FAMILY MATTER: Nahitaji ushauri, nashindwa kufanya maamuzi...

FAMILY MATTER: Nahitaji ushauri, nashindwa kufanya maamuzi...

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
772
Reaction score
2,421
Karibuni mnisaidie ushauri maana nipo njia panda....


Mwaka 2009 baada ya kumaliza kidato cha nne kijijini katika shule moja ya kata huko kanda ya ziwa, nilipata mwaliko kutoka kwa baba yangu mdogo anaeishi DSM alinitaka nikatembee na kubadili mazingira. Mwaliko ule ulikuwa ni kitu nilichokifurahia sana ukizingatia kuwa nilikuwa nimekaa kijijini pale kwa zaidi ya miaka 10 baada ya baba angu kuhamishiwa kikazi akitoka mkoa mmoja wa nyanda za juu kusini magharibi. Hivyo fursa ya kuja DSM ilikuwa ni ya kipekee na niliisubili sana hiyo siku ifike. Kweli, tarehe ilifika na nikaondoka kuja DSM kwa baba mdogo. Naomba nimuite Uncle katika story hii.

January 2010 ilikuwa ndio kwa mara ya kwanza nawasili jijini Dsm. Maisha ya dsm kwa uncle yalikuwa poa sana, niliendelea kuenjoy maisha na kusafisha macho huku nikisubiri matokeo yangu ya kidato cha nne. Muda ulienda kasi na mnamo mwezi wa pili mwaka ule matokeo yalitoka na kwa bahati mbaya sikuwa nimebahatika kufaulu. Niliumia sana na ukizingatia nilikuwa najitahidi kusoma kwa bidii. Wazazi wangu kule kijijini kanda ya ziwa walinitia moyo na nikakubaliana na hali halisi. Sikuwa na kitu kingine cha kusubiri pale Dsm maana kama kukaa nimekaa sana na nimeshafeli, sina uelekeo na sijui itakuwaje, hivyo nilianza maandalizi ya kujiandaa na safari ya kurudi kijijini kwetu ambako hata hivyo sikujua nini kingekuwa hatima ya maisha yangu. Nilipoteza kabisa uelekeo hivyo sikuwa na budi kwenda kadri ya vile upepo ungenipeleka.

Kama ilivyokawaida, nilipanga kumuaga uncle kuwa mimi narudi kijijini ila kabla sijapata nafasi ya kumuaga, siku moja usiku mida ya saa 7 usiku tukiwa tunaangalia Tv na kuzungumza mambo mbalimbali, uncle aliniambia sipaswi kurudi kijijini bali anampango wa kunitafutia shule jijini dsm ili nirudie masomo yangu. Uncle alisema kuwa ameona nina kitu ndani yangu na bado ana imani namimi licha ya matokeo yangu mabovu niliyokuwa nimeyapata ambayo hayakufaa hata kusomea ualimu wa primary kwa wakati ule. Uncle aliamini kuwa bado nina uwezo na ataongea na mshua wangu ili ajiandae kunilipia ada kwenye shule ya private huku jijini. Ndani ya moyo wangu nilifurahi sana, kwanza sikupenda kurudi kijijini japo nilikuwa nishaanza kujiandaa kurudi maana trend ya kijijini kwetu kwa vijana wanaomaliza shule huwa wanaishia kwenye ulevi wa pombe na ugoro. Mazingira ya kijijini kwetu hayavutii hata kwa uwekezaji, mzunguko wa pesa ni hafifu sana. Nilifurahi sana moyoni kwa kupata fursa ya kubaki mjini. Kitu pekee kilichonitia hofu ni swala la shule, uncle ameniamini ila je sitamuangusha? ikizingatiwa ilibidi nirudie masomo yote ili kusafisha cheti..Niliwaza sana ila nilijipa moyo kuwa itawezekana.

Hatimae march 2010 nilianza masomo kama private candidate katika shule moja maarufu hapa jijini iliyopendekezwa na Uncle wangu (Baba angu mdogo ambae ni mdogo wake na baba). Usimamizi wangu ulikuwa chini ya uncle na gharama zote za shule zilikuwa chini ya baba angu. Na mwezi march huo huo, nilihama kwa uncle wangu na kuhamia kwa shangazi yangu (mdogo wake na baba) ambae nae anaishi hapahapa dsm aliniomba niksihi kwake kwani alikuwa anakaa peke yake katika nyumba kubwa. Hivyo nilimuaga Uncle (baba mdogo) ambae nae bila hiyana aliniruhusu nikakae kwa dada yake. Maisha ya shule yaliendelea poa, nilijitambua, nikasoma kwa bidii na baba mdogo alinipa vitabu vingi sana na muhimu ili tu nisihangaike na nifanye vizuri..Na mwezi octoba 2010 nilimaliza kidato cha nne kama private candidate na matokeo yangu yalikuwa makubwa sana sana sana. Nilifanikiwa kupata ufaulu mkubwa tena kwa asilimia 100% (nilifaulu masomo yote). Ilikuwa ni furaha sana kwangu mimi, kwa familia yangu, uncle pamoja na shangazi.
NB: Hapa napenda nimpe moyo kijana yeyote anaerudia masomo sasa hivi, INAWEZEKANA na pia nimshukuru kwa dhati uncle wangu, aliyeniamini toka mara ya kwanza nilipofeli..

Tuendelee na uzi...........

