Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Wazo liko vizuri mkuu, tatizo ni maandalizi na maandalizi ni hela mtaji wa kufanya hivyo, bila mtaji wa kutosha unarudi mtaani mapema tu, Huyu mwenye mtaji wa ndoo moja mbili anafanyaje?
 
Mwisho utatuambia tufuge kuku wenyewe ili tuwe tunapata mayai yakukaangia chips.

Mwisho utatuambia tuchome mkaa porini ili tupate mkaa wakupikia ubwabwa wakuuza.

Mwisho utatuambia tukalime viazi kwaajili ya kupikia chips.

Mwisho utawashauri na walevi wawe wananunua pombe kwa jumla.
 
Mkuu hii kudeal na mambo mengi unaweza kujichanganya mwenyewe.
Naamini kila biashara ina faida yake unapoifanya lakini pia kuna faida nyingi tu za kuspecialize kwenye kimoja ili kufanya vizuri kumudu ushindani.

Wewe uuze sabuni uuze mkaa na uwe na mgahawa tena katika eneo moja.
Baadhi ya wateja watakukimbia mazingira yako hayatakuwa masafi.
 
Kwenye biashara kuna mambo mengi sana ambayo kabla hujafikiria kuanzisha biashara unatakiwa kuyafikiria ili isije tokea sababu yyte (ya kibinadamu) ikakuangusha chini ukafunga biashara yako.

Watu wengi sana kabla ya kuanzisha biashara zetu tunajiuliza "tutapata wapi bidhaa tunazotaka kuziuza"? kila mtu hupata jibu zuri ambalo humpa nguvu ya kuanzisha biashara yake na mwisho anachukua pesa yake anafata bidhaa tayari kuipeleka kwa mtumiaji wa mwisho (mteja).

Baada ya kufungua biashara kuna wenye bahati biashara zinaendelea,kuna wale wenzangu namimi hesabu hawakupga vizuri wanafeli na mwisho hukimbilia kusema biashara flani hailipi au haina faida. (jambo ambalo si kweli)

Leo nataka niwafungue macho wale wanaopeleka pesa kwa jirani wakati wanachoenda kukinunua uwezo wakukipata wanao, katika biashara usipokua na akili ukaamini biashara ni pesa tu umeumia. Hivi mfano unafuga kuku wa mayai nyumbani kwako halafu ukitaka mayai unaenda kununua kwa jirani au dukani,hivi hiyo ni akili au ni kitu gani?

Twende kwenye mifano ili tuelewane naongelea nini...Point yangu ni kumsaidia mfanyabiashara kuongeza faida ktk biashara anayofanya ili asije mtafuta mchawi badae.

Biashara ya CHIPS

Kuna watu mnafanya hii biashara sasa mna muda mrefu na wengine ni mnauza hadi gunia 3,4 mpk 5 kwa siku hizo ni chips tu mtu anauza,pia kuna wale wenzangu wa ndoo 1,2 mpk 3 na kuendelea. Lengo la hiii biashara ni kuuza chips tu,lakini swali ni huyu mtu anapata wapi viazi vya chips? au anapata wapi mayai? jibu analo.

Acha niongee na hawa wa ndoo 1,2 mpk 3, unapoanza kuuza chips viazi vikiisha unakimbilia kuongeza vingine,vkiisha unafata tena bei ya ndoo reja reja unanunua ndoo 20,000 kwa siku unaweza kununua ndoo mbili mpk 3,kumbuka unapoenda kununua ndooo kwa 20,000 yule anaekuuzia amepata faida Tufanye kila ndoo anapata faida 2000,wewe kwa siku unaenda nunua ndoo mpk 3 ina maana kwa siku unampa faida ya 6000.

Hivi viazi unakuja kuviuza unapata pesa ndio "sikatai" lakini kwanini hujiongezi kila siku unapoteza 6000 na saa zingine ukute mpk na nauli utatumia kufata hivyo viazi ina maana kuna zaidi ya 7000 unaipoteza kila siku unapoingia kazini "bila wewe kujua".

