalini Ila pia sitoacha kumuombea kila siku.

Ikiwa unataka kuwasiliana na Mimi au Kwa chochote Ni-PM.

Pia nina kiwanja Heka moja ni kiwanja kipo katika muundo wa shamba ninakiuza ili pia kinisaidie katika hiki kipindi .

Gharama ya kiwanja ni maelewano kipo Katoro Bukoba Vijijini (Kagera)

Mungu awabariki nyote.🙏🏽
Pole sanaa kwa changamoto hiyo
 
Sasa atajuaje kama ni wa wizi
Wafanya biashara wengi/wote kutokea mijini wanakuwa na wenyeji vijijini pengine ni kabla au baada ya kuanza biashara. Ndio sehemu ambayo hufikia akitoka mjini, kupitia hao anaweza kujua.

Ila tumpe pole sana anapita katika kipindi kigumu.
 
Nilichomgundua Mleta Mada Hana Changamoto Yoyote Isipokuwa Ana Shida Ya Michango Njia Alizopewa Na Wadau Hazitaki Ana Ng'ang'ana Na Milembe Sasa Kama Alikuwa Anataka Kumpeleka Milembe Angeenda Moja Kwa Moja Kwamba Anahitaji Pesa Ila Hapa Amejaribu Kuzunguuuka.

Muhuni huyo! Mtoto na Mama wa napata kicha kinachofanana, huwezi ona kuna shida hapo?
 
Maisha safari ndefu sana mwanangu
huwa nayakumbuka maneno haya siku zote alinambia mama Yangu

pole mkuu kwa mitihani
 
Hiyo depression wanapitia Wana familia yako,,,,milembe Dodoma ni sehemu sahihi kwako,au chato hapo kuna hosp ya rufaa km sikoei, kamwone Dr bingwa wa magonjwa ya akili itakusaidia
 
Anacharge mkuu tena hela ndefu.ndugu zang flan walicharge laki ,3
Hebu waulize vizuri. Alicharge yeye au kuna watu walikuwepo hapo kati kuchukua hiyo pesa. Yaweza pia kuwa walipigwa kisha jamaa wakawasogeza kwa Mwamposa..
 
Ajabu sana.

Halafu kwa manyau wanapigwa pesa ndefu. Kwa Mungu mfano kupitia Mwamposa na wengine ninaowajua sijawahi kusikia wanalipishwa ili waombewe. Zaidi ya sadaka zao za hiari kadri walivyoguswa.

Aende kuombewa
Ubarikiwe.
 
Habari wanaJF .

Kiufupi Mimi Baba wa watoto watatu ambao wote ni wa kike.

Naishi nao pamoja na Mama yao .

Tumefanikiwa kuishi miaka 12 mpaka sasa katika ndoa yetu.

Changamoto kubwa ambayo ninaipitia ni hii hapa.

Mimi kazi yangu kubwa ambayo huwa nafanya ni kuuza mazao , kuku wa kienyeji huwa naenda kijijini naangalia bei ndogo ya bidhaa Kama mahindi au kuku nanunua na kuja kuuza mjini.

Kiufupi Mimi ni mjasiriamali wa kiwango cha chini ambaye bado napambana.

Jambo Ambalo limenifanya nije ni changamoto iliyompata mke wangu na watoto.

Familia yangu ilikuwa vizuri Ila ilianza kuingia changamoto ambazo zimeniumiza Sana Akili na kunipa mawazo.

Mwezi wa kumi Mke wangu alianza kuumwa kawaida kabisa nikampeleka hosptali kumpima ikaonekana hana tatizo .

Ila nikikaa nae usiku halali anaongea mambo Kama ya kuchizika Anapasua vitu ndani .

Sasa nikaona hii hali itakuwa mbaya nimempeleka hosptali zote za mkoa Government na private Ila tatizo lipo pale pale .

Napoandika hapa mke wangu amefungiwa ndani , sasa hii hali Kama ya Mke wangu imeanza kumungia mtoto wangu wa kwanza Ana umri wa miaka 10 anaongea peke yake anaharibu vitu ndani .

Akikaa kidogo na wadogo zake wanapigwa kipigo kikali Sana hivyo mtoto na mama yao ambaye ni mke wangu ni Kama wanaumwa ugonjwa unaofanana.

Nimefatilia Sana katika familia zetu kujua Kama kuna mtu amewahi kupitia hali Kama hii sijafanikiwa kupata majibu.

Baada ya yote haya nimeamua nisafiri nimpeleke hosptali inaitwa milembe ipo Dodoma nimpeleke Mama na mtoto wawafanyie uchunguzi.

Wakuu naumia Sana Kazi haziendi mtaji umekata .

Ikiwa kuna wadau wanaweza nisaidia 400K nikapata nauli na kumsafirisha huyu Mama na binti yetu nitashukuru , Endapo nikifika Dodoma gharama zikahitajika zaidi nafikiria pia kuuza kiwanja ambacho nilikinunua Kwa ajili ya ujenzi.

Mrejesho

Wakuu nashukuru Kwa ushauri wenu mpaka sasa niseme nitaufanyia Kazi kadri nitakavyojaliwa.

Pia nimeona nianze na hii hatua ya maandalizi ya kumpeleka mgonjwa Dodoma yeye na Binti yetu pale Milembe , nitafanya huduma za hosptalini Ila pia sitoacha kumuombea kila siku.

Ikiwa unataka kuwasiliana na Mimi au Kwa chochote Ni-PM.

Pia nina kiwanja Heka moja ni kiwanja kipo katika muundo wa shamba ninakiuza ili pia kinisaidie katika hiki kipindi .

Gharama ya kiwanja ni maelewano kipo Katoro Bukoba Vijijini (Kagera)

Mungu awabariki nyote.🙏🏽
Kama inawezekana hapo ulipo
Hama mkoa, tafuta nyumba ya kupanga.
Kuna mambo kama unachukulia poa, utajikuta unatumia pesa nyingi sana. Kama una wazee nyumbani washirikishe
 
Back
Top Bottom