Baada ya hapo 2011 - 2013 niliendelea na masomo ya kidato cha sita nikiwa chini ya usimamizi wa uncle wangu na gharama zote zikiwa chini ya mzee wangu. Na mda wote huu bado niliishi kwa shangazi yangu kama nilivyomueleza hapo juu. Matokeo ya kidato cha nne yalinipa confidence na sasa nilipambana sana kwa kujiamini ili nifanye vizuri na kuzidi kumfurahisa uncle wangu na wazazi wangu. This time nilichukua masomo ya biashara, EGM, na mapambano yaliendelea. Kipindi chote hicho niliishi vyema na uncle pamoja na aunt. Naomba nikiri wazi kuwa uncle wangu ni mtu mwenye roho nzuri sana, alinilea kwa moyo mmoja na kwa upendo mkubwa yeye pamoja na mama mdogo (mke wake). Hivyo maisha yangu ya advance nikiwa kama school candidate katika shule ile ile yalikuwa ni mazuri na yasiyosahaulika. February 2013 nilimaliza kidato cha 6 na kama maajabu, nilikuwa ni mwanafunzi mwenye ufaulu mkubwa kwa kidato cha sita katika ile shule kwa mwaka ule na sasa nilikuwa naenda kujiunga na masomo ya chuo kikuu.. Maono ya uncle juu yangu nilikuwa nimeitimiza, na sasa nilikuwa naingia sehemu ambayo nilikuwa sina matumaini ya kuingia tena miaka 3 nyuma, Chuo kikuu. From being a reseater in 2010 to the best Form six student at my school in 2013.
Sisemi ufaulu wangu wa shule kwajili ya kuji proud hapana, bali kwajili ya kumtia moyo kijana yoyote ambae ndoto zake za shule zimepitia vikwazo kama vyangu. Napia ili kuweka wazi kila kitu na mchango wa kila mtu katika maisha yangu ili ndugu msomaji uwe katika angle nzuri ya kunishauri au kunikosoa mwisho wa hii story.

Baada ya kumaliza kidato cha 6, maisha yaliendelea kama akawaida, matokeo ya maombi ya chuo yalitoka na nilikuwa nimechaguliwa kujiunga na Chuo kikuu cha DSM. Hii ilikuwa ni furaha kubwa sana kwangu, kujiunga na hiki chuo ambacho siku zote kilikuwa ndani ya moyo wangu. Na hapa sasa nilikuwa naamini kabisa kuwa naukaribia mlango wa mafanikio yangu kimaisha ili niwe faraja kwa ndugu zangu, jamaa na marafiki. Ila katika hali nisiyokuwa nimeitarajia kabisa, uhusiano wangu na Uncle ulitetereka kwa kiwango kikubwa sana.

Nilikuwa nimeingia katika mgogoro baridi na uncle. Nauita mgogoro baridi kwasababu ni sisi wawili tu (mimi na uncle) ndiyo tuliojua kinachoendelea kati yetu. Ni mgogoro baridi mpaka hapa kwasababu impact yake ilikuwa bado haijaanza kugusa maisha ya wengine. Kutoka kuwa marafiki wa wakubwa, sasa tulikuwa maadui, kutoka kuwa mfano bora kwa uncle na kama reference ambayo alikuwa anaitumia katika kuelezea vijana bora, sasa niligeuka kuwa kijana mhuni, na mtu nisiyefaa. 'Ugomvi' wetu ulikuja kwa ghafla sana ila ndiyo hivyo sasa mambo yalikuwa yamebadilika na rafiki yangu mkubwa au mtu aliyebadili maisha yangu alikuwa hana maelewano mazuri namimi..Ni ngumu kukabiliana na situation kama hii hasa kwa mtu ambae amehusika kurudisha tumaini lililopotea kwenye maisha yako. Sikuwa na jinsi, Maisha ilibidi yaendeleee...........


NB: Kwasababu nahitaji ushauri, hivyo ningependa kuandika na kuweka wazi kila kitu ili tu nikosolewe au nishauriwe vile inavyotakiwa. Naomba radhi kwa wanaochukia story ndefu. Hii sio hadithi ya kutunga bali na ukweli halisi wa kitu kilichotokea hadi leo hii nakuwa njia panda. Nitatuma muendelezo nikipata nafasi.

 
Kaka umeshindwa kumaliza story sisi tukusaidiaje? hapo umefanya introduction tu hatuelewi kiini cha mgogoro.......wewe pambana na hali yako jombaaa
 
Enhee, nawe umeanza mambo ya itaendelea......

Kama unaomba ushauri jitahidi sana uweke bandiko zima kwenye part moja, unaombaje ushauri kwa kuweka parts kibao utadhani hadithi/simulizi?
Unforgetable
 
Vipi huu mgogoro wako baridi ndio ulisababisha kifo cha ma mdogo wako nini? Maana kwenye huu uzi wako ulisema ma mdogo alifariki ukiwa mwaka wa mwisho.


 
Siku hizi imeshakuwa fashion kutuletea story nusunusu humu.
 
Vipi huu mgogoro wako baridi ndio ulisababisha kifo cha ma mdogo wako nini? Maana kwenye huu uzi wako ulisema ma mdogo alifariki ukiwa mwaka wa mwisho.


hapana mkuu..kwenye hiyo story uliyotag, aliyefariki ni aunt yangu..ni mwingine wala hausiani na hii thread.
 
Back
Top Bottom