Ufanyeje sasa? unajua biashara yoyote si lazima uanze na mtaji mkubwa,ni kwanini usinunue gunia 1 ukalimwaga hapo pembeni mwa biashara yako ukawa unauza na viazi? ukapanga ndoo kubwa,ndogo,visado,nk ukawa unauza hapo lengo ni kuokoa zile 7000 tunazopoteza kwahyo Mteja no.1 wa biashara yako ya viazi ni wewe mwenyewe, akitokea mpita njia akataka viazi hewalaaaah,wakitokea majirani wakata uwauzie viazi hewalaaaah na uzuri wasipotokea hao wote pia Hewalaaaah kwasababu tulifungua hii biashara si kwa ajili yao ila tulifungua kwa ajili yetu wenyewe,maana yake unakua mteja mkuu ktk biashara yako wewe mwenyewe.

Hutoenda kununua viazi kwa jirani tena,utaokoa zile 2000 alizokua anakupga kwa kila ndooo na sasa utakua umejiongezea wewe faida utapata faida ya chipsi utapata faida ya viazi pia,Hivi utalalamika biashara mbaya kweli? sidhani kwasababu ikitokea chipsi zimegoma Viazi vitakupush,chpsi zikienda na viazi vyako vinaenda,Huko ndio kufanya biashara ndani ya biashara yako.

Mayai
nayo umeshajiona kwa siku unatumia trei mpk 10 za mayai lakini ajabu n kwamba unanunua trei 1 kwa mangi sh 7000,sawa unapata faida lakini kwanini usiuze nawewe mayai kwa jumla kama mangi? yeye anayatoa wapi ushindwe wewe kuyapata? kila trei mangi anapata faida 1000 wewe kwa siku unatumia trei mpk 10 ina maana unampa mangi faida 10,000 kila siku kwenye mayai,Wakati ulikua na uwezo wa kwenda kwa wafugaji ukamwambia unahtaji mayai kwa jumla,Ukanunua ukaja yaweka Ofisini kwako,Ukawa unajiuzia mwenyewe lakini pia utaweka tangazo kuwa unauza mayai kwa jumla na wewe.kwahyo utajikuta unaokoa zile 10k ulizokua unampelekea mangi kwenye mayai lakini zaidi sasa utajiongezea wateja wengine wa mayai utapga huku na kule,hivi biashara itakushnda kweli?

Biashara ya Vinywaji/Pub
Kuna watu wanafanya biashara za vinywaji siku hizi wanaita "cha kupima" mteja anakuja unampimia konyagi anajimiminia anasepa zake,huyu mtu kwasiku anaweza uza mizinga mikubwa ya konyagi mpk mizinga 5 - 8 (biashara ikiwa nzuri) lakini ajabu ni kwamba ananunua mzinga mmoja mmoja ukiiisha anafata mzinga mwingine,anaenda hivyo hivyo,Mzinga 1 wa konyagi ni 8000 ina mana kwa siku akinunua mizinga 7 anakua katumia 56,000, sawa hamna shida Faida unapata,umeshajua konyagi zinatoka kuliko kinywaji kingine "kwanini usinunue konyagi katoni zako ukawa unauza nawewe"? katoni ya konyagi ni 90,000 zinakaaa bapa 12.

Ukinunua kila bapa kwa 8000 ina maana kwa 12 n sawa umenunua katon kwa 96,000 wakati JUMLA katoni ni 90,000 ina maana kila siku unampelekea mwenzako faida ya 6000 (si unanunua kwa moja moja) huwezi ona kwasababu hupgi hesabu, sasa kwanini usijikakamue ukaenda kunua Katon yako nzimaa ukaileta dukani kwako/kibandani kisha ukaandika na katangazo kuwa unauza BAPA jumla na REJA REJA, unafkiri htouza? sio kila mtu anapenda za kupima kuna siku huyo mteja wa cha kupima anaziotea pesa anatamani kununua BAPA unamtandika bei 9000 au hata 10,000 unajipatia Pesa yako, lakini hata huyo mteja asiponunua,Utanunua mwenyewe "kumbuka tunafanya hivi ili kuokoa pesa tunayoipoteza kila siku.

