Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Wazo liko vizuri mkuu, tatizo ni maandalizi na maandalizi ni hela mtaji wa kufanya hivyo, bila mtaji wa kutosha unarudi mtaani mapema tu, Huyu mwenye mtaji wa ndoo moja mbili anafanyaje?
 
Mwisho utatuambia tufuge kuku wenyewe ili tuwe tunapata mayai yakukaangia chips.

Mwisho utatuambia tuchome mkaa porini ili tupate mkaa wakupikia ubwabwa wakuuza.

Mwisho utatuambia tukalime viazi kwaajili ya kupikia chips.

Mwisho utawashauri na walevi wawe wananunua pombe kwa jumla.
 
Mkuu hii kudeal na mambo mengi unaweza kujichanganya mwenyewe.
Naamini kila biashara ina faida yake unapoifanya lakini pia kuna faida nyingi tu za kuspecialize kwenye kimoja ili kufanya vizuri kumudu ushindani.

Wewe uuze sabuni uuze mkaa na uwe na mgahawa tena katika eneo moja.
Baadhi ya wateja watakukimbia mazingira yako hayatakuwa masafi.
 
Fact [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji123]
 
Msaada. Mfano mimi nauza simu na vifaa vya simu Jumla na rejareja.. Nisaidie namna gani Ntafanya biashara ndani ya biashara yangu.. Ahsante
 
Mawazo mazuri but too much theoretical. Practically inaweza ikawa ngumu kwa mtu anayeanza biashara.. mfano uuze mitungi ya gesi huku unapika utajigawaje, or uajiri mtu kwa ajili ya kuuza gesi napo gharama zitaongezeka.

Huwezi napo ukauza mtungi mmoja wa gesi lazima utanunua mitungi mingi napo mtaji lazima uwe mkubwa. Kwa mtu ambaye ana mtaji mdogo sioni Kama itamsaidia kupunguza gharama.

Maybe ungeweka mifano hai kupitia kwa kwako au kwa mtu ambaye amefanya hivyo ukaweka mahesabu ya faida aliyoipata, utakuwa umesaidia watu.
 
Daah alafu ukute wewe ndo kichwa cha familia🤔🤔
Mkuu rizki ya mtu hupita mkononi mwa mtu, wewe komaa na biashara yako tu, iboreshe zaidi na zaidi.

Ila ukitaka kufanya biashara zote lazima ukwame tu, kama juniamini jaribu hiyo uone.

Binafsi nilianzaga na biashara ya stationary nilivokuwaga chuoni (arround 2005). Nikawa nakomaa sana kukaa mwenyewe weekend ili wasinipige, yes nilikuwa napata ila nilikuwa natumia nguvu saaana.

Zilichanganya pale nilipotoka kutafuta tenda na kuzileta ofisin kwangu, hela ilikuwa inaingia moja kwa moja mfukoni, natoa comission kidogo nabaki na ziada kubwa huku nikiwa na muda wa kutosha kufanya issue nyingine.

Yaani komaa kuboresha biashara yako tu ikikua zaidi ajiri vijana wapige kazi, we endelea kusimamia vzr zaidi na kuhuisha masoko
 
Mawazo mazuri but too much theoretical.
Unahisi naandika vitu kutoka kwenye kitabu cha ujasiriamali kilichoandikwa na prof wa udsm au udom?

unatamani mifano hai,unahisi bei nilizoweka hizo chache hapo ni Halisi au nimebuni buni?

unahisi naandika copy n paste kwa unavyofikiri mkuu wangu?

Unahisi nilivyoandika hapo ni mawazo tu yakufikirika ila hayafanyiki au hayawezekaniki? si eti mkuu wangu?!

Nani alikwambia Kuuza gesi lazima uanze na mitungi mingi kama unavyosema?

Nimelenga wenye mitaji midogo ndio,ukiskia biashara ya gesi si kwamba lazima uwe na malaki ya pesa,ukisikia biashara ya viazi si lazima uwe na malaki ya pesa?

Unajua Gunia la viazi lipo la ujazo wa aina ngapi? na kila gunia 1 linauzwa kwa kiasi gani? Unahisi hilo gunia mfanyabiashara hatoweza linunua?

Ukija kwenye mkaa,unajua mkaa unawekwa kwenye magunia ya ujazo tofauti tofauti? unajua kila gunia lina bei yake tofauti? au ukiskia mtu anauza mkaa kwa jumla unatengeneza picha ya mtu mwenye stooo ya magunia 100 kwenda mbele??

Usifanye mambo kuwa magumu sana mkuuu kuna vitu huitaji kutumia nguvu nyingi sana,Neno JUMLA lisikutishe ukaliogopa, Unaweza ukawa na mtaji wa 50k na ukauza bidhaaa flani kwa jumla,inategemea na uvumilivu wako ktk hiyo biashara na malengo yako uliyojiwekea..

Natamani kukupa mifano hai ili unifahamu japo kidogo maana ulitaman mifano hai ila kwakua tuko JF tunachat kirobot robot,hilo tuliache kwasasa ila nakwambia tu kitu mkuu Usitishike na neno JUMLA ni neno la kawaida sanaaaaaaaaaaaaaa.....
 
Msaada. Mfano Mimi Nauza simu na vifaa vya simu Jumla na rejareja.. Nisaidie namna Gani Ntafanya Biashara Ndani ya Biashara yangu.. Ahsante
Wewe tayari unabiashara mbili yani JUMLA na REJAREJA hapa tulikua tunawasaidia wenzako wawe kama wewe.

Wauze jumla na reja reja,Biashara yakufanya kwawewe sasa hivi ni kuongeza biashara nyingine sehemu zingine ila katika hiyo biashara yako kwasasa wee chapa zako kazi,ushamaliza.
 
We jamaa sometimes nahisi niwadeni kwako inatubidi nyuzi kama hizi tuwe tunalipia
Sina pesa za kugawa kama wafanyavyo wenye uwezo huo,ila kuna kitu naweza kukigawa for free mkuu na ni hichi ninachokifanya hapa boss kwahyo uwe na amani kabisa,take this as a gift.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…