FAMILY MATTER: Nahitaji ushauri, nashindwa kufanya maamuzi...

FAMILY MATTER: Nahitaji ushauri, nashindwa kufanya maamuzi...

Nilichogundua ni kuwa ukoo wa upande wa baba yako ni moja ya koo hapa nchini unaoongeza ma CHIZI FRESH TANZANIA ushauri wangu ni kuwa acha kurithi adui coz adui wa baba yako sio lazima awe adui yako hivyo umtembelee ama usimtembelee huyo anko wako hakuongezi point yoyote kwenye maisha yako so jikite kwenye kutafuta pesa na kuimarisha maisha yako hicho ndicho kitakupa power kwenye kuwaunganisha hao wehu wawili(baba yako na uncle) Nasema hivyo kwa sababu ukiwaita wawili huku huna hela wataona kama unawapigia kelele ila ukiwaita huku una maisha safi watakuja huku wamefyata mikia na watakuona unaongea point.TRUST ME NILIKUWA NAONEKANA MWEHU NA NIMEPOTEZA DIRA NIKATENGWA NA UKOO MZIMA LEO HII MEMBERS OF THE CLAN WANAJIRUDI KWA KUPIGA MAGOTI KWANGU BAADA YA KUKOMAA NA MAISHA NA KUJIWEZA KIMAISHA
 
We bwana nenda kwa uncle hilo lipo wazi labda kama unatuchora tu hapa.
 
Hivi maisha yalivyo tight namna hii..muda wa kuwana beef mnatoa wapi?
 
Nilichogundua ni kuwa ukoo wa upande wa baba yako ni moja ya koo hapa nchini unaoongeza ma CHIZI FRESH TANZANIA ushauri wangu ni kuwa acha kurithi adui coz adui wa baba yako sio lazima awe adui yako hivyo umtembelee ama usimtembelee huyo anko wako hakuongezi point yoyote kwenye maisha yako so jikite kwenye kutafuta pesa na kuimarisha maisha yako hicho ndicho kitakupa power kwenye kuwaunganisha hao wehu wawili(baba yako na uncle) Nasema hivyo kwa sababu ukiwaita wawili huku huna hela wataona kama unawapigia kelele ila ukiwaita huku una maisha safi watakuja huku wamefyata mikia na watakuona unaongea point.TRUST ME NILIKUWA NAONEKANA MWEHU NA NIMEPOTEZA DIRA NIKATENGWA NA UKOO MZIMA LEO HII MEMBERS OF THE CLAN WANAJIRUDI KWA KUPIGA MAGOTI KWANGU BAADA YA KUKOMAA NA MAISHA NA KUJIWEZA KIMAISHA
Ushauri mzuri ila kuwaita wehu nimekumaind sana mkuu...Sitaki nikujibu vibaya ila we ni mtu mzima na story zako humu zina onesha kuwa una exposure.. Tumia busara mbona simple tu...shukrani.
 
Naona tatizo lipo kwako.
Hutaki kujishusha.

Kama ungejifunza kujishusha hata huo mgogoro usingetokea tangu mwanzo.

Na sasa bado unafikiria namna ya kujishusha,ukijishusha unaenda hutapungukiwa chochote.

Be humble
I agree mkuu...nimekuelewa sana.
 
Cut the crap....
Kumbuka wew kwa kiwango chake umechangia uncle na baba kuchukiana.
Afu sizani km reason zako za kutompigia simu uncle zina mashiko such a lame reason kwamba uncle hana weekend!?
Ungepiga akukatie
Waache wao wachukiane usiwe part ya ugomvi wao nenda kwa uncle wako kasalimie ikibidi uombe na msamaha kabisa then ona jinsi vitu zitakua.
 
𝕄𝕜𝕦𝕦 𝕨𝕖𝕨 𝕟𝕖𝕟𝕕𝕒 𝕤𝕒𝕓𝕒𝕓𝕦 𝕙𝕒𝕦𝕟𝕒 .... ℂ𝕙𝕒𝕟𝕫𝕠 𝕔𝕙𝕒 𝕙𝕦𝕠 𝕞𝕘𝕠𝕘𝕠𝕣𝕠 𝕨𝕒𝕠

ℙ𝕚𝕒 𝕨𝕨 𝕟𝕕𝕠 𝕦𝕟𝕒𝕨𝕖𝕫𝕒 𝕜𝕦𝕨𝕒 𝕤𝕦𝕝𝕦𝕙𝕚𝕤𝕙𝕠 𝕝𝕒 𝕙𝕦𝕠 𝕞𝕘𝕠𝕘𝕠𝕣𝕠 𝕤𝕠 𝕟𝕖𝕟𝕕𝕒
 
asante mkuu..ila sio kwamba sipendi kujishusha na sio kwamba sikuweza kumpigia simu...Uncle wangu ni nature ya watu wenye hasira sana..Mara mia ni bora kukaa kimya kuliko kumhoji, so sikutaka kuingia kwenye hot war nayeye na nikaamua kukaa kimya..maana kwa jinsi ninavyomjua, sauti yangu ingeleta maafa makubwa sana..ila asante kwa ushauri.
Ulitakiwa mwanzoni mwa tuhuma ungempigia simu anko na kuclear but inaonyesha huna moyo wa unyenyekevu na kujishusha. Sasa anko amekualika kwa heshima usipoenda ataona umemdharau na una kinyongo. Nakuomba uende tena wiki hii isiishe na vile vile rudisha ukaribu na anko wako. Pia wewe utafanyika daraja la kuwapatanisha baba na anko
 
Upendo hauhesabu makosa, samehe na uende ukamsalimia, yake na kaka yake (baba yako) yatabakia kuwa yao wenyewe, na iko siku yataisha pia mana ugomvi kwenye familia ni kitu cha kawaida, ila wewe cheza nafasi yako for ur own sake, mlango wa amani umeshafunguka ila kwa kuwa shetani hapendi atapitisha kichwani mwako kila wazo negative na douts zooote alimradi kuua ile amani ambayo imeshaanza kujitokeza, usimpe nafasi, na pia muombe Mungu.
 
Kama mwanamme mwenye uelewe, nenda kwake na ujenge urafiki wa baba na mtoto na unaweza kuwa chanzo cha wao kuwapatanisha.
 
Ushauri mzuri ila kuwaita wehu nimekumaind sana mkuu...Sitaki nikujibu vibaya ila we ni mtu mzima na story zako humu zina onesha kuwa una exposure.. Tumia busara mbona simple tu...shukrani.
Sorry Fohadi nilicoment nikiwa BAR naomba upokee ushauri wangu bila kuweka hayo maneno mabaya kwako
 
Mkuu nenda kamtembelee anko tusipende kurithi kurithi magomvi yasiyotuhusu,tena wewe unaweza kuwa chanzo cha kuwapatanisha hao wazee bila kutarajia cha kufanya tafuta siku moja unayojua anko yupo nyumbani pita mahali wanunulie mazagazaga ya kutosha nenda kamsalimie uone utakavyopokelewa kifalme.
 
Ukoo wenu una wachawi au washirikina wabaya sana....

Anko wako ni either kalogwa asipatane na wewe ili wewe usifike mbali AU alikuwa anataka kukutoa kafara kakushindwa
Nakubaliana na hili kuna nguvu ya kishirikina
 
Back
Top Bottom