Mama Ntilie unapofanya biashara yyte angalia matumizi yako makubwa yapo kwenye kitu gani,kisha angalia namna ya kufanya kukabiliana na hayo matumizi maana siku zote faida hupotea kwenye matumizi,usipo weza dhibiti matumizi hutoweza kupata faida wanayopata wenzako.

Mama ntilie matumizi yake makubwa ni kwenye Mkaa,yani hakuna mahali panamaliza pesa kwenye biashara ya chakula kama MOTO kwakua mama ntilie wengi wanalijua hilo ila vichwa vyao n vigumu anashndwa jiongeza.

Ukifanya mama ntilie au biashara ya chakula ni lazima lazima uuze Mkaaa na Sabuni za unga za kupima kila siku unatumia mkaa wa 8000 - 10000 kila siku kwa ajili ya kupikia,hivi unajua Kama unanunua mkaa wa 10,000 kwa mwezi n sawa umetumia mkaa wa 300,000? unajua bei ya gunia la mkaa? gunia la mkaa ni 150,000 tena ni gunia lenye ujazo heavy weight MC kwanini usinunue gunia 1 tu kisha ukapanga mkaa wako hapo nnje ukauzia wateja wengine,wafanyabiashara wenzako lakini hata ikitokea hajaja mtu utaweza Kujiuzia mwenyewe.

Ina mana utakua unaokoa pesa nyingi sana uliyokua ukiipoteza kwenye mkaaaa lakin pia utajiongezea faida kwasababu huwezi niambia wiki nzima akosekane mtu wakununua ule mkaa uliopanga pale nnje. Hii maana yake faida utakayopata kwenye mkaa + chakula = Tabasamu usoni mwako

Kuna wale wenzangu wa jikoni watumia GAS,amenunua kamtungi kake kadogo anakatumia ndani ya siku 4 kamaliza anaenda nunua mwingine,hivi kwanini usiuze gas? Shida ni kwamba mtu anafkiri kufanya biashara ya gas au chochote n lazima uanze na vitu vingi,Jambo ambalo si kweli. Mtungi mdogo gas ni 20,000 sehemu zingine hadi 21,000 wakati ukisema uuze gas utanunua gas kwa 17,000 maana yake wewe ukija kuuza ukiuza 20k faida yako ni 3000.

Sasa kwasababu umeshajua gas ndio inapoteza pesa na ndio matumizi pasua kichwa,Uza gas nunua complete zako za Mitungi midogo kama unaotumia miwili tu kisha weka pale nnje Andika Gas Inauzwa HAPA halafu endelea na ratba yako ya kila siku,gas ikiisha usiende kwa mangi Nunua kwako mwenyewe ambapo utanunua kwa 17,000 (bei ya jumla) utaokoa zile 3000 ulizokua unazipeleka kwa mangi,lakini pia kuna siku atatokea mteja anataka gas Utamuuzia utapata faida tena,na uzuri n kwamba hii biashara ya gas uliifungua kwa ajili yako mwenyewe ili kuokoa pesa kupunguza matumizi kwahyo mteja wa nnje aje asije Hupasuki kichwa,akija sawa asipokuja sawa..Hiyo ndio biashara ndani ya biashara.

Sabuni ya unga ya kupima kila siku n lazima ununue sabuni ya kuoshea vyombo ya sh 1500 kipande 500 unga buku, ukpga kwe mwezi ni 45,000 wakati una uwezo wakununua mfuko wa Klee soft unauzwa 25,000 nina uhakika hata usipouza Huwezi maliza ile sabuni,na ukipima ukaweka pale nnje ukawa unauza utapata faida zaidi kutoka kwa wanunuaji,lakni hata asipotokea mnunuzi utanunua mwenyewe kwahyo ile cost ya sabuni kila siku utaiondoa lakn zaidi utajiongezea faida kwenye biashara yako,utaona matunda ya kazi yako kwasababu matumizi pasua kichwa utakua umeyaondoa.

Saloon (kiume/kike) utaratibu wetu ni ule ule kuangalia wapi ambapo ofisi inachukua matumizi mengi kuliko pengine,kwasaloon zakiume n ukweli usiopingika Poda,spiriti,pamba/sponj,nk ndio matumizi yetu makubwa, kwasababu tumeshajua hilo unajiuliza kwasiku natumia poda kopo ngapi? sprit je? ukishaona hivyo unashtuka haraka unatengeneza shelf hapo saloon kwako,Acha kufata poda kwa Mangi anakupiga asee Anakuuzia poda 1000 wakati kainunua 500 katon nzima anapata faida mpk 3000 kwani unashndwa nini kuingia duka la jumla ukachukua katoni 1 ya poda ukaja ukapanga saloon kwako ukawa unajiuzia mwenyewe na majirani zako?

Uwezo upo ni hujataka tu,spirit je unajua kidumu cha sprit cha lita 5 n sh ngapi? leo hii unanunua kichupa cha mils ngapi sjui sh 1000 tena spirit umechakachuliwa mpk tabu kwann usiwaze zaidi namna yakuokoa hizo pesa? Pamba je? uwezo wakufikiri zaidi unao ni basi umeamua kumfanya mangi kuwa best friend wako.

Saloon ya kike shampoo ndio pasua kichwa akija mteja kama mtu wangu flani humu (unajijua) unywele upo huku kiunoni,unamuosha mpk unahisi anamaliza shampoo yote peke ake maana nywele ni nyingi,lakini kila siku hukomi kununua shampoo kwa mangi kidumu 10,000 hivi utajiongeza lini? kutengeneza shampooo si mnafundishwa jamani kwenye ma group huko ya kina mama? au hata ukiingia google unaweza jifunza tengeneza shampoo ukauzia wengine na wewe mwenyewe..Trip za kwa Mangi zipunguze ndio zinazopukutisha faida yako mwsho unasema huoni faida,kumbe si kweli shda ni wewe mwenyewe....

Biashara zipo nyingi hasa hizi za kijasiriamali watu mkiweza tambua wapi mnakosea mtavuka na mtaupenda ujasiriamali sana,kuna mtu unapga nae story anakwambia PESA anapata,wateja anapata ila haoni faida ya kazi anayofanya,hana chochote anachoona amekipata kuptia kazi yake ndio mana kaamua kuacha (lazy people) nawaitaga hivyo kimoyo moyo kisha nakausha,nampa pole maisha yaendeleee.

Watu hapa washaanza kusema "haiwezekani" sawa haiwezekanii kama umeweza fungua hiyo biashara yako nakuhakikishia hushndwi fanya nilichokiandika hapa,Angalia kwenye hiyo biashara yako kitu gani kinatoka sana,kama n duka angalia n kitu gani kinatoka sana angalia kisha kilete karibu hicho kitu,Tuache kulaumu biashara flani hailipi wakati hujaziba mirija inayopoteza faida yako.

Biashara unayoifanya sasa ni nzuri kuliko unayowaza kuifanya baada ya hiyo,usiache unachokifanya Boresha Fungua puzzle hizo Utanishukuru siku 1.
Fact [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji123]
 
Msaada. Mfano mimi nauza simu na vifaa vya simu Jumla na rejareja.. Nisaidie namna gani Ntafanya biashara ndani ya biashara yangu.. Ahsante
 
Mawazo mazuri but too much theoretical. Practically inaweza ikawa ngumu kwa mtu anayeanza biashara.. mfano uuze mitungi ya gesi huku unapika utajigawaje, or uajiri mtu kwa ajili ya kuuza gesi napo gharama zitaongezeka.

Huwezi napo ukauza mtungi mmoja wa gesi lazima utanunua mitungi mingi napo mtaji lazima uwe mkubwa. Kwa mtu ambaye ana mtaji mdogo sioni Kama itamsaidia kupunguza gharama.

Maybe ungeweka mifano hai kupitia kwa kwako au kwa mtu ambaye amefanya hivyo ukaweka mahesabu ya faida aliyoipata, utakuwa umesaidia watu.
 
Daah alafu ukute wewe ndo kichwa cha familiašŸ¤”šŸ¤”
Mkuu rizki ya mtu hupita mkononi mwa mtu, wewe komaa na biashara yako tu, iboreshe zaidi na zaidi.

Ila ukitaka kufanya biashara zote lazima ukwame tu, kama juniamini jaribu hiyo uone.

Binafsi nilianzaga na biashara ya stationary nilivokuwaga chuoni (arround 2005). Nikawa nakomaa sana kukaa mwenyewe weekend ili wasinipige, yes nilikuwa napata ila nilikuwa natumia nguvu saaana.

Zilichanganya pale nilipotoka kutafuta tenda na kuzileta ofisin kwangu, hela ilikuwa inaingia moja kwa moja mfukoni, natoa comission kidogo nabaki na ziada kubwa huku nikiwa na muda wa kutosha kufanya issue nyingine.

Yaani komaa kuboresha biashara yako tu ikikua zaidi ajiri vijana wapige kazi, we endelea kusimamia vzr zaidi na kuhuisha masoko
 
Mawazo mazuri but too much theoretical.
Unahisi naandika vitu kutoka kwenye kitabu cha ujasiriamali kilichoandikwa na prof wa udsm au udom?

unatamani mifano hai,unahisi bei nilizoweka hizo chache hapo ni Halisi au nimebuni buni?

unahisi naandika copy n paste kwa unavyofikiri mkuu wangu?

Unahisi nilivyoandika hapo ni mawazo tu yakufikirika ila hayafanyiki au hayawezekaniki? si eti mkuu wangu?!

Nani alikwambia Kuuza gesi lazima uanze na mitungi mingi kama unavyosema?

Nimelenga wenye mitaji midogo ndio,ukiskia biashara ya gesi si kwamba lazima uwe na malaki ya pesa,ukisikia biashara ya viazi si lazima uwe na malaki ya pesa?

Unajua Gunia la viazi lipo la ujazo wa aina ngapi? na kila gunia 1 linauzwa kwa kiasi gani? Unahisi hilo gunia mfanyabiashara hatoweza linunua?

Ukija kwenye mkaa,unajua mkaa unawekwa kwenye magunia ya ujazo tofauti tofauti? unajua kila gunia lina bei yake tofauti? au ukiskia mtu anauza mkaa kwa jumla unatengeneza picha ya mtu mwenye stooo ya magunia 100 kwenda mbele??

Usifanye mambo kuwa magumu sana mkuuu kuna vitu huitaji kutumia nguvu nyingi sana,Neno JUMLA lisikutishe ukaliogopa, Unaweza ukawa na mtaji wa 50k na ukauza bidhaaa flani kwa jumla,inategemea na uvumilivu wako ktk hiyo biashara na malengo yako uliyojiwekea..

Natamani kukupa mifano hai ili unifahamu japo kidogo maana ulitaman mifano hai ila kwakua tuko JF tunachat kirobot robot,hilo tuliache kwasasa ila nakwambia tu kitu mkuu Usitishike na neno JUMLA ni neno la kawaida sanaaaaaaaaaaaaaa.....
 
Msaada. Mfano Mimi Nauza simu na vifaa vya simu Jumla na rejareja.. Nisaidie namna Gani Ntafanya Biashara Ndani ya Biashara yangu.. Ahsante
Wewe tayari unabiashara mbili yani JUMLA na REJAREJA hapa tulikua tunawasaidia wenzako wawe kama wewe.

Wauze jumla na reja reja,Biashara yakufanya kwawewe sasa hivi ni kuongeza biashara nyingine sehemu zingine ila katika hiyo biashara yako kwasasa wee chapa zako kazi,ushamaliza.
 
We jamaa sometimes nahisi niwadeni kwako inatubidi nyuzi kama hizi tuwe tunalipia
Sina pesa za kugawa kama wafanyavyo wenye uwezo huo,ila kuna kitu naweza kukigawa for free mkuu na ni hichi ninachokifanya hapa boss kwahyo uwe na amani kabisa,take this as a gift.
 
Back
Top Bottom